Kutoka Mahakamani - 15 Septemba, 2026: John Heche aendelea kutoa ushahidi

Kutoka Mahakamani - 15 Septemba, 2026: John Heche aendelea kutoa ushahidi

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,176
Reaction score
58,287

Shahidi John Heche tayari amewasili mahakamani, ni siku nyingine tena tunaendelea kupambana na kesi ya uhaini ya Mh. Tundu Lissu aliyopewa na Jamhuri

Kaa tayari kwa updates


=======

Leo September 15, 2026

Last time tuliishia Sehemu ya 417

Sehemu ya 418

Majaji wameingia muda huu hapa Mahakamani na sauti ya high Courtttttttttt kali imepigwa na leo imepigwa tena na Mwanadada.

Anasimama Karani wa Mahakama kusoma namba ya kesi.

Anasimama wakili wa Serikali Ajuaye Zengeli akiwa na wenzake Katuga, Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Mbiringe na Winniwa anasema wapo tayari kuendelea.

Mhe. Lissu nae anasema yupo tayari.

Shahidi namba 5 tayari yuko kizimbani

Jaji Ndunguru anamkumbusha Shahidi kwamba yupo chini ya kiapo.

Anasimama Katuga kwa ajili ya kuendelea na cross examination

Katuga: Shahidi habari ya asubuhi

Heche: Salama

Katuga: Ni ushahidi wako kwamba Mshtakiwa alisema na kuweka msimamo kwamba hatuko tayari kushiriki kwenye chaguzi za namna hii ambayo matokeo yake ni mauaji

Heche: Huo msimamo uliwekwa na Kamati Kuu ya Chama

Katuga: Ni sahihi kuwa msimamo ulikuwa kutokushiriki uchaguzi wa namna hiyo mpaka mabadiliko yafanyike?

Heche: Sahihi

Katuga: Uliiambia Mahakama hii kuwa Lissu alipokuwa akipita kwa wadau hakusema neno kuhamasisha uasi

Heche: Sahihi

Katuga: Kama kutakuwa na shahidi akasema kuwa Lissu alitumia neno uasi wakati anapita kwa wadau

Heche: Niulize ushahidi wangu nitakujibu usiniulize ushahidi wa mtu mwingine ila majibu yangu niliyotoa ndo sahihi.

Katuga: Ni ushahidi wako kwamba maneno tutahamasisha uasi na wewe kusema kuwa hakutumia neno tutahamasisha uasi

Heche: Inategemeana na context, Lissu alitumia maneno hayohayo inawezekana asitumie neno hilohilo ila context

Katuga: Katika ushahidi wako ulisema vyombo vya habari havitoi nafasi sawa

Heche: Sahihi

Katuga: Ulisema hii inatokana na mapungufu ya mfumo wa uchaguzi

Heche: Sahihi

Katuga: Katika ushahidi wako uliiambia Mahakama ni sheria ipi au mapungufu gani ya mfumo wa uchaguzi yanayopelekea upendeleo?

Heche: Nilieleza

Katuga: Ulieleza ni Sheria gani inayozuia waandishi au kuelekeza waandishi watoe habari za huyo na kuacha za yule?

Heche: Vyombo vya habari huwa vinafungiwa wakati wa uchaguzi, nchii hii imejaa impunity sheria hazifuatwi.

Katuga: Shahidi jibu swali au unataka nikubembeleze?

Heche: Kabembeleze mke wako

Katuga: Ni ushahidi wako kuwa mawakala wamekuwa wakipata usumbufu, procees inakuwa inacheleweshwa na kuzuiwa au kucheleweshewa viapo

Heche: Ni sahihi

Katuga: Ulitaja kuwa ni kituo fulani na kituo fulani?

Heche: Nilisema ni nchi nzima

Katuga: Unajua au hujui kuwa uliposhinda uchaguzi ulituhumiwa kuingiza kura feki mpaka ukashinda uchaguzi?

Heche: Hilo unaniambia wewe mimi sijui

Katuga: Unajua au hujui kuwa mwanasiasa akishindwa huwa hakubali kirahisi?

Heche: Sisi ni chama cha demokrasia ukishindwa unaenda nyumbani.Katuga: Waambie majaji kama kweli wewe uliposhindwa ulienda nyumbani?

Heche: Uchaguzi haukuwa huru na haki

Katuga: Kwahiyo unaiambia mahakama hii kuwa ukishindwa ukaenda nyumbani inategemea na aina ya Uchaguzi?

Heche: Uchaguzi ni aina moja tu na Mahakama ilishasema uchaguzi usiokuwa huru na haki sio uchaguzi

Katuga: Uchaguzi wa 2015 ulioshinda uliukubali au uliukataa?

Heche: Niliukubali japo ulikuwa na makosa mengi.

Katuga: Jimboni kwako uchaguzi ulikuwa huru na haki?

Heche: Haukuwa huru na wa haki wagombea wa udiwani walienguliwa.

Katuga: Unajua mahakamani hatuwi kama makasuku?

Heche: Wewe ndio kasuku

Katuga: Ni sahihi kama uchaguzi wa jimboni kwako haukuwa na haki, ulikuwa na uhuru wa kutokukubali kutangazwa au kukubali kutangazwa?

Heche: Nililazimisha kutangazwa na uchaguzi haukuwa huru na haki na nchi hii haijawahi kuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Katuga: Kama wewe ni mtu wa haki na sio pepepe ulikuwa na uwezo wa kukataa au kukubali kutangazwa??

Heche: Fafanua maana ya pepepe

Katuga: pepepe ni maneno ya mdomoni

Heche: Ok, sikuwa na uwezo wa kukataa kutangazwa maana wananchi walikuwa wananiunga mkono sana


Sehemu Part 419


Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche.

Katuga: Waambie Majaji kuwa wewe ulitangazwa katika uchaguzi usio huru na haki lakini haukuukataa.

Heche: Sahihi

Katuga: Ni sheria gani ya uchaguzi au yoyote ya nchi inayokulazimisha wewe ukitangazwa kwenye uchaguzi usiokuwa huru inakulazimisha usiukatae?

Heche: Ni wananchi, sheria siijui

Katuga: Wewe binafsi ukitangazwa kuwa mshindi, uchaguzi unakuwa sio wa haki?

Heche: Sio kweli

Katuga: Kwahiyo uliingia Bungeni kupitia uchaguzi usio huru na haki?

Heche: Sahihi kabisa

Katuga: Ukaserebuka

Heche: Kuna kuserebuka Bungeni? Watu kicheko

Katuga: Nilikusikia ulisema kuwa kuna Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi baadae akaenda kugombea jimbo la Butiama ?

Heche: Sahihi

Katuga: Hakuna mtu aliyewahi kufanya kazi Serikalini na baadae akajiunga na chadema?

Heche: Wapo

Katuga: Mtu yeyote aliyekuwa mtumishi wa umma, mfanyakazi wa Serikali nikisema kuwa atakuwa na haki ya kujiunga na Chadema?

Heche: Mtu akiwa mtumishi wa Umma halafu akajiunga na Chadema watamfukuza, ila akimaliza sawa

Katuga: Ni sahihi mtumishi wa umma akistaafu anahaki ya kujiunga na chama chochote?

Heche: Sahihi

Katuga: Ni sheria gani huyo mgombea wa Butiama aliyovunja yeye kujiunga na kugombea CCM?

Heche: Kwa utaratibu wa CCM huwezi kugombea kama hujawa mwanachama kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita kwahiyo alijiunga CCM akiwa Mkurugenzi wa Tume

Katuga: Ni sahihi kuwa msimamo wa Chadema ulimaanisha bila mabadiliko uchaguzi usogezwe mbele?

