Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,139
Woman eating cake

CHANZO CHA PICHA,EPA
Watafiti nchini Ufaransa wanasema kuna uhusiano kati ya vyakula vilivyosindikwa na maradhi ya saratani.
Watafiti hao wameainisha vyakula ikiwemo keki,kuku na mikate kuwa vinasindikwa sana.
Utafiti uliofanywa kwa watu 105,000 umeonyesha kuwa vyakula hivyo huliwa zaidi, hivyo wako hatarini kupata saratani.

Tahadhari nyingi zimetolewa lakini wataalamu wanasema kuzingatia lishe bora ni bora zaidi.

Mambo kumi unayoweza kufanya kupunguza hatari ya kuugua saratani:​

  • Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote
  • Hakikisha nyumbani kwako hamna moshi
  • Kula chakula chenye afya
  • Kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani
  • Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV
  • Epuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo.
  • Punguza uchafuzi wa hewa ndani na nje ya nyumba
  • Jishughulishe kuupa mwili mazoezi
  • Punguza unywaji wa pombe
  • Jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.
Lishe bora imefahamika kuwa inaweza kupunguza hatari ya kuugua saratani.
Kuwa na uzito mkubwa ni moja ya sababu kubwa baada ya uvutaji wa sigara, Shirika la Afya duniani limesema nyama ya kusindika inaongeza kidogo hatari ya kupata saratani.

Wanasayansi kutoka chuo kikuu Sorbonne jijini Paris walifanya utafiti kufahamu vyakula ambavyo watu hupendelea kula, ambapo Wanawake wa makamo walikuwa wakifuatiliwa kwa miaka mitano
Supermarket-sliced loaves and fresh bread from a bakery

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Je, aina ya mkate unaokula waweza kuleta utofauti ya hatari ya kupata saratani?

Matokeo kutoka jarida la kitabibu la nchini Uingereza yanaonyesha kuwa ikiwa kiasi cha vyakula vilivyo sindikwa sana vitaongezeka kwenye mlo kwa 10% basi idadi ya ongezeko la ugonjwa litafikia 12%

Hali ya Ugonjwa wa Saratani ukoje Afrika Mashariki?​

Nchini Kenya, ni ugonjwa wa pili unaochangia vifo vya watu baada ya magonjwa ya moyo.
Licha ya kuidhinishwa kwa baadhi ya malipo ya matibabu katika bima ya kitaifa ya afya nchini, bado tatizo lipo kutokana na kutowepo kwa taasisi za kutosha za umma zinazotoa huduma hizo - na kwa chache zilizopo, hazina vifaa vya kisawasawa.
Ni wachache wanaoweza kumudu gharama kubwa katika hospitali za kibinafsi.
Saratani

CHANZO CHA PICHA,SCIENCE PHOTO LIBRARY
Tanzania hali sio tofauti sana, wakati kunashuhudiwa uhaba wa vituo vya kutibu wagonjwa wa saratani - kuhudumia idadi jumla ya zaidi ya watu milioni 50 nchini .
Takwimu zinaonyesha kuwa saratani ya mfuko wa uzazi ni chanzo kikuu kwa wanawake wanaougua saratani Tanzania.
Kwa mujibu wa taasisi ya habari kuhusu kirusi cha HPV na saratani #ICO - tofauti na saratani nyingine, saratani ya mfuko wa uzazi inaweza kutambuliwa na kuzuiwa kabla ishike kasi na kusamabaa kwa ukubwa.chanzo.BBC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom