Kabla haujamuona Mtu yeyote yule kwamba ni mdhambi ni Vizuri ukamuombea kwanza. Kitendo cha kuacha Mambo yako kumuombea uliyemuona Tuseme Mwasherati na Mzinzi kitakufanya ujione upo katika Nafasi gani mbele za Mungu. Nifatilie kidogo.

Kiongozi wako unaempelekea Sadaka na kujihudhurisha huko. Yeye ni kioo yaani ni Jicho lako. Maanake pale unaenda Kujiangalia inatakiwa ujione. Usipojiona ipo shida. Sikiliza mtoto wa Mungu ukijiangalia kwenye kioo nyumbani kwako ni dhahiri haichukui dkk 1 unakuwa umeshajisahau ulivyo kwa sbb u mavumbi na mavumbini utarudi.

Jicho lako likikukosesha ling’oe bora uende na chongo mbinguni. Maana kila mtu anataka mbingu Hakuna mtu anachagua kwenye Moto. Ila matendo yanakuchagulia sikutishi si kosa lako bali ni JICHO LAKO unalolipelekea pesa na michango lakini halioni kwamba umefungwa Pingu na umetupwa kwenye Gereza baya sana.

Sikia. Unapo Muombea mtu toba basi unajiona kumbe na wewe si kitu(Katika Roho). Nakufundisha kusimama mwenyewe Hakuna mtu atakuonyesha njia isipokuwa wewe kupambana na Mungu wako akusaidie. Lazima ujikane sio kujikinai.

Wafu ni wale waliokufa kiroho lakini kikwili wapo hai. Wazinzi, waasherati na hao wa kufana nao.Wafu wanamakazi yao pia makaburini(makanisa yasiyomjua Mungu). Hutasikia uzinzi unakemewa wala uasherati maana na Yeye anakula kimasihara kondoo zake.

Lakini Wewe una Neema kubwa sbb Yohana : 5 : 28 - Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Sauti Ndio hii naipitisha maana maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu. Yesu akasema wazi kaeni ndani yangu nami ndani Yenu. Hivo yupo anatenda amekuja kukuweka huru na vifungo vyote vya uzinzi na uasherati. Unafufuliwa ulikuwa umekufa sasa u hai ukikubal kutii utakula mema ya nchi. Isaya 1:19

Unapoamua kuacha kwa Msaada wa Mungu yaani wewe kuomba Mungu akusaidie kuacha Mambo machafu basi umeisikia sauti ya Mungu amekutoa kwenye kaburi wala huwezi kukubali Kubak kaburini utawaacha wafu wazike wafu wao.

Kupiga mzigo ni raha lakini ni laana. Nipo hapa kukukumbusha kwamba wewe haujachelewa wakati ni sasa tulia na mkeo. Mwenye mchumba oa hakuna kona kona. Hii itakusaidia kupata ulinzi wa Mungu popote uendapo mabaya hayatakupata.

Hata vitabu vya dini zote vinakataa Uzinzi na uasherati ukiona unafurahia basi Mungu hayupo nawe ila upo kama watu wengine tu ambapo mvua inanyesha wote tunalima tunavuna. Tubu anza upya Mungu akusaidie mpendwa[emoji7]
 
Bagosha [emoji15][emoji15][emoji15][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Mwanakwaya aligegedwa kimasihara hahahaa
 
Sasa mtumishi wewe kwa hizi comments za humu unafikiri watafuatilia hivyo vifungu. Usije kuwa kama yule mtumishi aliyefungua kanisa uwanja wa fisi, anawaita waumini watarajiwa wenyewe wako bize na kusaka utamu na hela.
 
Sasa mtumishi wewe kwa hizi comments za humu unafikiri watafuatilia hivyo vifungu. Usije kuwa kama yule mtumishi aliyefungua kanisa uwanja wa fisi, anawaita waumini watarajiwa wenyewe wako bize na kusaka utamu na hela.

Sbb alienda kwa akili zake. Mimi wala sina shida afatilie asifatilie nimemaliza nilichowiwa kusema. Si wote ni wa Mungu ila wote wameumbwa na Mungu hata ibilisi. Hapa nakumbusha Toba yaani ukitoka kujichafua basi jioshe ipo neema. Ukinya lazima uchambe. Au mtu ajaribu kutembea bila kuchamba aone inafananaje na kiroho ni hivo hawachambi hawa nawakumbusha.
 
Ni hekima kufanya kila jambo kwa wakati na mahali sahihi. Unayapata haya mashambulizi kwa kuwa ujumbe wako hauko mahali sahihi. Ndo maana sisi watu wazima tunasoma bila kuweka mikasa yetu ya ujanani, lakini ninayoyasoma yananikumbusha niliyofanya zaidi ya miongo mitatu iliyopita. Then unajua hakuna jipya chini ya jua. Waachie hawa vijana wetu nao waongee, hayo ya biblia yana platforms zake nyingi sana hapa nchini.

Nakupa mkasa uliotokea nikiwa nasafiri na basi mmoja, aliingia muhubiri akaanza kushusha nondo zake lakini kumbe yale mahubiri yaliikwaza familia moja iliyokuwa inakwenda msibani. Kilichofuatia ni kondakta kusserender na kumshusha mtumishi. Ila kosa lake kubwa ni kutokuwa mahali sahii na kutoijua audience yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…