Heche: Ni sahihi

Katuga: Ulieleza sheria gani inaruhusu uchaguzi kusogezwa mbele?

Heche: Sikueleza

Katuga: Ni sahihi kuwa wewe Lissu na Lema mlienda Kenya kumuona Raila Odinga?

Heche: Ni sahihi

Katuga: Huko Nairobi mlimwambia Raila kuwa mnaenda kuzuia uchaguzi? Tunaenda kukinukisha?

Heche: Tulimueleza matatizo yote ya uchaguzi wa Tanzania

Katuga: Nina wasiwasi kama kweli ulipata division one

Heche: Una haki ya kuwa pia punguza hasira na wasiwasi japo na mimi nina wasiwasi sana na Degree yako ya Mzumbe

Jaji Ndunguru: naomba twendelee tukimaliza hapa mtaenda kulumbana huko nje

Watu: Kicheko

Heche: Waheshimiwa majaji tulizungumza mambo yaleyale ingawa hatukutumia exactly words.

Katuga: Taarifa zinazotolewa na Brenda ni wewe unamuelekeza atoe?

Heche: Ofisi ya Katibu Mkuu

Katuga: Uliulizwa na mshtakiwa kwamba yeye anashtakiwa kwa kuandaa mkutano na kutamka aliyoyatamka, wewe ukasema sio kweli

Heche: Sahihi

Katuga: Kabla hujaja kutoa ushahidi ulisoma hati ya mashtaka?

Heche: Niliisoma

Katuga: Waambie majaji kuna sehem imeandikwa Lissu anashtakiwa kwa kuandaa mkutano?

Heche: Nipe hati ya mashtaka niisome ila nakumbuka ameshtakiwa kwa mambo yaliyotokea kwenye mkutano

Katuga: Jibu swali

Heche: Sijui

Katuga: Ni ushahidi wako ulisema kuwa tuhuma za kualika waandishi wa habari sio sahihi na Sekretarieti ndio ilialika?

Heche: Sahihi

Katuga: Waambie majaji mshtakiwa anashtakiwa kwa kualika waandishi wa habari?

Heche: Sijui

Katuga: Waambie majaji kama Mwenyekiti Lissu alitaka au hakutaka hotuba yake ya 3/4/2025 alitaka iwafikie umma

Heche: Siwezi kujua kama alitaka

Katuga: Ni kweli au sio kweli kuwa 3/4/2025 kuna mambo ya ndani yalifanyika huku waandishi wa habari wakiwa wametolewa?

Heche: Sikumbuki

Katuga: Na ulikuwepo kwenye mkutano?

Heche: Mwanzo mwisho

Katuga: Mr Sikumbuki

Heche: Unataka nijibu majibu yako unayoyataka wewe, huku anacheka.

Katuga: Waambie majaji Lissu alikuwa na uwezo wa kukataa au hakuwa na uwezo wa kukataa kuongea na waandishi?

Heche: Sijui

Katuga: Lissu alikuwa na uwezo wa kukataa au kukubali kuongea na waandishi wa habari?

Heche: Secretariat haina uwezo wa kumlazimisha Mwenyekiti.

Katuga: Unafahamu au hufahamu kama kulikuwa na hotuba rasmi iliyokuwa imeandaliwa?

Heche: Aliyoandaa yeye au?


Sehemu ya 420

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche.

Katuga: Mikutano ya Chadema huwa inahifadhi minutes au haina minutes?

Heche: Sio yote.

Katuga: Nani alikuwa Mwenyekiti wa mkutano wa 3/4/2025?

Heche: Haukuwa na Mwenyekiti

Katuga: Nani alikuwa mzungumzaji mkuu kwenye huo mkutano

Heche: Mwenyekiti wa Chama Taifa

Katuga: Wewe uliongea kwenye huo mkutano?

Heche: Ndio, niliongea.

Katuga: Muda gani?

Heche: Kama nusu saa hivi.

Katuga: Uliiambia Mahakama wewe uliongea nini?

Heche: Sikuiambia Mahakama maneno niliyoongea.

Katuga: Ulimsikia Mwenyekiti akisema tutazuia uchaguzi.

Heche: Ndio

Katuga: Ulimsikia Mwenyekiti akisema tutauvuruga huu uchaguzi

Heche: Nilisikia

Katuga: Ulimsikia Mwenyekiti akisema tutahamasisha uasi

Heche: Aliongea mengi maana ulikuwa mkutano wa zaidi ya masaa 3

.Katuga: Ulimsikia Mwenyekiti akisema tutakinukisha vibaya sana

Heche: Alisema na mengine mengi sio hayo tu ambao umechagua wewe kuyatumia kufungua kesi.

Katuga: Ulimsikia akisema Majaji ni MaCCM

Heche: Alisema na akatoa ushahidi wa Majaji ambao ni Wanaccm akiwemo Jaji Augustino Ramadhani.

Katuga: Ulimsikia akisema Mahakamani hakuendeki

Heche: Alisema

Katuga: Ulimsikia akisema mapolisi huingia na vibegi vya kura feki

Heche: Alisema

Katuga: Unafaham mshtakiwa anashtakiwa kwa kesi ya kutoa taarifa za uongo mtandaoni katika mahakama ya kisutu

Heche: Najua anashtakiwa ila kosa silijui kwa ufasaha

Katuga: Unajua au hujui kuwa wakati wa hoja za awali Kisutu maneno kuwa Majaji ni MaCCM aliikataa

Heche: Sijui

Katuga: Unajua Ushahidi wako huu unaweza kutumika Kisutu?

Heche: Sijui

Katuga: Waambie Majaji kama Lissu aliwaambia njia za kuvuruga uchaguzi?

Heche: Hakutuambia Katuga: Waambie Majaji kama Lissu aliwaambia njia za kuzuia uchaguzi?

Heche: Hakutuambia

Katuga: Waambie Majaji kama Lissu aliwaambia njia za kuhamasisha uasi?

Heche: Hakusema

Katuga: Waambie Majaji katika ushahidi wako kama ulisema tuhamasishe uasi dhidi ya nani? Ulisema katika ushahidi wako in chief?

Heche: Nilielleza extensively, Tume ya uchaguzi na mifumo yote ya uchaguzi ndicho nilichoeleza, tatizo la Katuga anataka kunipandikizia majibu yake

Jaji Ndunguru: Katuga usimpandikizie majibu

Katuga: Ni ushahidi wako uasi ni dhidi ya Tume ya Uchaguzi?

Heche: Sahihi

Katuga: Ni kweli Polisi walihusika katika ulinzi wa Mkutano Mkuu ambao wewe na Lissu mlichaguliwa?

Heche: Sijui

Katuga: Waambie majaji kama Polisi waliingiza kura ili ushinde

Heche: Uchaguzi wa Chadema? Hawakuingiza kura ili nishinde.

Katuga: Kwa mujibu wa Sheria ni nani anahusika kutangaza tarehe ya uchaguzi Mkuu?

Heche: Tume ya Uchaguzi

Katuga: Unajua au hujui kuwa Katiba, inaeleza kuwa Tume ya Uchaguzi kutokuingiliwa na mtu yeyote wakati inafanya majukumu yake?

Heche: Tume ipi? Katiba inasema Tume ya Uchaguzi na kuna Sheria inatambua Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

Katuga: Tume iliyopo kwenye katibaHeche: Haipaswi ila imekuwa ikiingiliwaKatuga: Ni Ibara ya ngapi ya Katiba?

Heche: Ibara ya 74

Katuga: Ni kweli Chadema inaamini Demokrasia?

Heche: Sahihi kabisa

Katuga: Ni sahihi kuwa No Reforms No Election ni msimamo wa Chadema

Heche: Sahihi kabisa Katuga: Unajua Chadema ina haki ya kushiriki au kutokushiriki uchaguzi mkuu?

Heche: Najua ndio

Katuga: Unajua kuna vyama vingapi vilivyosajiliwa?

Heche: Vipo 19 Vingine ni majina tu, Vyama serious havizidi viwili.

Katuga: Nani kakuuliza userious hapa?

Heche: Wewe.

Katuga: Unajua au hujui kuwa vyama vingine vinamsimamo wake kuhusu uchaguzi?

Heche: Inawezekana

Katuga: Unajua kuwa Uchaguzi Mkuu upo kwa mujibu wa Katiba?

Heche: Uchaguzi huo lazima uwe HURU na wa HAKI ndio unakuwa kwa mujibu wa Katiba kwahiyo najua.


Sehemu ya 421

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche

Katuga: Kwa vile ni Haki Chadema kutokushiriki Uchaguzi kikatiba, ni haki vilevile vyama vingine kushiriki uchaguzi mkuu.

Heche: Uchaguzi ambao ni batili sio haki, ila uchaguzi huru na haki ni sawa

Katuga: Kwenye Katiba ni wapi imeandikwa kuwa uchaguzi batili sio haki kushiriki

Heche: Ibara ya 27(2) inaruhusu kupiga vita matumizi mabaya ya mali za umma ikiwemo Uchaguzi usio huru na haki

Katuga: Unajua mshtakiwa anashtakiwa na aina gani ya uhaini?

Heche: Kuchapisha maneno kwa nia ya kuitishia Serikali

Katuga: Unajua ama hujui kwamba mshtakiwa ameshtakiwa kwa kutoa na kuchapisha maneno kwa nia ya kuitishia Serikali

Heche: Najua

Katuga: Kwenye haya maneno kuna neno kuitishia serikali au kwa nia ya kuitishia Serikali?

Heche: Naomba hati ya mashtaka niisome, neno ni nia ya kuitishia serikali

Katuga: Kwa maana ya hiyo hati ya mashtaka Serikali kutishika au nia ya kutishia serikali ni kiini au sio kiini?

Heche: Kiini maana yake ni nini? Kiini cha yai au???

Katuga: Leo hujui viini?

Katuga: Jana majaji uliwaambia kuwa kwenye ile video tuliyokuonyesha picha ilikuwa ya kwako au sio ya kwako?

Heche: Sasa kama video sio yangu picha inakuwaje ya kwangu?

Katuga: Kwa mujibu wa hati ya mashtaka kutishika au kutokutishika kwa Serikali sio kigezo cha kosa la uahini?

Heche: Sijui

Katuga: Baada ya Mwenyekiti wako kufunguliwa hii kesi, wewe uliendeleza nia ya kuzuia uchaguzi

Heche: Msimamo wa Chama chetu uko palepale tangu 2024 msimamo wetu ni No reforms, No election.

Katuga: Unakumbuka kuwa kupitia vyombo vya habari ulisema uchaguzi wa 2025 hautafanyika na kwamba mko determined?

Heche: Sikumbuki.

Katuga: Ni kweli au sio kweli katika kuzuia Uchaguzi mlikutana na viongozi wa dini?

Heche: Ni kweli.

Katuga: Uliwahi kutoa tamko kupitia East African radio kuutangazia umma kuwa uchaguzi wa 2025 hautafanyika?

Heche: Nimeenda mara nyingi sana sikumbuki hicho unachokisema.

Katuga: Kwa vile hukumbuki uko tayari kukumbushwa kupitia hiyo video?

Heche: Msimamo wangu ni kama jana tu kuwa sipo tayari kwasababu unaweza kuwa umetengeza na kusingizia watu kesi.

Katuga: Nikisema kuwa hauko tayari kwasababu unajua ukweli wake nitakuwa sahihi?

Heche: Siko tayari kwasababu wewe unaleta vitu feki.

Katuga: Kwa ridhaa ya mahakama naomba kumuonyesha shahidi video

Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji upande wa mashtaka hauko peke yao kwenye kesi hii. Naomba wakili wa serikali asiruhusiwe kumkumbusha shahidi kwasababu shahidi ndio anayepaswa kuomba kukumbushwa maneno aliyoyasema au kuandika kabla, hii ndio effect ya Kifungu cha 177 cha Sheria ya Ushahidi. Waheshimiwa Majaji, kama Upande wa mashtaka unataka kutumia hicho walichonacho to cross examine shahidi lazima wafuate utaratibu wa kifungu cha 63 kama ilivyoelezwa kwenye kesi maaeufu ya Lilian Fortes. Hivyo maombi yao hayana msingi wa kisheria.

Jaji Ndunguru: Anajadiliana na majaji wenzake kwa muda kadhaa kama dakika 7 ngoja tuone wataamua nini. Jaji Ndunguru anawauliza upande wa mashtaka mnasemaje?

Katuga: Tumesikia pingamizi la mshtakiwa. Kinachoendelea sasa ni cross examination na umuhimu wake uko chini ya kifungu cha 164 cha Sheria ya Ushahidi ambacho kinazungumza kuhusu kumjua shahidi na kingine to shake credibility ya witness.

Kifungu cha 156 cha Sheria ya Ushahidi ndio kinaeleza kuwa examination in chief ndio lazima ijikite kwenye relevant facts sio kwenye cross examination. Shahidi amesema hakumbuki na hataki kukumbushwa, Kwahiyo kifungu cha 177 hakina relevance.



Sehemu ya 422

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche Katuga anaendelea kusema Waheshimiwa Majaji Shahidi huyu huyu aliomba Mahakama akumbushwe kuhusu nyaraka na alikumbushwa.

Sisi cross examination yetu inahusu nyaraka ambazo sisi tunazo na jana tulimuhoji kuhusu card za magari na hakukuwa na pingamizi, kifungu cha 177 sio applicable hapa. Pia waheshimiwa Majaji utaratibu huu mliishautolea maamuzi jana kwahiyo hamuwezi kutoa uamuzi mara mbili kutakuwa na contradiction. Hata wakati wa in chief shahidi alionyeshwa ripoti kadhaa na alizizungumzia.

Waheshimiwa Majaji utaratibu huu tumekuwa tukiutumia katika practice kwahiyo tunaomba turuhusiwe tuendelee na cross examination

Lissu: Waheshimiwa Majaji hoja za wakili wa serikali hazina msingi, anasema wanatumia kifungu cha 164 cha Sheria ya Ushahidi, hakiruhusu kufanya wanachotaka kufanya, kifungu kinazungumzia maswali halali wakati wa cross examination, hakizungumzii namna ya kumkumbusha shahidi on his previous statement. Ukitaka kumkumbusha shahidi on his previous statement be it electronic or document unaenda kwenye section 177, hoja ya wakili wa Serikali is completely out.

Wakili wa Serikali amesema anatumia section 156(2) kuwa anaweza kuuliza swali lolote, hii sio hoja, hoja ni kwamba hauwezi kumkumbusha shahidi under 156(2), ukitaka kumkumbusha shahidi unaenda 163 or 177 hivyo hicho anachoataka kukifanya ni completely dissallowed.

Wakili wa Serikali amesema hiki kilifanyika jana hakukuwa na objection, na kuwa mahakama ilitoa uamuzi jana. Sasa kama anasema hakukuwa na objection sasa ruling ilitokana na nini? Jambo kama hili halikuwepo jana na hakukuwa na ruling Wakili wa Serikali amesema ni practice na sio sheria. Waheshimiwa majaji it is a matter of law na sio practice.

Relevant provisions ni Section 177 au 163 of the Evidence Act kwahiyo sio suala la practice it is a matter of law

Jaji Ndunguru: Tume pitia hoja zote, kifungu cha 177 hakisemi kuwa shahidi ataomba kukumbushwa, hivyo ni sahihi kumkumbusha ili ajibu hivyo tunaelekeza shahidi akumbushwe.

Katuga: anasimama na kuplay video ya east Africa Radio

Katuga: Hicho ulichokisia kina ushahidi wowote unaofana na ushahidi ulioutoa jana?

Heche: Kwenye eneo gani?

Katuga: Ni kweli kuna ushahidi wa kuonana na viongozi wa dini?

Heche: Sahihi

Katuga: Ni kweli nyaraka inasema kwamba mtaonana na watu mbalimbali

Heche: Inasema hivyo

Katuga: Ni kweli kuna maneno mtaonana na viongozi wa dini?

Heche: Ni kweli

Katuga: Ni kweli kuwa huwa unaenda kuzungumza East africa radio?

Heche: Mara nyingi sana

Katuga: Ni lini ulizungumza hayo uliyoyasikia kwenye video?

Heche: Sikumbuki

Katuga: Ni kweli jana ulisema ulisikiliza hotuba ya jaji chande?

Heche: Nilisikiliza

Katuga: Ni kweli hotuba hiyo ilisema kwamba vurugu za Oktoba zililenga kuzuia uchaguzi?

Heche: Sikumbuki eneo hilo

Katuga: Ni kweli hotuba ya Chande ilisema kwamba vurugu zilitokana na madai ya wanasiasa ya muda mrefu

Heche: Sikumbuki

Katuga: Unakumbuka Jaji Chande alisema kuna askari 16 waliuwawa

Heche: Sikumbuki najua tu watu waliuwawa

Katuga: Ni kweli hotuba ya Chande ilisema vurugu za Oktoba 29 zilipangwa na kuratibiwa?

Heche: Nilimsikia

Katuga: Kwenye video kuna maneno uchaguzi hautafanyika? Heche: YapoKatuga: Kuna maneno mko determined?

Heche: Yapo.

Katuga: Kwa uelewa wako kati ya Kanuni ya Adhabu na Katiba ipi inatengeneza makosa ya Jinai?

Heche: Mimi sio Mwanasheria

Katuga: Ulipokuwa unasema unajua je?

Heche: Usiongee na mimi kama mtoto wako, stop harrassment.

Jaji Ndunguru: Twendeleee.

Katuga: Ulipokuwa unajibu wakati wa inchief ulijua ni kwa sheria ?

Heche: Nilisema kwa ufahamu wangu

Katuga: Ni kweli ulitaka Tume ndio iwe na mamlaka ya kupanga majimbo.



Sehemu ya 423

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche

Heche: INEC sio huru, Tume ambayo inateuliwa na mgombea wa CCM inakuwaje huru? Nilisema Tume Mpya itakayoundwa na iwe huru, usije na majibu yako

Katuga: Nani anayepanga majimbo ya uchaguzi?

Heche: Mchakato unaanza kwenye halmashauri.

Katuga: Soma Ibara ya 75(3)?

Heche: Anasoma.

Katuga: Wasomee majaji Ibara ya 75(4)?

Heche: Anasoma kuwa ni Tume inaweza kupanga majimbo kulingana na idadi ya watu.

Katuga: Ni kweli kwenye hizo ibara Tume inaweza kugawanya majimbo kwa kuzingatia idadi ya watu?

Heche: Hicho ni mojawapo tu ya kigezo.

Katuga: Ni Haki au sio Haki kwa mtu yeyote aliyesikiliza Hotuba ya Mwenyekiti kuchagua njia yake kutafsiri hotuba ya Mwenyekiti?

Heche: Sijui

Katuga: Ni haki au sio haki kwa mtu yeyote aliyehamasika na Hotuba ya Mwenyekiti kuchagua njia yake kutumia njia yoyote kuuvuruga uchaguzi?

Heche: Sijui

Katuga: Ni haki au sio haki kwa mtu yeyote aliyesikiliza hotubu ya Mwenyekiti kuchagua njia yake kukinukisha?

Heche: Sijui

Katuga: Kuchoma vituo vya kupigia kura na vifaa vyake ni njia ya kuzuia uchaguzi?

Heche: Sio njia

Katuga: Waambie majaji kuchoma mwendokasi, vituo vya mafuta kunaweza kuvunja amani

Heche: Sijui

Katuga: Waambie Majaji siku ya kupiga kura kama kuna fujo ambayo haiwezi kuzuiwa inaweza kuzuia upigaji kura?

Heche: sijui

Katuga: Waambie majaji kama kukata watu vidole waliojitolea kupiga kura kunaweza kuwatisha watu wengine wasiende kupiga kura

Heche: Sijui

Katuga: Halafu wewe unajiita shahidi?

Heche: Ndio ni shahidi, Wewe ni wakili muongo unayebambikia watu kesi za uwongo.

Katuga: Uliwaeleza majaji katika ushahidi wako kuwa mtazuia uchaguzi kwa njia gani?

Heche: Ndio, nilieleza kuwa tutatembelea viongozi wa dini.

Katuga: Kuzuia uachaguzi unakutana na viongozi wa dini?

Heche: Kwani uchaguzi unafanywa na mizimu? Si watu? Leo Katuga anakula za uso sana.

Katuga: Ni kweli au sio kweli kuwa kuchoma vituo vya kura ndio tafsiri ya uasi?

Heche: Sio kweli

Katuga: Uasi maana yake nini?

Heche: kupinga mifumo kandamizi, sheria mbovu na maovu yote katika nchi

Katuga: Vituo vya kupigia kura vinasimamiwa na nani?

Heche: Tume ya Uchaguzi

Katuga: Jibu tena ,

Heche: Nimeshasema, nimeshasema, nimeshasema.

Jaji Ndunguru: Tumemsikia shahidi akisema kuwa ni Tume ya Uchaguzi

Heche: Waheshimiwa Majaji ni ukorofi wa Katuga tu ili mnione mbaya lakini mimi sitakubali.

Hapa hadi Majaji wamecheka

Katuga: Ulisema jana hujawahi kuitwa kwenye Tume ya Jaji Chande?

Heche: Sikuwahi kuitwa

Katuga: Kuhusu chama chako kuitwa ulisema pia hamkuitwa?

Heche: Nilisema sina kumbukumbu kuhusu kiongozi wala chama kuitwa.

Katuga: Ni sahihi kuwa taarifa ya watu kuitwa ilichapishwa kwenye gazeti la Serikali?

Heche: Sijui

Katuga: Uliisikia Tume ikisema kuwa kuna watu wanawazuia wengine wasiende kusema walichoona siku ya Oktoba 29?

Heche: Sijui

Katuga: Unajua kuwa Tume ilikuita ukakataa kwenda?

Heche: Sikuwahi kuitwa.

Katuga: Ni sahihi kuwa Tume ilitangaza katika mbao mbalimbali kuita watu wakatoe ushahidi wa kile wanachokijua kuhusu matukio ya Oktoba 29?

Heche: Sijui

Katuga: Unaishi Tanzania au Kenya

Heche: Tanzania

Katuga: Kwa ridhaa ya Mahakama naomba nimuonyeshe shahidi nyaraka / barua alizoandikiwa na Tume.

Jaji Ndunguru: Sawa

Katuga: Hiyo ni nakala ya nini?

Heche: Ni barua

Katuga: Imeandikwa jina la nani?

Heche: John Wegesa Heche

Katuga: Kuna Makamu wangapi wenyeviti wa Chadema wenye jija hilo?

Heche: Yupo Mmoja tu anaitwa John Wegesa Heche

Katuga: Sanduku la Posta 31191 Dar es Salaam ni sanduku la nani?

Heche: Ni la Chadema

Katuga: Hiyo barua ni ya tarehe gan?

Hache: 21 December 2025

Katuga: Barua imesainiwa na nani?

Heche: Honorious J. Njole



Sehemu ya 424

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche

Katuga: Kichwa cha barua kimeandikwaje?

Heche: Kuwasilisha Ushahidi kwenye Tume kuhusu matukio ya Oktoba??

Katuga: Naomba nimuonyeshe barua ya pili

Jaji Ndunguru: sawa

Katuga: hicho ni nini?

Heche: Barua

Katuga: Ni ya tarehe ngapi?

Heche: Januari 2026

Katuga: Ilikuwa inaenda kwa nani?

Heche: John Wegesa Heche

Katuga: Barua hiyo imeandikwaje?

Heche: Wito wa kukutana na Tume ya Rais ya kuchunguza matukio kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025

Katuga: Imesainiwa na nani?

Heche: Honorious Njole

Katuga: Naomba nimuonyeshe shahidi barua nyingine ya mwisho

Jaji Ndunguru: sawa

Heche: Nimeiona

Katuga: Hiyo barua inatoka wapi?

Heche: Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29

Katuga: Ni ya tarehe ngapi?

Heche: 2 Januari 2026

Katuga: Addressee alikuwa ni nani?

Heche: Katibu Mkuu Chadema

Katuga: Barua hiyo ilikuwa inataka nini?

Heche: Kukutana na Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29.

Katuga: Hizo barua ungependa ziwe sehem ya ushahidi wako?

Heche: Hapana

Katuga: Unafahamu Tume ilitangaza kuwa mtu asiyetaka kwenda atume picha, nyaraka au video kuhusu hayo matukio?

Heche: Sijui

Katuga: Naomba nimuonyeshe nyaraka nyingine

Jaji Ndunguru: sawa

Katuga: Hiyo ni nini?

Heche: Taarifa kwa umma

Katuga: Inawaalika nini umma?

Heche: anasoma, ni kualika watu kutoa ushahidi kuhusu matukio ya Oktoba 29

Katuga: Njia gani zimetajwa?

Heche: Sms hata kwa WhatsApp, sms , email etc

Katuga: Wewe ni sehemu ya umma?

Heche: Mimi ni sehem ya umma

Katuga: Naomba nimuonyeshe nyaraka nyingine

Jani Ndunguru: sawa

Katuga: Hiyo nyaraka ni ipi?

Heche: Taarifa kwa Umma

Katuga: Imeandikwaje

Heche: Tume ya Uchunguzi

Mhe. Lissu: Hivi sasa ni saa saba kamili naba twende break

Jaji Ndunguru: amalizie hapo

Katuga: Taarifa hiyo ililenga kubainisha umma nini?

Heche: Anasoma kuwa kumekuwa na watu wanaowashawishi watu kutokushiriki kutoa taarifa kwenyw tume kuhusu matukio ya Oktoba 29……… “

Katuga: Ni kweli ulisema hamkuikubali Tume ya Jaji Chande

Heche: Ni sahihi

Katuga: Je Tume mliipa ushirikiano?

Heche: Unampaje mtu ushirikiano bila kualikwa?

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji wakiwa wanafanya cross examination upande wa mashtaka wao wanaruhusiwa kuendelea tu?

Jaji Ndnguru: Amalizie swali la mwisho, au sawa tumekuelewa mshtakiwa

Jaji Ndunguru: Shauri linaahirishwa hadi 14:40 tunaongeza na dakika 5.

Inapigwa High Coooouuuuurrrrrttttt

Majaji wanasimama na kutoka.


Sehemu ya 425

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche

Katuga: Waambie Majaji kuhusu kama Chadema mlikuwa tayari kutoa ushirikiano kwenye Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29..?

Heche: Hatukuwa tayari kwasababu hatukualikwa

Katuga: Ni ushahidi wako kuwa hamkuikubali Tume ya Jaji Chande?

Heche: Ndio

Katuga: Kwa jibu lako kuwa hamkuwa mmeikubali Tume ya Chande nitakuwa sahihi nikisema hamkuwa tayari kuipa ushirikiano?

Heche: Sijui.

Katuga: Kwa jibu lako, ni kweli ulikuwa hujui kama Chadema mlikuwa tayari au hamkuwa tayari kutoa ushirikiano?

Heche: Ni kweli

Katuga: Ulipata wapi mamlaka ya kumjibu mshtakiwa kuwa Tume ya Chande haikuwaita?

Heche: Ni kweli haikutuita.

Katuga: Mihimili ya dola ni ipi?

Heche: Bunge, Serikali na Mahakama

Katuga: Unajua ni jukumu la serikali kusimamia sheria..?

Heche: Najua

Katuga: Unajua ni Serikali ndio ina jukumu la kumshtaki mtu yeyote aliyevunja sheria?

Heche: Ni sahihi

Katuga: Unajua Jukumu la kulinda amani limekuwa vested kwa Serikali…?

Heche: Najua

Katuga: Waambie Majaji kama unajua ama hujui kuchoma kitu cha mpira unakifanya kitoe harufu???

Heche: Inategemea kitu chenye harufu kitatoa harufu kama hakina harufu hakitoi harufu

Katuga: Waambie Majaji kuchoma matairi yanafanya yatoe harufu?

Heche: Sijawahi kuchoma matairi kwahiyo sijui.

Katuga: Unajua au hujui kuna njia nyingi za kukifanya kitu kinuke au kukinukisha?

Heche: Sijui

Katuga: Unajua moja ya njia ya kukifanya kitu kinuke ni kukichoma???

Heche: Sijui

Katuga: Nilikusikia ukisema kuwa ulimsikia P17 yeye ndio alichapisha hotuba ya 3/4/2025.??

Heche: Niliskia

Katuga: Ulimsikia akisema kupitia wewe sisi tumechapisha?

Heche: Sikumsikia

Katuga: Unakumbuka au Hukumbuki kuwa P3 (PW13) alisema yeye alipanga kuzuia uchaguzi kwa kurusha mawe.

Heche: Sikumbuki

Katuga: Unapotisha kuvunja amani unakuwa unamtisha nani?

Heche: Sijui.

Katuga: Ulieleza kuwa kwenye hotuba ya Jaji Chande hakuna majina ya watu waliouwawa au waliokufa

Heche: Ndio

Katuga: Uliisoma hotuba ya jaji Chande?

Heche: Ndio niliisoma.

Katuga: Unajua au hujui taarifa rasmi ya jaji Chande ilikabidhiwa kwa Rais.

Heche: Najua alisema anamkabidhi na alisema ni ya kwake.

Katuga: Ushahidi wako ni kwa mujibu wa hotuba au taarifa rasmi?

Heche: Unatokana na hotuba na taarifa ile aliyoisoma.

Katuga: Unajua au hujui Chadema kupitia kwa Katibu Mkuu John Mnyika kilialikwa na kilishiriki kutoa maoni kuhusiana na mabadiliko ya sheria za uchaguzi

Heche: Najua.

