Ulipata Hisia gani baada ya wewe na mkeo kupima Ukimwi na kukuta mpo Salama?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema!

Katika vitu nilikuwa naogopa ni kupima VVU. Ukimwi sio poa aseeh! Kwa sisi tuliouona miaka hiyo Watu wakiugua huo ugonjwa tumeathirika kisaikolojia. Hasa sisi wanaume ndio tunaogopa zaidi.

Haya. Embu eleza hisia ulizopata baada ya wewe mkeo kupima na kupata matokeo negative, yaani mpo salama. Ilikuwaje?

Kwa upande wangu, muda wote nilikuwa na hofu kubwa.
Nilikuwa nawaza itakuwaje kama mmoja wetu akipatikana na ugonjwa huo? Nini kitatokea.
Vipi nikikutwa na hayo maambukizi. Maana Mwanamke yeye hakuwa na wasiwasi, ila mimi hofu ilikuwa dhahiri.

Matokeo yalitoka vizuri. Hiyo ilimaanisha tupo salama na kila mmoja anapaswa kumlinda mwenzake.

Vipi kwako
 
Miaka hiyo tukitafuta watoto/mimba, relief yake sio kidogo japo hata hakukuwa na mcheps. Leo hii hunipimi hata kwa "greda"!

😂😂
Hata kwa mtutu.

Yaani bora upimwe ukiwa kitandani lakini sio ijipeleke kupima wakati unajiona mzima kabisa
 
Sijawahi kuogopa Mimi ninachokiogopa ni kuhamishiwa majibu yasiyokua ya kwangu, imagine nimeenda na majibu yangu kwamba nipo fresh alafu majibu yanarudi naambiwa sipo fresh lazima niwashangae mmekosea mmenibadirishia hivyo vipimo sio vyangu
 
Ila kupima asikwambie mtu hata kama umepima mara 10 siku ukienda lazma ka presha kawepo....,mara ya kwanza kupima ilikua dodoma enzi hizo maisha ya chuo niko na mapombe yangu kichwani mchana jua kalii, akili ikanituma niingie hospitali ya karibu nipime nilifanya kama utani ila walipochukua damu naambiwa nisubiri majibu dah pombe zote zilikata halafu wakipita manesi wanaongea huku wanacheka nahisi kama nachekwa mie, na kichwani yanakuja mawazo ya madem wote nliokula kavu na wengine ndom zilipasuka, nilivyopata majibu nikasema sirudii tena
 
Kwema!

Katika vitu nilikuwa naogopa ni kupima VVU. Ukimwi sio poa aseeh! Kwa sisi tuliouona miaka hiyo Watu wakiugua huo ugonjwa tumeathirika kisaikolojia. Hasa sisi wanaume ndio tunaogopa zaidi.

Haya. Embu eleza hisia ulizopata baada ya wewe mkeo kupima na kupata matokeo negative, yaani mpo salama. Ilikuwaje?

Kwa upande wangu, muda wote nilikuwa na hofu kubwa.
Nilikuwa nawaza itakuwaje kama mmoja wetu akipatikana na ugonjwa huo? Nini kitatokea.
Vipi nikikutwa na hayo maambukizi. Maana Mwanamke yeye hakuwa na wasiwasi, ila mimi hofu ilikuwa dhahiri.

Matokeo yalitoka vizuri. Hiyo ilimaanisha tupo salama na kila mmoja anapaswa kumlinda mwenzake.

Vipi kwako
kwa nini wanaume huwa tunauogopa kuliko hawa wenzetu?

Kwa kweli mpaka wa leo nauogopa mnooo
 
Unaenda Morogoro kupima mwenyewe kivyako vyako ndio unakuja Naye kupima KWA pamoja
 
katika kitu sikuwahi kuogopa kupima ni ukimwi. sielewi kwanini tu sina hofu japo ni mzee wa kunjunja sana. na huwa sisiti kupima wala sijiulizi
 
Back
Top Bottom