Ulitumia njia ipi kumwacha ex wako?

Au ulikuwa na mashauzi sana ? maana nanyi mkishatongozwaga na kuambiwa mnapendwa basi huwa mnadhani hakuna mwanamke mwingine mzuri zaidi yenu.

sijui nani kawaloga. Ukishasifiwa tu mzuri na ukiwa na kitako ndio basii .badilikeni mtaachwa sana msipokuwa makini.
Mi wa kwangu alileta hizo za kujiona mzuri sana na kunikalia kichwani nilipomwambia tuachane akaleta Swagg za kunywa sumu... Nilikonda penzi nililiona chungu kama sifongo nikamtelekeza kimya kimya
 
Kaka sipo hivo kabisa yaan,nilikuwa namuheshim mno, nimemsaidia mengi, sijui kuringa wala kuonyesha zarau mim ni mpole ukiniona utafikir no mlokole aliyeshika dini, mim sio muongeaji, unaweza nikera na nikacheka,
Hongera sana, na hata uandishi wako na maneno yako inaonyesha ulivyo na upendo na huna makuu. Lakini amini Mungu ni mwema, utakuja kumpata shemeji mwingine mwenye mapenzi ya dhati na ukamsahau huyo engineer wa kipare. Hakika amini maneno yangu, zidi kuomba na sifa za utukufu umpe Aba/Mungu wa kweli...atajibu tu maombi dada yangu.
 
Jamani natoa ushauri nasaha kwa vijana,wanaotafuta wachumba,walioko kwenye mahusiano wanataka kufanya malengo ya ndoa....nimejikita kwenye counseling with youth,pia kama una matatizo ya kifamilia,una stress,au matatizo mbali mbali...yanayokuumiza kichwa yanakunyima raha,,unatamani kuacha kutumia pombe au vilevi vngine kama dawa za kulevya,bangi nitafute kwenye namba hyo,
 
Sasa una mtu mwengine, au naweza pata fulsa ya kuondoa upweke
Naona unawahi fursa mapema! we sio wa mchezo mchezo

Lakini huyo ni binti wa kirombo sio mmachame, mmarangu wala wa kishumundu. Binti wa kirombo ni jembe la ukweli na huwezi kumpata kirahisi hivyo mkuu!
 
As
Naona unawahi fursa mapema! we sio wa mchezo mchezo

Lakini huyo ni binti wa kirombo sio mmachame, mmarangu wala wa kishumundu. Binti wa kirombo ni jembe la ukweli na huwezi kumpata kirahisi hivyo mkuu!
Asante kwa kumpa taarifa,anafikir sisi warombo in wapenda dezo eeeh
 
Mimi wangu alinipenda sanaa nilimpenda sanaa niliitwa majina yote mazuri lakini siku zilivyosonga akaona sina mademu nikawa committed na alivyo mbali taratiibu akaanza jibinua nikaanza kubinya nje yale mapenzi yaliyokuwepo nikaanza pungua simu alikuwa anapiga hata mara 5-6 kwa siku na nikitoka kazini hata masaa mawili huisha tunaongea tatizo akikosea hajui neno samahani hivyo nilichomfanya simu asipopiga simtafuti nimepunguza mawasiliano 95% kwa siku tunaongea mara moja au mbili na hata sekunde 30 hazifiki....miezi miwili iliyopita nime upgrade job ndo anapagawa akawa mpole ataomba msamaha lakini hakuna mapenzi tunasogeza siku tu nakuogopa marafiki & dada zake maana walinikubali nilivyomjali lakini demu anamatusi,haambiliki lakini ukimwambia tuachane anasema haji kupata mwanaume wakumpenda km mm lakini mwisho wa mwezi akija ndo basi mawasiliano ni F
 
Hivi kwa wale ving'ang'anizi wenzangu huwa mnatumia njia Gani? Yaani kila ukibadili namba anaitafuta na kupiga tena kuomba msamaha,huwa mnafanyaje nami ni mjanga wa hili aisee.
 
Nilimuacha kmyakmya alipga simu miez zaid ya mitat had numb ya baba akampgia mim nimekula tu mute
 
Mimi nilimuacha kwa kumuita na kumueleza "face to face" kama wasemavyo watoto wa malikia.

Binti alikuwa mrembo haswa akipita mtaani kama wewe ni dume la mbegu udenda lazima ukutoke,tabia yake kubwa hakuwa muaminifu.Baada ya kupata habari za mtaa wa sita juu yake nilifanya uchunguzi na kujilisha kuwa yanayozungumuzwa ni ya kweli,japo alikuwa muigizaji mzuri akidai yuladhi kufa mimi.


Hivyo nilimuita nikamjuza kuanzia leo mwisho wa mahaba yetu na hasira zilipo zidi nusura nimufanyie kitu cha Is.Lakini nachokikumbuka kwake ni tabasamu lake na utamu wake usioelezeka.
 
Back
Top Bottom