Katuga: Unajua au hujui kuwa Kati ya mapendekezo ya Chadema ya kutowashirikisha watumishi wa umma kwenye uchaguzi kulipelekea Mabadiliko ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Uchaguzi

Heche: Hayo sio mapendekezo yetu, mapendekezo yetu yalikuwa juu ya mfumo mzima.

Katuga: Unajua au hujui kwamba mwaka 2024 kifungu cha 6 cha Sheria kilibadilishwa na kuondoa wakurugenzi kusimamia uchaguzi?

Heche: Najua kilibadilishwa na kusema watumishi waandamizi ndio watasimamia uchaguzi.

Katuga: Waambie Majaji kama uliiambia Mahakama hii kuwa tarehe 29 Oktoba 2025 ulikuwa mahabusu Mtumba.

Heche: Ndio nilikuwa mahabusu.

Katuga: Ulisema ulipotoka mahabusu uliambiwa na watu kuhusu vurugu zilizotokea na hotuba ya Chande?

Heche: Sahihi

Katuga: Huu ni ushahidi wako au kwa mujibu wa hotuba ya Chande?

Heche: Hotuba ya chande

Katuga: Ni sahihi ulisema kuwa kipindi hicho ndio watu wengi waliuwawa?

Heche: Ni kweli

Katuga: Ni sahihi kuwa mali zenye thamani nyingi zilichomwa?

Heche: Sikumbuki ila alisema zina thamani fulani.

Katuga: Ni sahihi kuwa mali nyingi sana ziliharibiwa?

Heche: Sina ufahamu

Katuga: Unajua kuwa 70% ya waliokamatwa baada ya vurugu za Oktoba 29, 2025 alisema kuwa walichocheka na hotuba zenu?

Heche: Sijui wewe ndio unaniambia

Katuga: Unamjua Katibu wa Chadema kata ya Mikocheni?

Heche: Simjui

Sehemu ya 426

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche

Katuga: Unamjua Katibu wa Chadema kata ya Mikocheni anaitwa Ishengoma?

Heche: Tuna kata zaidi ya 4,000 kwahiyo siwezi kujua

Katuga: Unajua kuwa huyu Katibu wa Chadema, Ishengoma alisema kuwa mlishiriki vurugu za Oktoba 29?

Heche: Sijui

Katuga: Ni sahihi Lissu asingealikwa kwenye mkutano wa Tarehe 03/04/2025 asingeongea?

Heche: Sijui

Katuga: Unajua maana ya constructive publication?

Heche: Sijui

Katuga: wewe ni shahidi wa nini kama kila kitu hujui?

Heche: Shida unakuja na majibu yako ya uongo.

Katuga: Ni sahihi ulitaja ripoti nyingi za nje kuhusu uchaguzi wa mwaka jana?

Heche: Sahihi

Katuga: Unajua kuwa opinion ya EU sio binding kwenye mahakama hii?

Heche: Najua

Katuga: Ulieleza kuwa umezilete hizo ripoti hapa mahakamani?

Heche: Sikueleza

Katuga: Njia ipi ulitumia kubadilisha jina kutoka Wegesa Charles Heche kwenda John Wegesa Heche

Heche: Kiapo na Deedpoll na zilitangazwa kwenye gazeti la Serikali

Katuga: Ni ushahidi wako kuwa kwenye kubadilisha jina ulitangaza kwenye gazeti la Serikali?

Heche: Ndio utaratibu

Katuga: Ila wito wa Tume ya Chande hukuona kwenye gazeti la Serikali

Heche: Kwani mimi naona magazeti yote ya serikali? ndio sikuliona hilo tangazo.

Katuga: Nilikusikia uliirejea taarifa ya Thabo Mbeki Foundation

Heche: Ni sahihi

Katuga: Unajua ama hujui kuwa sio Foundation ya kimataifa?

Heche: Mi najua ya kimataifa.

Katuga: Iko chini ya umoja gani wa kimataifa?

Heche: Mi najua ni ya kimataifa.

Katuga: Mwalimu Nyerere Foundation iko chini ya kimataifa?

Heche: Sijui.

Katuga: Unajua au hujui kama walichokitoa foundation ni maoni?

Heche: Ni maoni yao.

Katuga: Unajua au hujui kuwa Thabo Mbeki Foundation walichukua maoni kutoka UN na SADC?

Heche: Najua walichukua AU na SADC sio UN

Katuga: Unajua Thabo Mbeki hawakuwa waangalizi wa uchaguzi?

Heche: Nalijua hilo

Katuga: Kwa vile umesema ya Thabo Mbeki ni maoni, Je mahakama inapokea ushahidi wa maoni?

Heche: Sijui

Katuga: Waheshimiwa majaji naona mimi niishie hapa.

Sasa ni zamu ya Tundu Lissu kuuliza maswali ya Re Examination.

Part 427 itaendelea kwenye post inayofuata,

PART 427​


Mhe. Lissu ameanza kumfanyia Re-examination Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche.


Jaji Ndunguru:
Mshtakiwa, uko tayari? Na tunaamini utakuwa na maswali machache.


Mhe. Lissu: Niko tayari Waheshimiwa Majaji, ila inategemea na speed ya nyie kuandika pia, maana mimi ndiyo niko Gerezani kule, sio Sheraton Hotel Waheshimiwa Majaji.


Jaji Ndunguru: Bado una mashahidi watatu. Tutamaliza within time, mshtakiwa, maana tulitegemea Ijumaa mngewasilisha final submissions.


Mhe. Lissu: Kwanza hao mashahidi wangu nahitaji kuonana nao ili tupange mkakati wa kesi yetu.


Watu wamecheka sana mpaka Majaji, kuhusu Mkakati wa Lissu na mashahidi wake, yaani IGP Wambura, CDF Mkunda, na DCI Kingai. 😂😂😂


Tunaendelea na Re-examination


Mhe. Lissu:
Wakili Mwinuka alikuuliza yale matatizo yanayohusiana na fomu. Ulisema hukupata shida ya kuambiwa ulijaza fomu vibaya, ila ulisema ujazaji fomu ni moja ya kigezo.


Heche: Ni kweli nilisema suala la ujazaji fomu ni sehemu ya matatizo ya uchaguzi yanayotumika kuengua wagombea, hasa wa upinzani. Kuna wakati mtu anaambiwa CDM badala ya CHADEMA.


Wakili wa Serikali Mwinuka: Jibu la shahidi lina-attract sisi kuja kufanya cross examination. Yeye atoe tu clarification.


Mhe. Lissu: Fafanua bila kutoa mifano.


Heche: Kuna vigezo vingine vingi ambavyo vinatumika kuengua wagombea na vinatumika kwa wagombea wa upinzani tu, hasa Chadema.


Mhe. Lissu: Umejibu vizuri.


Mhe. Lissu: Uliulizwa kuwa kwa vile wewe hukuenguliwa na ulishinda, ukaulizwa kwa vile ulishinda, basi Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.


Heche: Uchaguzi niliochaguliwa haukuwa huru na haki kwa sababu kuna watu waliouwawa.


Wakili Mwinuka: Waheshimiwa Majaji, hii kwa sababu watu waliuwawa ina-attract nafasi ya sisi kufanya cross.


Mhe. Lissu: Hilo hapana, Wakili wa Serikali hayuko sawa sawa. Shahidi katika ushahidi wake aliulizwa kuhusu mauaji na alisema alishuhudia wakati wa kampeni kulikuwa na mauaji Nyamongo na alishuhudia.


Jaji Ndunguru: Endelea Heche.


Heche: Waheshimiwa Majaji, kampeni zetu ziliingiliwa na Polisi, watu waliuwawa, lakini pia hata Mawakala wetu walienguliwa.


