Kwa hiyo ngoja na sie tuwe wazinzi kweli kweli ndio tutaanza kutubu. Yeye wakati wa kumrudia Mungu umefika, sisi badobado kidogo. Mwenyewe nasoma hapo anasema "wakuu kimasihara ziendelee"...
[emoji1][emoji1] si kitu rahisi mkuu... Humu bado watu tunaendelea kuchukua kozi. Amini nakuambia, siku Neema ya Mungu ikikushukia utabadilika tu, Kwa njia yoyote ile hata kama ni ngumu. Kila mtu ana wakati wake sahihi. Lkn bila Neema lol!!. Yataingilia sikio la kulia na kutokea la kushoto. Na wengine watakuwa km zile mbegu zilizopandwa kwenye miiba, udongo wenye rutuba, mchanga, kwenye mawe [emoji13]. Ila wakati ukifika,,, unabadilika tuu.
 
Wewe kijana acha fear of the shetani. Sio Elisha na Eliya ndio maana nakuambia haupo makini wewe. Na sio kila kinacho kuja kukufunda the right path usifiri ni shetani.. Hapo ndio unakwama hata mie nakuombea hapa Mungu akufungue macho uone unapo elekea, ulipo na ulipotoka ili kazi ifanyike vyema katika kumtukuza Mungu
 
Deby mimi nilishabadilika zamani sana..[emoji3]hapa na uzee huu nafurahisha ubongo wangu tu! Kila mtu atabadilika kwa namna yake, asitumie nguvu nyingi huyu mchungaji mla kimasihara..
 

Ukiniambia una niombea nashukuru. Lakini maombi ya mwenye dhambi ni Kupayuka na makelele mbele za Mungu labda kama umetubu kwanza ktk Roho na kweli sasa mda mchache tu umekuja na masihara Mungu sio mshamba
 
Mzee mwenzangu umenikumbusha mbali "Operesheni Nidhamu", hiyo ilikuwa 1990, na ndiyo niliyoitumikia 833 KJ Oljoro
 
Ukiniambia una niombea nashukuru. Lakini maombi ya mwenye dhambi ni Kupayuka na makelele mbele za Mungu labda kama umetubu kwanza ktk Roho na kweli sasa mda mchache tu umekuja na masihara Mungu sio mshamba
Ona ulivyo na ushamba wa Mungu. Naimbie mie na wewe nani mwenye dhambi ?
 
Ona ulivyo na ushamba wa Mungu. Naimbie mie na wewe nani mwenye dhambi ?

Kaka Tamani kuishi maisha ya Toba nyakati zote. Toba inakufanya uwe mtakatifu kuhusu wewe au mimi nani mwenye dhambi Muulize roho wa Mungu. 1 Wakorintho : 2 : 11 - Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
 
Sasa kwanini ulisema uliniambia maombi ya mwenye dhambi ni makelele huku hujui state ya roho yangu ilivyo ? Toba haikufanyi kuwa mtakatifu. Niambie ni wapi Mungu anafanya toba na ilhali yeye ndie Mtakatifu wa wa takatifu ? Utakatifu ni nature yako ambayo umeithiri kutoka katika DNA za Mungu, pale tu aliposema na tumfanye mtu kwa mfano wetu na sura yetu kuanzia pale ulikuwa mtakatifu kama yeye alivyo kuwa mtakatifu, but unatakiwa ku work out ili u display huo utakatifu
 
Mwambie huyo mtoto hajielewi
 
Sio kila abwetaye Bwana bwana atauona uzima wa milele
 
Mkumbushe Mungu kitu ambacho hukipendi lakini unakifanya na unatamani kuacha lakini unashindwa. Nazungumzia UZINZI NA UASHERATI basi kama kuna kingine ninwewe sasa na Mungu lakini nasema ukweli wa Mungu kwamba ni wewe unaechelewa kumwambia Yeye ana subir umwambie atende. Ndo maana ni lazima kuomba.

Isaya 43:26 - Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. Hapa naongea na wale wanatamani kuacha Mambo haya ya UZINZI NA UASHERATI wanaopenda kuendelea waendelee tu.

