Ulinzi na Usalama wa Kazi zetu

Ulinzi na Usalama wa Kazi zetu

mkuu The bold pole sana.
Nina ushauri mdogo kwako, ukiupokea na kuufanyia kazi sawa,ukiuupuza sawa.

kama umeamua kufanya uandishi wa makala za kitafiti katika mitandao ya kijamii kuwa ni kazi yako ya kudumu,basi una kila sababu ya kuanza kutumia verified ID(jina lako la kiserikali)achana na hiyo ID unayotumia sasa.ibaki kama alias name.

nalisema hili kwasababu endapo utaamua kuwashitaki wanaoiba kazi zako ambazo umezi-post kwa kutumia ID ya the bold,mahakamani watataka utoe vithibisho vinavyotambulika kisheria kuwa wewe ni the bold wa jf.

nadhani wanaoiba makala zako wamengundua hiyo weakness kiasi kwamba wanajiamini hata ukiwashtaki wa najua watakubana wapi ili uachane nao.

Mimi sio mwanasheria,ila sina shaka wanasheria wanaweza kukushauri vizuri katika hili.jaribu ku-consult nao.kuna yule mwanasheria anayesimamia kazi za mwana fa na AY.yupo vizuri sana ktk hizi mambo.
umeonge jambo kubwa sana mkuu cha msingi ni kutumia jina halisi na kusajili mabandiko yote COSOTA na kuwa na mwanasheria
 
kampuni ya Newhabari ipo/ilikua chini ya @BASHE(MB),kama mkurugenzi,hivyo mkuu @TheBold ungewasiliana nae kabla hujachukua hatua za kisheria,pole kwa vikwazo ulivyopata hata hivyo waandishi weledi jitathmini kwa taaluma si kutumia jasho la wengine kama @TheBold
 
Jamiiforum ni media kama media zingine, imesajiliwa kama magazeti, TV nk. Mtu anapokopi ni lazima ataje chanzo cha hiyo habari. Kama ameitoa jf anatakiwa ataje jf.
Lakini pia kama ni ya biashara , ni lazima amuone mwandishi Wa makala hiyo wakubaliane malipo. Ni kama kunakili wimbo Wa mtu lazima makubaliano yawepo.
Kwa walichokufanyia wewe na jf pamoja na sisi mashabiki wako ni dharau iliyopiliza.
Nenda uwaone wenyewe kwanza mnaweza kuyamaliza. Wakikataa, waone wanasheria.
Hao ni wezi kama vibaka Wa Manzese tu.
Pole @Thebold
 
1.Verify account yako
2.Sajili kazi zako COSOTA
3.Ongea na hao jamaa wa magazeti uwe unawapa makala zako wawe wanakulipa
4.

Dunia ya leo kuna challenge kubwa sana kwenye hati maliki ya kazi za wasanii/waandishi ni ngumu sana kukwepa kuibiwa
 
hahah basi fanya uniletee malalamiko kimaandishi nifungue kesi, ila hiyo family yenu itakuwa inaeendeshwa kwa makesi kesi
Ndio maana nimeacha [emoji4]
Hata hivyo sio mbaya,mbona akina Tundu Lissu wanaishi? [emoji23] [emoji23]
 
Yani kuna watu ni wazembe balaa yani wameshindwa hata kubadili hata title?,kwa uandishi huu kweli kwanini mwakyembe asiwaburuze kadili atakavyo!.pole mkuu the bold.

Jf management unyesheni uwepo wenu juu ya hili.ikumbukwe siku si nyingi zilizopita jf mlikua na mgongano wa ki maslahi na the bold.kama jinsi jf mlivyo simamia maslahi yenu,basi ipo haja na maslahi ya mkuu the bold yasimamiwee.
 
Kazi ya Sanaa inayowekwa hapa au hata use jalalani, inalindwa na Sheria ya Hakimiliki. Hakuna namna unaweza ukakopi na kupesti hadithi ya mtu kwenye gazeti halafu usiwe umevunja Sheria kama hukupata ridhaa ya mwenye kazi.

Kitaaluma, ni makosa kukopi na kupesti hata kazi zako mwenyewe(self-plagiarism). Lazima uonyeshe kuwa unaitoa kutoka mahala fulani.
Good point,hai hitaji degree kuelewa kua huyo mwandishi aliyekop na ku pest ni kilazaaa.yani sijui hata amesomea huo uandishi.
 
Kwa nini Jamii forums isiweke taratibu ya kuzuia kukop na kupaste Makala zinazochapishwa humu ndani..

Then wawe wanaweka nembo ya JF Kama Millard Ayo anavyofanya
umeongea vyema mkuu ,,hii kitu nimeona kwenye swahilitimes.com
 
pole sana mkuu

ni kweli hii kitu kikifumbiwa macho itakuwa sio vizuri inaumiza sana kuona mtu unatenga mda wako na kuandaa makala alafu mtu anacopy na paste alafu na mwandishi bila aibu anajitaja jina kama ndo mwadaaji wa hizo makala ..bhasi tuseme wamekosea ila wawe wanaweka id yako wanapocopy ili wakubland ...sorry mkuu ila haki yako utaipata
 
Asante sana mkuu kadoda11,

Umepita mule mule ambapo kuna mwanasheria nilikuwa naongea naye pia aligusia vitu kama hivi...