Mhe. Lissu: Uliulizwa kama Makamu wa Rais alikuja wakati nikiwa Nairobi Hospital. Ulisema alikuja na alikuwa kwenye mkutano.


Heche: Ni kweli Makamu wa Rais alipoenda Nairobi kwenye kikao na baada ya kumaliza kikao ndiyo alienda kumuona Lissu Hospital.


Mhe. Lissu: Uliulizwa kama nilikupa jukumu la kufuatilia mafao yangu ya Hospital. Ulijibu sikukupa jukumu ila ulikuwa kwenye Kamati ya Chama ya matibabu yangu, fafanua.


Heche: Mhe. Lissu aliposhambuliwa iliundwa kamati na Chama na mimi nilikuwa sehemu ya kamati ya kufuatilia na hakulipwa.


Mhe. Lissu: Uliulizwa kama Chadema mlikuwa na imani na Tume ya Chande. Ulijibu hamkuiamini na tuliamini itaficha mauaji na kulinda walioua.


Heche: Ni kweli hatukuwa na imani kutokana na jinsi ilivyoundwa, kwahiyo tuliamini ingeficha ukweli wa kilichotokea na kusafisha watu waliohusika.


Mhe. Lissu: Shahidi, wakili Katuga alikuuliza kuhusu Tone tone na michango ya chama uliyopokea. Uliyajibu suala la michango ya chama sio la Makamu Mwenyekiti, fafanua.


Heche: Suala la michango yote ya chama linasimamiwa na Katibu Mkuu ambaye ni accounting officer na linapita kwenye account rasmi za kichama. Haiwezekani kwa vyovyote vile Makamu Mwenyekiti akahusika na michango ya chama.


Mhe. Lissu: Kwenye masuala hayo hayo ya pesa za michango, uliulizwa kuhusu Salman na Nilesh, na uliambiwa kwenye account yako umekewa 10M na 20M, ulisema huwajui.

Katuga: Jibu lilikuwa siwajua, kuna ufafanuzi gani? Sisi tunapinga kuanzia swali kwa sababu jibu litaleta majibu mapya.

Mhe. Lissu: Wakili wa Serikali anapaswa kujua kuwa kabla ya shahidi hajajibu, hapaswi kutabiri jibu. Hoja ni kwamba suala la 10M na 20M lilikuwepo, hivyo lazima liwe re-examined.

Jaji Ndunguru: Haya shahidi, fafanua.

Heche: Siwajua na sijawahi kuwaona.

PART 428 itaendelea kwenye post inayofuata.​


PART 428​


Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re-examination Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche.


Mhe. Lissu:
Ulionyeshwa video ukaulizwa kama ni wewe na kama hayo maneno yanaelekea kuwa ni ya kwako, na ukasema hukumbuki kutoa hotuba ya aina hiyo.


Heche: Sikumbuki kutoa hotuba hiyo, wametumia akili mnemba kuitengeneza.


Mhe. Lissu: Fafanua Akili Mnemba.


Watu kicheko 😂😂😂😂


Heche: Akili Mnemba ndiyo Artificial Intelligence (AI).


Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu magari manne ya bei mbaya, ukasema una magari mawili, fafanua.


Heche: Nilimaanisha nina Prado na Hilux ambazo ndiyo huwa nazitumia, hiki ndiyo nilichomaanisha.


Mhe. Lissu: Unakumbuka kuhusu kukamatwa kwako nje ya Mahakama na kuwa unapelekwa Tarime? Uliulizwa ulienda Kenya? Ukasema nilizuliwa, fafanua.


Heche: Nilizuiliwa na Immigration kwenye mpaka wa Sirari.


Mhe. Lissu: Unakumbuka uliulizwa na mawakili wa Serikali kuhusu wewe kukutana nao Oysterbay Police na walisema kwamba 70% ya waliokamatwa walikutaja wewe kuwa unahusika na kuratibu wewe hizo vurugu, ukasema hujui, fafanua.


Heche: Nilikuwa ndani tangu tarehe 22 Oktoba 2025. Kwa vyovyote vile siwezi kuhusika na yaliyotokea Oktoba 29, 2025.


Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu matibabu yangu, hasa kuhusu matibabu nje ya nchi. Ulijibu kwamba wakili wa Serikali alikuwa sahihi nusu na sio sahihi nusu, fafanua.


Heche: Kuna mazingira ambayo Mbunge anaweza asifuate utaratibu wa kawaida, mfano mazingira kama ya dharula.


Mhe. Lissu: Uliulizwa ni lazima Mbunge mpaka apate referral kwenda nje ya nchi? Ukasema sio lazima apate referral.


Heche: Mbunge akiwa mahututi sio lazima apewe referral.


Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji, muda umeisha. Hivi sasa ni saa kumi na moja. Tunaomba ahirisho hadi kesho saa tatu kamili asubuhi.


Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji, huyu John Heche ndiyo shahidi wangu wa mwisho kwa ambao ni raia. Kwahiyo kesho tutamaliza sio zaidi ya lisaa. Kwahiyo naomba kesho mashahidi wengine waje ili niongee nao kujua namna tunavyoenda na ushahidi uliobaki.

Watu kicheko 😂😂😂😂😂😂

Jaji Ndunguru: Shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi. Shahidi bado hujamaliza kutoa ushahidi wako.


Imepigwa High Cooooouuuuuurrrrrtttt


Majaji wanatoka.


Tukutane kesho saa tatu kamili asubuhi ✌️
 
MAHAKAMA IMEANZA WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 1 TAREHE 15.9.2026.


Majaji wameingia Mahakamani pamoja na Lissu.

Mawakili wa Serikali wapo tayari.

Shahidi yupo tayari kwenye kizimba.

Karani wa Mahakama anajiandaa kusoma kesi Criminal Session, Kesi Namba 19605 ya mwaka 2025.

Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Anasimama Wakili Ajuaye. Waheshimiwa Majaji, iwafurahishe:

1. Nassoro Katuga – Wakili wa Serikali
2. Tawabu Issa – Wakili Mwandamizi
3. Job Mrema – Wakili wa Serikali Mkuu
4. Cuthbert Mbilinyi – Wakili wa Serikali
5. Winnie Kasara – Wakili wa Serikali

Mshtakiwa yupo kizimbani, anajitetea mwenyewe.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa Lissu?

Lissu: Nipo tayari.

Jaji Ndunguru: Shahidi?

Heche: Nipo tayari.

Nassoro Katuga: Habari za asubuhi.

Heche: Salama.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba ni msimamo wako kwamba Mshtakiwa ni msimamo wake kwamba hamko tayari kushiriki uchaguzi.

Heche: Huo msimamo uliwekwa na Kamati Kuu ya chama.

Nassoro Katuga: Ni wewe ndiyo uliiambia Mahakama?

Heche: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema kwamba msimamo ulikuwa kutokushiriki uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike?

Heche: Ni sahihi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHA ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA2.

Nassoro Katuga: Nakumbuka uliiambia Mahakama hii tukufu kwamba Bwana Lissu alipokuwa anapita kwa wadau hakutumia maneno “uasi”.

Ni ushahidi wako huo?

Heche: Kweli.

Nassoro Katuga: Kama ikatokea shahidi akasema kuwa alikuwa anahamasisha uasi, hizi shahidi mbili zipo sawa au hazipo sawa?

Heche: Hazipo sawa, Wajumbe.

Nassoro Katuga: Kwa ushahidi wako, maneno kwamba “tutahamasisha uasi” na wewe unasema hakutumia maneno “tutahamasisha uasi”, kwa ushahidi wako yapo sawa?

