Duka la Kwanza la Pombe kufunguliwa Saudi Arabia

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,025
Duka la kwanza la kuuza Pombe kufunguliwa Saudi Arabia baada ya miaka 70 ya Maisha bila Pombe

Duka hili ni maalum kwa wahamiaji wasio Waislam. Duka hili litakuwa mjini Riyadh.

Source: Jambo TV

===========

Saudi Arabia imesema itafungua duka la pombe kwa wahamiaji maalum wasio Waislamu mjini Riyadh, likiwa ni la kwanza kufunguliwa kwa zaidi ya miaka 70

Wateja wa eneo hilo watakuwa wafanyakazi wa Balozi mbalimbali ambao kwa miaka mingi wameagiza pombe kutoka nje katika vifurushi rasmi vilivyofungwa vinavyojulikana kama mifuko ya kidiplomasia

Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Shirika la Habari la Kimataifa la Uingereza (BBC) leo, Alhamisi Januari 25.2024 imeeleza kuwa Serikali ya Saudi Arabia imesema duka hilo litakabiliana na 'biashara haramu ya pombe' inayotajwa kushamiri kwa sasa Nchini humo

Marufuku ya kuuza pombe imekuwa sheria tangu 1952 baada ya mmoja wa watoto wa kiume wa Mfalme Abdulaziz ambaye alikuwa amekunywa hadi kulewa kumuua kwa kumpiga risasi Mwanadiplomasia wa Uingereza wakati huo

Kulingana na waraka ulioonekana na Mashirika ya Habari ya Kimataifa ya AFP na Reuters kwa nyakati tofauti wametoa taarifa kuwa Duka hilo jipya litakuwa katika eneo linalopendwa sana na wanadiplomasia hao Magharibi mwa katikati ya jiji

Watumiaji wataruhusiwa kunywa ‘pointi’ 240 za pombe kwa mwezi ambapo lita moja ya vinywaji vikali itakuwa na thamani ya pointi sita, lita moja ya divai pointi tatu na lita moja ya bia pointi moj

Pia hakuna mapendekezo kwamba wateja wataongezwa na kuorodhesha wageni 'wa kawaida'

Chini ya sheria ya sasa ya Saudia, adhabu za unywaji pombe zinaweza kujumuisha faini, kifungo cha jela, kuchapwa viboko hadharani na kufukuzwa nchini kwa wageni ambao hawajaidhinishwa.

Hati hiyo pia ilisema mamlaka inapanga mfumo mpya wa udhibiti ambao pia utaruhusu kiasi maalum cha pombe kuletwa na wanadiplomasia ili kukomesha ubadilishanaji usiodhibitiwa wa bidhaa kama hizo

Kwa miaka mingi wafanyakazi wa kidiplomasia wamelazimika kutumia "pochi" zao, ambazo haziwezi kuingiliwa na mamlaka katika nchi mwenyeji, kuleta kiasi kidogo cha pombe

Credit: Jambo Tv
 
Tuliwahi kuwaambia hapa watawala wa Saudia haswa mwanamfalme sio muislamu kabisa....Watu watabisha waislamu na viongozi wana uongozi wao chini ya msikitini wa Mecca.

Tangu huyo jamaa ammalize yule jamal khashongy kwa ukatili ,ni dhahiri sio muislamu.... Ushirikiano na Isral $USA sio muislamu..

Duka hilo linafunguliwa wiki moja mbele tena inawezekana tayar.

Taratibu mnakuja kuwaelewa Iran..
 
Nchi ya mtume ni Hijjaz yaani Makkah na Madina.

Huko Riyadh panaitwa Najd, siyo nchi makazi ya mtume!. Kama watu wa Najd wanataka kufanya mambo yao wafanye tu lakini uchafu huo kamwe hautotia mguu Makkah na Madina!.

Nasikia huko Najd siku hizi wamefungulia maconcert, disco mtindo mzima.
Ufalme wa Saudia unaipenda dunia,wacha waitafute na wataipata!
 
Back
Top Bottom