Ulitoboa maisha ukiwa na umri gani?

Ulitoboa maisha ukiwa na umri gani?

Haya ngoja nianze kusave mia mia

Kupata milioni siyo kazi,kazi kuitunza milioni jinsi ya kuitunza hiyo milioni kwa sababu utaanza kuhitaji mambo meengi.kwa sababu kila unavyonenepa matatizo ndiyo yaaongezeka.unaweza kushindwa vita ila usipoteze jeshi hilo ndilo muhimu kwa sababu unaweza ukajipanga na jeshi lako ukarudi tena vitani upya.
 
Kupata milioni siyo kazi,kazi kuitunza milioni jinsi ya kuitunza hiyo milioni kwa sababu utaanza kuhitaji mambo meengi.kwa sababu kila unavyonenepa matatizo ndiyo yaaongezeka.unaweza kushindwa vita ila usipoteze jeshi hilo ndilo muhimu kwa sababu unaweza ukajipanga na jeshi lako ukarudi tena vitani upya.
Kiukweli nina tatizo la savings, nimeshindwa kabisa najionea huruma
 
Usikae chini na kuwaza Sana young anzia hapo ulipo tafuta kile unachopenda kukifanya alafu Anza kukifanyia kazi Kam ni biashara hakikisha kwanza umefanya uchunguzi wa kutosha wa hiyo biashara then anzia hapo ulipo.
Banafsi nlikua kama wewe ila baada ya kuanza biashara ya mtaji wa elfu 35 wa kuuza kitimoto adi Sasa namtaji wa mil 2 na ni kwa mda mfupi na ad Sasa ninavijana watatu nmewaajiri.
Kikubwa ni ujasiri wako unahitajika hapo
 
Nipo hapa Ligend, kwahiyo kua karbu na mimi humu utajua vingi.

Note:
Usije na nyuzi za kukosoa watu humu, ni wanamapovu humu ni balaaa 🤣🤣
 
Kutoboa kimaisha haijalishi umri angalia hawa jamaa halafu uwe na amani kuwa ipo siku
IMG_0046.jpg
 
Jambo la kwanza la kufanya ni kutoka nyumbani..omba support kwa wazazi nenda mkoa mwingine tofauti na walipo wazazi upange chumba chako uanze kujitegemea. Njaa na gharama za mahitaji mengine zitakupa akili na kukufanya usichague kazi. Hapo utaanza kufikiri na kufanya kazi ili uweze kujilipia kodi, chakula na mavazi baada ya support ya wazazi kuisha.

LABDA NIKUPE HISTORIA YANGU....

Baada ya kumaliza chuo sikurudi nyumbani (nilijua nitalemaa na kuzembea)....nikaenda Dar na kuanza kupambana na jiji..nakumbuka tulikuwa watu 8 tunakaa ghetto moja, kila jioni kila mtu alipaswa alete chochote mezani. Na ukichelewa kulikuwa na kuwahi kitanda, watu wanne walilala kitandani na mliochelewa mnalala sakafuni..mito ilikuwa viatu vya washkaji [emoji23][emoji23]. Na kila siku kulikuwa na zamu ya kupika...Hatujui utapika nini ila tunataka tule na tushibe.Hapo akili ikachaji haraka...nikaomba kujishikiza kwenye stationery moja pale Mabibo Hostel. Nikiwa na laptop yangu niliyotoka nayo chuo na smartphone yangu nikaanza kuwa nawaandikia wanachuo kazi zao wanazopewa (wengi huwa hawana muda kutokana na vipindi kubana), kuweka table of contents, wengine wanakuja na maswali waliyopewa (sana sana individual work) nawafanyia - Si nilikuwa fresh kichwa bado kinakumbuka. Kama sifahamu swali nagoogle. Kutype na kuedit Page nilikuwa natoza Tsh 1000. Table of content ilikuwa Tsh 5000. Bahati nzuri mwaka huo Halotel ndio wamekuja TZ, walikuwa wana promo ya unlimited internet Tsh 1000 kwa masaa 24. Nikawa naweka kifurushi kwa siku nawasha hotspot naunga kwenye computer nawauzia watu internet kwa dakika 15 (Tsh 500), nusu saa (Tsh 1000) na lisaa (Tsh 2000). Pia nikawa nadownload movies na nyimbo nawauzia wanachuo na raia wengine kama siku hiyo sikupata wateja wa internet. Nyimbo moja Tsh 200 na Movie Tsh 500. Hapo nikaweza kupanga chumba changu maeneo ya Riverside (karibu na Mabibo ili kuepuka gharama za usafiri) na kununua mahitaji muhimu (Godoro, feni, vyombo, jiko la gesi na vyakula - mchele, unga, sukari)

Kila siku nilikuwa naomba kazi zisizopungua 5 - sikujali experience,location wala level of employment. Mungu mwema nikapata kazi na sasa nipo kwenye nafasi nzuri.

Naamini nimekuhamasisha.
 

Watu wengi walioshindwa kufanikiwa age ya 20s huwa wanaishia kukata tamaa ata kwenye mahusiano yao huwa na changamoto nyingi
Komaa upate hata boda au kiwanja kwa miaka hiyo itakusaidia kusogea mbele
Ukikata tamaa ni mbaya zaidi sababu unaweza kujikuta unaiashia kwenye ulevi au madawa
 
Ukiwa kama kijana shupavu...basi nakushauri ili mtaji wa 3M unatengenezwa na wewe hapo kupitia kitu unacho kifanya, actually hayupo mzazi wa hvo wa kuoa milion tatu kukupa kufanya biasha kubwa ikiwa hauna idia na hyo biashara yaan haujawai kuifanya ila wanacho fanya ukupa msingi ambao ukuwezesha kuanza ili kufikia uo mtaji mkuu...mtaji wa milion tatu uzalishwa na laki

so anza na mtaji mdgo kama upatikan wa m3 ni mgumu
Tatizo kubwa linalonikumba pia ni jinsi ya kuondoka nyumbani kutafta maisha...Kila nikiwaeleza wazazi wanakomalie nibaki nisubiri ajira, inafika time natamani ata niondoke bila kuaga ila wanaanza misemo yao ile " asiyesikia la mkuu, huvunjika guu" YANI TABU TUPU
 
Back
Top Bottom