Heche: Anaweza asitumie neno moja, lakini context inaweza kuelekea katika jambo lilelile.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa, sijui kama jibu lake mmelipata.

Jaji Ndunguru: Anasema yote sawa.

Nassoro Katuga: Unakumbuka ulisema vyombo vya habari havitoi haki sawa kwa wagombea?

Ukionyesha sheria za uchaguzi na mifumo, hauko balanced.

Katika ushahidi wako umeiambia Mahakama ni sheria ipi au mfumo upi unafanya upendeleo?

Heche: Nilieleza.

Nassoro Katuga: Kama ulieleza, waambie Waheshimiwa Majaji ni sheria ipi inayozuia au kuelekeza waandishi wa habari watoe taarifa ipi na ipi wasitoe.

Heche: Sijui Mpaka nirefresh.

Nassoro Katuga: Nimesikia pia ukiwaambia Waheshimiwa kuwa kutokana na kutokuwa fair kwa sheria na mfumo mzima wa uchaguzi, mawakala wa wagombea wamekuwa wakipata usumbufu wa viapo au kuzuiwa kituoni.

Je, katika ushahidi wako umetaja kituo fulani?

Heche: Kwa nchi nzima.

Nassoro Katuga: Hivi unajua au hujui kwamba uliposhinda uchaguzi pia ulituhumiwa kufanya fujo na kuingiza kura feki?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Unajua au hujui kuwa mwanasiasa au mgombea akishindwa, kutokubali kirahisi matokeo?

Heche: Sisi watu wa CHADEMA ni watu wa haki, ukishindwa unaenda nyumbani.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA2.

Nassoro Katuga: Nakumbuka uliiambia Mahakama hii tukufu kwamba Bwana Lissu alipokuwa anapita kwa wadau hakutumia maneno “uasi”.

Ni ushahidi wako huo?

Heche: Kweli.

Nassoro Katuga: Kama ikatokea shahidi akasema kuwa alikuwa anahamasisha uasi, hizi shahidi mbili zipo sawa au hazipo sawa?

Heche: Hazipo sawa, Wajumbe.

Nassoro Katuga: Kwa ushahidi wako, maneno kwamba “tutahamasisha uasi” na wewe unasema hakutumia maneno “tutahamasisha uasi”, kwa ushahidi wako yapo sawa?

Heche: Anaweza asitumie neno moja, lakini context inaweza kuelekea katika jambo lilelile.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa, sijui kama jibu lake mmelipata.

Jaji Ndunguru: Anasema yote sawa.

Nassoro Katuga: Unakumbuka ulisema vyombo vya habari havitoi haki sawa kwa wagombea?

Ukionyesha sheria za uchaguzi na mifumo, hauko balanced.

Katika ushahidi wako umeiambia Mahakama ni sheria ipi au mfumo upi unafanya upendeleo?

Heche: Nilieleza.

Nassoro Katuga: Kama ulieleza, waambie Waheshimiwa Majaji ni sheria ipi inayozuia au kuelekeza waandishi wa habari watoe taarifa ipi na ipi wasitoe.

Heche: Sijui Mpaka nirefresh.

Nassoro Katuga: Nimesikia pia ukiwaambia Waheshimiwa kuwa kutokana na kutokuwa fair kwa sheria na mfumo mzima wa uchaguzi, mawakala wa wagombea wamekuwa wakipata usumbufu wa viapo au kuzuiwa kituoni.

Je, katika ushahidi wako umetaja kituo fulani?

Heche: Kwa nchi nzima.

Nassoro Katuga: Hivi unajua au hujui kwamba uliposhinda uchaguzi pia ulituhumiwa kufanya fujo na kuingiza kura feki?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Unajua au hujui kuwa mwanasiasa au mgombea akishindwa, kutokubali kirahisi matokeo?

Heche: Sisi watu wa CHADEMA ni watu wa haki, ukishindwa unaenda nyumbani.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Katuga ana-dribble
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 3.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo ukishindwa unaenda nyumbani?

Heche: Kwenye uchaguzi huru.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo ukishindwa inategemea na mazingira?

Heche: Nchi hii ina figisu nyingi.

Nassoro Katuga: Ulisema uligombea 2008 na 2015?

Heche: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Ule uchaguzi uliogombea 2015, wewe ukashinda, uliukubali au hukuukubali?

Heche: Niliukubali.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, huo uchaguzi ulikuwa huru na haki?

Heche: Haukuwa huru na haki.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kama wewe ni mtu wa haki na unasema uchaguzi haukuwa huru na haki, je, ulikuwa na uwezo wa kukataa (kutokubali) ushindi wako au ulilazimishwa?

Heche: Jimboni nilikuwa pia na Madiwani.

Jaji Ndunguru: Hajakuuliza Madiwani.

Nassoro Katuga: Kama wewe ni mtu wa haki, tuache pepepepe. Ulikuwa na uwezo wa kukataa kutangazwa mshindi wa uchaguzi ambao haukuwa huru na haki au ulilazimishwa?

Heche: Pepepepe ni nini kwanza ili nijue kujibu?

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba wewe ulitangazwa katika uchaguzi ambao haukuwa huru na haki, lakini hukuwa na jinsi.

Heche: Nilitangazwa kwa nguvu ya umma.

Nassoro Katuga: Ni sheria gani ya uchaguzi au ya nchi inayokulazimisha ukitangazwa mbunge wewe huna uwezo wa kukataa?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Ni kweli au si kweli uliingia Bungeni kwa uchaguzi ambao ni batili?

Heche: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Ukaserebuka.

Heche: Kuna kuserebuka Bungeni?

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 3.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo ukishindwa unaenda nyumbani?

Heche: Kwenye uchaguzi huru.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo ukishindwa inategemea na mazingira?

Heche: Nchi hii ina figisu nyingi.

Nassoro Katuga: Ulisema uligombea 2008 na 2015?

Heche: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Ule uchaguzi uliogombea 2015, wewe ukashinda, uliukubali au hukuukubali?

Heche: Niliukubali.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, huo uchaguzi ulikuwa huru na haki?

Heche: Haukuwa huru na haki.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kama wewe ni mtu wa haki na unasema uchaguzi haukuwa huru na haki, je, ulikuwa na uwezo wa kukataa (kutokubali) ushindi wako au ulilazimishwa?

Heche: Jimboni nilikuwa pia na Madiwani.

Jaji Ndunguru: Hajakuuliza Madiwani.

Nassoro Katuga: Kama wewe ni mtu wa haki, tuache pepepepe. Ulikuwa na uwezo wa kukataa kutangazwa mshindi wa uchaguzi ambao haukuwa huru na haki au ulilazimishwa?

Heche: Pepepepe ni nini kwanza ili nijue kujibu?

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba wewe ulitangazwa katika uchaguzi ambao haukuwa huru na haki, lakini hukuwa na jinsi.

Heche: Nilitangazwa kwa nguvu ya umma.

Nassoro Katuga: Ni sheria gani ya uchaguzi au ya nchi inayokulazimisha ukitangazwa mbunge wewe huna uwezo wa kukataa?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Ni kweli au si kweli uliingia Bungeni kwa uchaguzi ambao ni batili?

Heche: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Ukaserebuka.

Heche: Kuna kuserebuka Bungeni?

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Kweli target 🎯 ipo kwa Heche, fujo ni nyingi juu ya yeye na ndani anabanwa, mara bank, mara magari, mara passport yake amepewa na mkuu wa usalama....
 
Back
Top Bottom