Mzee inaonekana wewe ni mtu wa KIU KALI. Lakini kama ungekuwepo kipindi hicho kiu yako hiyo ingekatika yenyewe. Lakini pia hata pesa ya kununua hizo bia nayo ilikuwa haipo. Uzalishaji wa bia kipindi hicho ulikuwa mdogo sana. Na kwa kuwa UJAMAA ni kugawana UMASIKINI tulionao, ndio maana ukawekwa mgao wa bia angalau kila mtanzania aliyetaka kunywa bia anywe japo kidogo. Kwa wale wavutaji wa sigara, ilifika wakati sigara zikauzwa kwa pafu/fundo. Yaani wavutaji sigara wanajipanga foleni, halafu sigara inawashwa watu wanauziwa kwa pafu/fundo la moshi unaovuta. Wakati mvutaji anapiga pafu/fundo, muuzaji anakuwa amemshika koo, akizidisha pafu/fundo la moshi anamkaba koo.