Alinieleza kuhusu hili suala la alias ninayotumia inavyoweza kuleta mushkeli mahakamani kwa maana ya kwamba nitaenda kufungua kesi mahakamani nikiwa kama "Khabib" (jina langu halisi) lakini aliyeibiwa kazi yake ni "The Bold", kwa hiyo tutatakiwa kuthibitisha kuwa Khabib ndiye The Bold kitu ambacho wanasheria wa utetezi wanaweza kutumia huo mwanya kugeuza kesi in their favor...

Nashukuru sana kwa kugusia hili suala!! Nadhani inapaswa nilishghulikie hili haraka iwezekanavyo..
Mkuu nianze kwa kukupa pole kwa hilo, I can feel your pains bro, kwa jinsi unavyotumia jitahada nyingi hadi kuleta makala zinazovutia kwa msomaji halafu mtu mwingine anakuja kuzitumia kumuingizia pesa kirahisi bila kukushirikisha mmiliki kwa vyovyote inaumiza sana.

Nnachoweza kushauri mimi kama walivyosema baadhi hapo juu, hili suala usichukue kwanza hatua yoyote ya kisheria Fanya kuonana nao faragha waambie wewe ndio mmiliki halali wa makala hiyo inayowaingizia hela, na baada ya kuwadhibitishia waambie mgawane maslahi vinginevyo utawashitaki.

Kwa sababu stori bado haijaisha na wao bado wanahiitaji na wewe ndio chanzo chao, ni ngumu sana wao kukataa wasi wasi labda upo kwenye hela ambayo wewe unawaambie wakulipe wanaoweza wakaona ni kubwa, na mimi nakushauri watajie hela kubwa sio kidogo.
 
Duh!! Kumbe heshima zote zile alizojipatia jamaa pale Global ni za bure!!? Kwa style hii kaiba kazi za watu wangapi? Ila mkuu The Bold nenda kashitaki najua mwisho wa siku wanaweza kuibuka washindi ila walau watanzania na jamii kwa ujumla watajua kuwa wale wote ni wezi wa kazi za watu
 
The bold,
Jisajili na kulipia ada/ leseni mfano domain .co.tz www.the bold. co.tz kama sheria za Tanzania zinavyosema.

Baada ya hapo kazi zako zote unazotupia exclusive jamiiforums lazima umalizie kwa kuweka angalizo haki zote miliki ni za www.thebold.co.tz na huna ruhusa kunakili au kusambaza kazi hii bila ruhusa ya mmiliki ama sivyo hatua za kisheria zitachukuliwa kulinga na sheria za kusimamia mitandao, magazeti na mawasiliano za Tanzania.
 
Haina ugumu, makala ya The Bold imeandaliwa hapa JF au popote pale ina timestamp. Huyo mwandishi aseme ameandalia wapi na atupe timestamp. Mambo ya Time Created na Time Modified-File forensics 101.
Sooth uko nondo nakuchungulia kwa mbali unavyodondosha madini mwanamke wa shoka [emoji23][emoji23][emoji23] au dume? Manake jf hiii.

Hao jamaa ni majizi. Waandishi kama hawa hawafai na ndio maana hatuna waandishi mahiri hasa kwenye kufuatilia mambo yaliyojificha sana na yanayohitaji upembuzi na uchunguzi.

Wao wanasubiri bahasha za kampeni tu. The Bold pole sana.
 
The bold nakuonea kijicho maana soon unaenda kuwa tajiri,
any way cha kwanza fata ushauri wa ndugu yangu Hassan Mambosasa wa kujisajili cosota au pia wana taasisi yao inaitwa UWARIDI, nina imani utakuwa safe kwenye kutetea kazi yako.
pili kuna ushauri mwingine hapo umepewa nahisi na kadoda11 anza sasa kujiweka wazi sasa, ushakuwa celebrity, we must know you bro, anza kutumia hata jina lako kamili phone no, email etc. hii itapelekea watu kukujua na kukufatilia maybe kazi pia inaweza ongezeka.
la tatu nala mwisho maana umenikatisha kuendelea kula hapa nilipo, POLE SANA, HIKI NI KIPIMO TOSHA KUWA WW NI TISHIO HAPA NCHINI KATIKA SEKTA HII, kuna maandiko mangapi humu jf? kwa nini wewe kila siku?
Shukrani sana shemeji..

Na shukrani kwa kutuaapoti Sikh zote na kututia moyo... We really appreciate kutoka kwenye sakafu za mioyo yetu!

Naona hawa wanataka kunipa hela ili nikupe ile kazi ileeeee hahahah
 
pole sana mkuu

ni kweli hii kitu kikifumbiwa macho itakuwa sio vizuri inaumiza sana kuona mtu unatenga mda wako na kuandaa makala alafu mtu anacopy na paste alafu na mwandishi bila aibu anajitaja jina kama ndo mwadaaji wa hizo makala ..bhasi tuseme wamekosea ila wawe wanaweka id yako wanapocopy ili wakubland ...sorry mkuu ila haki yako utaipata
Shukrani sana mkuu lee empire kwa ushauri na kututia moyo..
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom