Ulitoboa maisha ukiwa na umri gani?

Ulitoboa maisha ukiwa na umri gani?

Tatizo kubwa linalonikumba pia ni jinsi ya kuondoka nyumbani kutafta maisha...Kila nikiwaeleza wazazi wanakomalie nibaki nisubiri ajira, inafika time natamani ata niondoke bila kuaga ila wanaanza misemo yao ile " asiyesikia la mkuu, huvunjika guu" YANI TABU TUPU
[emoji23][emoji23] Eti mosemo yao ile...
Mkuu hakuna mzazi anaruhusu mtoto kujitegemea ikiwa hauoni akishughulisha na kitu cha kumuingia hela ndo maa nimekambia maisha yanaanzia hpo ulipo ulipo ili kujipnga ukitoka hpo ujue unaanzia wap na unaishia wap sasa wew utoke home uende wap hauna kazi,hauna hela,hauna kitu cha kukuingizia hela

kwa style hyo mzazi hawezi kukuruhusu maan anajua ukitoka home utaenda kwa marafiki ambao ata pengine hawana future

so mzazi anakuwa na wasiwasi usije enda kuwa mvuta bange tu

Ila ukianzia hapo ulioo ukawaonesha mfano kuwa we ni mpambanaji lazima wakupe baraka na aakusaport pia
 
Jambo la kwanza la kufanya ni kutoka nyumbani..omba support kwa wazazi nenda mkoa mwingine tofauti na walipo wazazi upange chumba chako uanze kujitegemea. Njaa na gharama za mahitaji mengine zitakupa akili na kukufanya usichague kazi. Hapo utaanza kufikiri na kufanya kazi ili uweze kujilipia kodi, chakula na mavazi baada ya support ya wazazi kuisha.

LABDA NIKUPE HISTORIA YANGU....

Baada ya kumaliza chuo sikurudi nyumbani (nilijua nitalemaa na kuzembea)....nikaenda Dar na kuanza kupambana na jiji..nakumbuka tulikuwa watu 8 tunakaa ghetto moja, kila jioni kila mtu alipaswa alete chochote mezani. Na ukichelewa kulikuwa na kuwahi kitanda, watu wanne walilala kitandani na mliochelewa mnalala sakafuni..mito ilikuwa viatu vya washkaji [emoji23][emoji23]. Na kila siku kulikuwa na zamu ya kupika...Hatujui utapika nini ila tunataka tule na tushibe.Hapo akili ikachaji haraka...nikaomba kujishikiza kwenye stationery moja pale Mabibo Hostel. Nikiwa na laptop yangu niliyotoka nayo chuo na smartphone yangu nikaanza kuwa nawaandikia wanachuo kazi zao wanazopewa (wengi huwa hawana muda kutokana na vipindi kubana), kuweka table of contents, wengine wanakuja na maswali waliyopewa (sana sana individual work) nawafanyia - Si nilikuwa fresh kichwa bado kinakumbuka. Kama sifahamu swali nagoogle. Kutype na kuedit Page nilikuwa natoza Tsh 1000. Table of content ilikuwa Tsh 5000. Bahati nzuri mwaka huo Halotel ndio wamekuja TZ, walikuwa wana promo ya unlimited internet Tsh 1000 kwa masaa 24. Nikawa naweka kifurushi kwa siku nawasha hotspot naunga kwenye computer nawauzia watu internet kwa dakika 15 (Tsh 500), nusu saa (Tsh 1000) na lisaa (Tsh 2000). Pia nikawa nadownload movies na nyimbo nawauzia wanachuo na raia wengine kama siku hiyo sikupata wateja wa internet. Nyimbo moja Tsh 200 na Movie Tsh 500. Hapo nikaweza kupanga chumba changu maeneo ya Riverside (karibu na Mabibo ili kuepuka gharama za usafiri) na kununua mahitaji muhimu (Godoro, feni, vyombo, jiko la gesi na vyakula - mchele, unga, sukari)

Kila siku nilikuwa naomba kazi zisizopungua 5 - sikujali experience,location wala level of employment. Mungu mwema nikapata kazi na sasa nipo kwenye nafasi nzuri.

Naamini nimekuhamasisha.
Shukran Mkuu, umenihamasisha...Bado nipo napambana na Stage one ambayo ni "KUTOKA NYUMBANI" kila nikijaribu nakutana na vipingamizi vya wazazi na kwa maisha ya hom hawawez kubali kunipa mtaji wanadai wadogo zangu nao inabidi wasome
.
Ila Inshaallah, i believe 2021 hautaisha bila kuwa na direction yoyot
 
Shukran Mkuu, umenihamasisha...Bado nipo napambana na Stage one ambayo ni "KUTOKA NYUMBANI" kila nikijaribu nakutana na vipingamizi vya wazazi na kwa maisha ya hom hawawez kubali kunipa mtaji wanadai wadogo zangu nao inabidi wasome
.
Ila Inshaallah, i believe 2021 hautaisha bila kuwa na direction yoyot
Tafuta mtaji mwenyewe acha unazi... kwanza we jinsia gani mpaka unasubiri upewe mtaji na familia?¡
 
Maisha wala hayana formula mdogo wangu.
Unaweza at 22 ukawa na ndoa, nyumba, watoto, mji, biashara af ukavippteza at 45 vyote, na ukavipata tena at 60's

Na unaweza usivipate vyote mpk unakufa.
Na unaweza uvipate uvikose uvipate uvikose.
Na unaweza uvikoseeeeee, uje uvipate at 50's

Wewe pambaaaaaaaanaaaaa.
Pambana ya hela yote.
Achana kutizama life timelines za watu.

Utasanda
 
Maisha wala hayana formula mdogo wangu.
Unaweza at 22 ukawa na ndoa, nyumba, watoto, mji, biashara af ukavippteza at 45 vyote, na ukavipata tena at 60's

Na unaweza usivipate vyote mpk unakufa.
Na unaweza uvipate uvikose uvipate uvikose.
Na unaweza uvikoseeeeee, uje uvipate at 50's

Wewe pambaaaaaaaanaaaaa.
Pambana ya hela yote.
Achana kutizama life timelines za watu.

Utasanda
I get your point..Shukran Mkuu
 
Pole, una shida inayohitaji kushauriwa lkn una shida pengine ya kutofanyia kazi ushauri unaopewa, sasa:-
(a). Umekuwaje muhitimu halafu uwe mtu wa kusubiri chakula mezani iwapo ni mzima wa afya? Hapo uliposimama ziko fursa nyingi - acha aibu na kufikiria utakavyofikiriwa ukionekana ktk kazi fulani fulani (wengi wa waliotoboa hawakuchagua kazi)

(b). Kila hatua ya maisha utakayofikia ina changamoto zake - hata hivyo kila changamoto ina majibu yake

Mwisho, kama kweli wewe ni graduate na unasubiri chakula mezani basi unaumwa ugonjwa wa kisaikolojia na unahitaji dawa
 
Mafanikio yangu ni kuweza kupambana na viumbe waseng....kama hawa..... Au kuna mafanikio mengine ndg zangu[emoji16][emoji16]
FB_IMG_16092300396691981.jpg
 
Usipotumia uwezo wako kutimiza zako, wapo watakao tumia uwezo wako kutimiza ndoto zao

Acha aibu ya kuchagua kazi na acha uoga wa kufikiria watu watakuchukuliaje mtaani

People will always judge you no matter what...
 
Back
Top Bottom