Ulitoboa maisha ukiwa na umri gani?

Ulitoboa maisha ukiwa na umri gani?

Mimi nina 47 tayari nimetoboa maisha.

Ninaendesha bodaboda, nalisha familia yangu na nalipa kodi ya pango kwa wakati.

Hapo sijatoboa maisha ndugu zangu?
Hongera sana, ila kwa ushauri kumbuka kuweka akiba ndugu, maana kama unamudu hilo walau uhakika upo kwa zile siku utakazoshindwa kufanya kazi kwa sababu moja au nyingine, mfano kuugua. kuuguza, kuhudhuria shughuli za lazima za kijamii nk. Changamoto inayokabili ajira binafsi zinazotegemea nguvu ya mtu mara nyingi ni hizo, kwamba usipoingia job na hela haiingii
 
Wakati npo sec nikawa napga mahesabu kuwa nkifika 30yrs lazma nimilik gar hata la mkopo,hapo nikiwa naamin ntakuwa nimeshaajiriwa tena serikalini,nmemaliza sec nkajchanganya nkaenda kusoma coz ya ajabu ambayo serikal yetu inaajir watu wachache sana,nkakosa ajira,nikaamua kwenda kusoma tena coarse zenye soko wakati huo yupo kikwete,nmemaliza akaingia magu akaanza kutoa ajira kwa kudonoa nikawa mtu wa mawazo sana,nikawa nawaangalia watu maarufu ambao wako chini yangu kiumri lakin wana mabilion afu Mimi nkawa nasubir ugali wa shikamoo,ila kama ipo ipo tu,mzee akasitaafu akabuni bonge moja la mradi afu boss nikawa Mimi,mambo yanaenda poa sana,najihis nmetoboa,ila sometimes napata wasiwasi tra wanaweza Kuja nibana
Hujui kuandika mkuu
 
Usiwe na haraka na maisha. Kwa sasa tafuta maarifa na nidhamu pindi ukiwa unajichanganya na watu waliofanikiwa kimaisha ila usiwaombe pesa hutapata mchongo. Kitu cha kuzingatia kuwa makini usije kutegeka ukapewa mzigo wa majukumu mapema kwa kumpa msichana mimba. Zingatia ibada.
 
Unaweza kutoboa muda wowote ukipata cha kujiingizia kipato kikubwa utakacho Pata jitahidi kusave na kusolve mipango uliyojiwekea kingine jitahidi kuweka siri kwenye kipato chako kwa Kila mtu hata unayempenda ndo panakwamisha, watu watakuuliza kipato hata wazazi wakati wewe hujui kipato chao ukishawaambia wanapanga matumizi na mipango yao kupitia mapato yako bila wewe kujua wanatoa shida zao uzitatue mwisho mipango yako haitafanikiwa mpaka uzeeni. Tatua shida za watu huku mipango yako ikiwa ndo kipaimbele.
 
Ikiwa alimaanisha kutimiza yaliyomuhimu ktk maisha na si utajiri basi mi ilikuwa at 33,mambo ya kodi ya pango, kula,mavazi matibabu kwangu na wategemezi wangu pmj na gharama za elimu za watoto sio vitu vinavyonilaza macho kwa kunikosesha usingizi
 
Maana halisi ya kutusua kwangu ni financial freedom

Kwamba nisiwe nafanya kazi pesa yangu niliyowekeza inafanyie kazi mimi ni kula good times tu

Bado sijafikia hio level niko kwa ground i hope 2030 nitafika huko inshallah
 
Tatizo kubwa linalonikumba pia ni jinsi ya kuondoka nyumbani kutafta maisha...Kila nikiwaeleza wazazi wanakomalie nibaki nisubiri ajira, inafika time natamani ata niondoke bila kuaga ila wanaanza misemo yao ile " asiyesikia la mkuu, huvunjika guu" YANI TABU TUPU
Kuna ndugu huwa wanakatisha ssna tamaa .

Wazazi wako hawakutakii mema.

Unaweza shangaa 35 hio hapo inakukuta uko home hapo ndio wataanza kukuchukia wakati ni wao wana kukwamisha

Mimi siku zote nasikiliza moyo wangu unanimbia nini kama nikifeli its ok nimejaribu and i feel proud about it kwamba nilijaribu .

Siku ukitusua huko unakwenda watasahau maneno yao ya kukatisha tamaa .

Unachopaswa kujua hatma ya maisha yako na familia yako mwenyewe iko mikononi mwako

Chukua hatua usiishi katika fikra na mitizamo ya wengine
 
Back
Top Bottom