Mbunge Mwinjuma afungua duka la vifaa vya michezo la Dodoma Jiji FC

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ameipongeza Timu ya mpira wa Miguu ya Dodoma Jiji FC kwa kufungua duka la vifaa vya michezo na kupata mwekezaji WAZAWA NET SPORTS.

Mhe. Mwinjuma ametoa pongezi hizo leo Septemba 5, 2023 jijini hapo ambapo amewapongeza kwa kuwa na huduma ya MOBILE SHOP inayowarahisishia wateja kununua Jezi na vifaa vingine kwa urahisi.

"Tunafarijika sana kuwapata wazawa wa kuweka fedha kuboresha kiwango cha ligi yetu hata ukiangalia ubora wa jezi ni mzuri, na kwa sisi tusioweza kupiga mpira tutataka kwenda nazo kwenye concert" amesema Mhe. Mwinjuma.

Mhe. Mwinjuma amewakaribisha wadau wengine kufanya uwekezaji katika michezo ili kuunga mkono juhudi za Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Katika hafla hiyo, Mhe. Mwinjuma alipokea zawadi ya jezi kwa ajili ya baadhi ya Viongozi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

IMG-20230905-WA0218.jpg
 
Mpe hadhi yake unapoandika maana Title inasema mbunge mwinjuma....

Sema "Naibu waziri wa sanaa na michezo Mh Hamisi Mwinjuma (MB)" NA Baada ya jina lake unaweza ukaandika neno MB ukimaanisha mbunge kama nilivyoandika mimi hapo..
Jaribu kuzingatia Itifaki unapowataja viongozi Mbele ya Umma...

Back
Top Bottom