Mwambie Mungu akusaidie. Kiu iwe ndani ya Nafsi yako omba msaada hata wewe unaejichua umejiunganisha na kuzimu pasipo ww kujua omba Nguvu ya Mungu ishuhurike na hayo maeneo. Mungu atakuvusha na maeneo mengine ambayo hujaomba. Suleman aliomba Hekima akapewa na utajir kwa nn sio wewe. Inawezekana kama unataman ujue si wewe bali Roho wa bwana ameanza kaz yake. Nipo hapa kukuambia Muda ni sasa usirudi Nyuma.

Neno la kusimama nalo katika toba ni Isaya 1:16,Isaya 1:18,Yoel 2:13, Ebrania 8:12 na mengine Mengi utajuzwa kadir utakavo simama. Kwa nn nimekupa Neno. Kwa sababu shetani haogopi maombi yako bali anaogopa Neno. Ukitubu unapata kibali. Simama mwanangu kwa miguu yako usigope unaweza.

Baba Naomba kibali juu yao wakupendao. Amina
 
Huyu choko anayeleta mahubiri humu kwenye uzi wetu ebu mpeni ajira. Naona hana kazi zaidi ya kutujazia uzi wetu huu
 
Shemu 😳
 

Mfano mimi sijajua lengo lako lakini najitahidi kukujibu kwamba utanielewa hata kesho.

Kwanza Mungu sio jina bali ni Sifa ya uungu. Ni kama kusema Rais manake ni cheo cha mwisho na hakuna kingine zaidi ya hicho. Rakini Rais ana jina lake Mh Samia Suluhu Hassan. Hivo nae Mungu analo jina lake hivo Mjue kwanza Mungu wako ili Umwabudu. Shida watu wengi hawajui wanachokiabudu mimi najua.

Kama kuna DNA YA MUNGU HILI JIPYA. mbona nisha sema kaka kwamba Shetani alimla hawa akapatikana mwana mwenye Kuasi. Mwanadamu wa kwanza kufanya Agano na Mungu ni Adamu. Je kabla ya Adam hakukuwa na watu? Kaini alienda kumuoa nan bas? Sihitaji hata unijibu haya

Kama ndivyo DNA YA MUNGU basi jiulize maneno haya Mathayo : 26 : 73 - Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.

Kwann basi hao wanaomuuliza Petro wasingekuwa tu upande wa Yesu. Ama hujui alifanyika mwili akaa kwetu na watu wakamkataa. Kama dna inasoma utamkataaje Baba yako aliyekuumba.

Hapa mchawi shetani. Adui wa mwanadamu ni shetani wapendwa si mwanadamu. Mimi kazi yangu kukuombea ili roho chafu ya shetani ikuache wewe hapo uwe huru twende mbinguni. Kosa langu nini Hakuna mtu nimemjeruhi ila nimejeruhi roho chafu.

Jana wakati nimelala nikapigwa risasi ya kifua [emoji16] kwa jinsi ya Roho nikaamka nikatakasa nikajua tu shetan hapendi. Risasi ni maneno mabaya, yenye kuvunja Moyo, machafu. Hata nyie mnaona wengine wananiambia Nakatwa[emoji16][emoji16], Mshamba[emoji123] na mengine ya kufanana na hayo. Baba anaona nami nasema awasamehe maana hamjui mlitendalo.
 
Sie wenyewe Mungu ni baba yetu. Ushauri wangu ulikuwa simple. Hubiri injili wisdome ni fungu maarifa na ufahamu vitakuongoza. Sipo kupingana na wewe.. Injili kikubwa ifike iwe inahubiriwa kwa hila au kwa upendo.. kikubwa Kristo ahubiriwe
 
Hivi mtumish unauhakika wa kweli km mungu na Yesu unaowahubiri wapo kweli?!!

Na hakika mkuu. Kama shetani anaonekana kupitia matendo ya mtu ama mtu mwenye mapepo. Basi Yesu yupo maana kwa Jina lake anakemea na inakuwa.

Waebrania 11:1 - Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Imalisha tu imani yako. Mwambie Yesu anapowatembelea wengine na wewe akutembelee si unataka kumuona imalisha maana ndivyo hata Tomaso alimuona. Amini ni kweli na hakika.

Ukimpata Yesu lazima upitie misukosuko ya familia yako. Maana miungu migeni inachachamaa dhidi ya Mungu uliyempata naye ni Yesu. Utaambiwa hio imani sio yetu, sbb umelidhi dini ya baba na babu yako hiyo wala haikupeleki popote. Tamani kukutana na Yesu ni Moto ulao nae ndiye Njia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…