Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,671
Habari wakuu,
Nimejikuta imenibidi kukatisha mfululizo wa makala inayohusu kifo cha Rais JF Kennedy ili kutafakari na kutafuta msaada wa kisheria kutokana na gazeti la RAI kunakili makala hiyo na kuanza kuichapa bila makubaliano yoyote.
Huwa nasema mara kwa mara kwamba hakuna mtu mwenye hati miliki ya kuandika kuhusu tukio fulani, lakini ni kosa kisheria na kitaaluma pale ambapo mtu akifanya utafiti wake na kuandika kwa maneno yake na mtazamo wake kuhusu tukio fulani alafu akaja mtu mwingine akanakili andiko hilo kama lilivyo na kwenda kulitumia pasipo makubaliano au ruhusa.
Hiki ndicho ambacho wamekifanya Gazeti la Rai, wamenakili mfululizo wa makala hii ninayoiandika hapa Jamii Forums na kwenda kuichapa kwenye gazeti lao na tovuti yao huku mwandishi wao akijifanya kuwa yeye ndiye muandishi.
Si hawa tu, pia mtu ninaye muheshimu sana, Eric Shigongo naye kupitia mtandao wake wa vyombo vya habari vya Global Publishers wamenakili makala niliyoandika kuhusu kifo cha Pablo Escobar na kwenda kuichapa kama makala yao.
Changamoto hii pia ilitokea mwaka Jana kwa gazeti la Kisiwa kunakili makala ya "Geranimo" na kwenda kuichapa kwenye gazeti lao pasipo kuwasiliana na mimi (hawa waliomba radhi toleo lililofuata).
Japokuwa nimeanza kutafuta msaada wa kisheria dhidi ya Gazeti la Rai, lakini kinachonifanya nilete mjadala huu kwenu ni kuomba ushauri wa namna gani nzuri ya kuwadhibiti hawa wahuni ili huu mchezo ukome?
Najua kuna suala la kusajili kazi za uandishi, lakini hili suala kidogo linakuwa ni zito kwa watu ambao karibu kila wiki tunaandika makala mpya.... Je, ni njia gani nyingine nzuri zaidi ambayo kisheria inasaidia kuhahakikisha kazi ya ubunifu wa mtu inakuwa salama baada ya kuwekwa Public sehemu kama hii??
Lakini pia ningependa kusikia kutoka kwa Jamii forums, Maxence Melo, Invisible, Paw ni namna gani wanatusaidia kuhakikisha kuwa makala zetu, simulizi, hadithi, chambuzi na mada tunazoandika humu pale zinapotumiwa na watu wengine kwa maslahi yao ya kibiashara tunakuwa na uwezo wa kuwawajibisha kwa msaada wao (Jamii Forums).
Nazingatia kwamba kuna waandishi wengi humu ambao wanaweka mabandiko murua kabisa yenye kukonga nyoyo, nikiwataja wachache; lara 1, mshana jr, CHIEF MKWAWA, barafu, Pascal Mayalla, SteveMollel, ONTARIO na wengineo wengi..
Sasa kama kama hakutokuwa na namna fulani ambayo Jamii Forums mnatusaidia kulinda maandishi haya, tunaweza kujikuta watu hawa wanafanya kazi kubwa sana lakini kuna wahuni fulani huko nje wanafaidi jasho lao...
Wakuu, nimeandika maneno haya kwa uchungu kwa sababu imeniuma mno, kuona kuna watu wananufaika na kazi zetu ambazo sisi tunaweka hapa bure kushea na wanafamilia wenzetu wa Jamii Forums..
Naomba tusaidiane kushauriana kwenye hili.!! Ni namna gani tufanye kuwawajibisha hawa watu?? Tunakomeshaje huu uhuni wa waandishi wa habari makanjanja kuiba maandiko humu na kwenda kuyachapa huko nje kana kwamba ni kazi zao???
Huu ndio uhuni walioufanta gazeti la Rai kwenye mfululizo wa makala ya kifo cha Kennedy ninayoiandika hapa JF
Hapa chini ni uhuni uliofanywa na Global Publishers kutumia makala yangu ya "Plata O Plomo - kuhusu maisha ya Pablo Escobar"
Shukrani sana sana kwa wakuu wote ambao mmenipatiataarifa kuhusu vyombo vya habari wanaonakili maandiko yangu na kuyatumia... elmagnifico, AKILI TATU
Naomba tusaidiane kwenye hili wakuu!!! Tunafanya nii?? Hii inauma sana aisee..