Ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Mar 30, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna watu wanatolea mfano wa kushindwa kwa sera za Mwalimu Nyerere kwa kuhusianisha na DUKA LA KAYA. Enzi hizo wengine tulikuwa tunakimbizana na magari ya "Ugawaji" kwenye kila duka wanalosimama, wakati mwingine tukiyakimbiza magari hayo umbali wa hadi kilomita tano au sita.

  Ilikuwa ni kawaida kupita kwenye maduka na kukuta msururu mreefu wa mawe yaliyopangwa kama alama ili wenye mawe hayo wakija wapate nafasi ya mbele kwenye foleni. Nakumbuka kulazimishwa kununua unga wa muhogo wenye mchanga ili tuweze kupata sukari kilo mbili na nusu kwa mujibu wa Kadi yetu ya Duka la kaya iliyokuwa inayonyesha kwamba nyumba yetu ina wanakaya 5.

  Enzi hizo mgambo waliokuwa wanalinda kwenye maduka ya Kaya (Consumer's Cooperative shop) walikuwa wanaabudiwa sana mitaani kwani wao kila ukija mgao na wao hawakosi kupewa, tofauti na watu wa kawaida ambao wao ni mpaka "zamu" yao ifike. Wauzaji wa maduka haya walikuwa hawajui kabisa kubembeleza wateja kwani wateja walikuwa hawana uchaguzi kutokana na kutakiwa kununua mahitaji yao kwenye maduka walikoandikishiwa kama Wateja.

  Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Masikini CCM
  Mnawalaumu hadi wafu, Mungu apishie mbali laana hii.
   
 3. maziwa ya mgando

  maziwa ya mgando Senior Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  So???
  Nyerere alijaribu kufanya alichofanya kwa kiasi chake, wewe unafanya nini?

  Siamini katika kucheza 'mwathirika" (don't play victim)
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ninakumbuka ila nilikuwa bado mdogo, enzi hizo kuna ndugu yetu alitokea malawi alituletea Sabuni na sukari, mzee alikuwa anashauri tuvifiche maana ile product tungeulizwa imetoka wapi in case ikionekana. Lakini binafsi ninamkubali sana Nyerere amekaa madarakani kwa miaka 23 lakini Mwinyi miaka10+, Mkapa10, na sasa Kikwete miaka5 halali na Mmoja wa usio halali. Lakini mpaka sasa ukiangalia vitu tangible vilivyofanyika enzi za Nyerere ni vingi kuliko vilivyofanyika ndani ya Tawala hizi tatu.
   
 5. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wewe unadhani mimi namlaumu Mwalimu? Mimi kati ya watu ambao ni watetezi wakubwa wa Mwalimu lakini sikuleta hii mada ili kumhukumu Mwalimu.

  Mimi nilishiriki kuiishi hali hii, nilikula unga wa YANGA, nikabugia BURGA, nikaogea MAJANI YA MPAPAI,nimekunywa chai kwa kuchemsha sukari kwa ukosefu wa majani ya chai, nimeogea sabuni ya MAGADI. Huu ni uzowefu wangu wala sina uchungu na sera za Mwalimu!!
   
 6. kiagata

  kiagata Senior Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Ndugu umenikumbusha mbali sana, Enzi za kuvaa mtumba toka Burundi unaonekana mhujumu wa uchumi,kuogea Sabuni ya Magwanji na kuvaa Batiki.
  Mwl,alijaribu kwa kiasi chake aka prove filure ktk sera za ujamaa na sasa utandawazi.
  Enzi za kusikiliza praye(santuri) na mwenye cassete memory Q tajiri?.
  Ahsante kaka,
   
 7. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Du, kweli umenikumbusha mbali. Nakumbuka kijijini kwetu kulikuwa na Mama aliyekuwa muuzaji (shopkeeper) katika lile duka letu la Ujamaa alikuwa ndo star pale kijijini. Tulikuwa tunasubilia mafuta ya taa au kiberiti. Mungu bariki ugali si chakula chetu kwa hiyo atukula sana unga wa Yanga mpaka wakati wa Vita ya Tz na Uganda.
  Nadhani Nyerere alikuwa na nia njema lakini strategy haikufanikiwa.
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  NMC shops models?
   
 9. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hazifanani kabisa wala na yale maduka ya RTC. Duka la kaya hupati kitu mpaka mjumbe wa nyumba kumi akutambue kama wewe ni makazi wake halafu unaingizwa kwenye Leja wewe na watu wanaokutegemea. Siku ya mgao inawezekana ikawa kila siku ya jumatatu ndiyo zamu yako kama haupo basi mgao wako unahifadhiwa au mgambo kwa kushirikiana na muuzaji wanauza kwa bei ya kuruka.
   
 10. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duka la kaya lilikuwa noma, nakumbuka la mwisho lilikuwa pale Sinza Matokeo.

  Nimekunywa sana uji wa chumvi kulaleki, maana mgao wetu sisi ulikuwa kama kilo 2 za sugar hivi. Sometimes unakata.

  Kuna siku mzee akarudi kazini na kiroba cha Sukari sijui alikifumania wapi wacha tufurahi.
   
 11. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kisa kikubwa sana kinachokumbukwa wakati wa Duka la Kaya ni pale Mjumbe wa Nyumba Kumi alipozabwa kibao na kufa na kijana ambaye alikuwa anaahirishiwa "zamu" yake kila siku. Kisa hicho kilitokea maeneo ya Manzese kwa mfuga Mbwa!!
   
 12. b

  bohha Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  OMBI KWA WANWARUMERU MASHARIKI:
  Ndugu zangu wana wa Arumeru mashariki kesho ni siku muhimu kwenu
  kuchagua maendeleo ama ubabaishaji, Chonde Chonde chagua kiongozi unyemdhani anayajua matatizo yenu na atayafanyia kazi si wale tuliowazoea na ahadi zao toka tupate uhuru msifanye kosa CHAGUENI MTU AMBAYE AMEZALIW ARUMERU, AMESOMA ARUMERU , AMEKULIA ARUMERU NA MTAFANYA KAZI WOTE ARUMERU BAADA YA TAREHE 1/4/2012.
   
 13. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Ndugu,

  Wakati huo nilikuwa ndogo wa kutumwa dukani, umenikumbusha enzi hizo. Namkumkuka mwandishi wake mahiri Mh. Ndimara I. Tegambwage, nawakumbuka baadhi ya wahusika kama vile Bibianna. Nakumbuka mzee mmoja aliyelala usingizi chini ya mti mpaka akakosa huduma ya sukari, akawa nyonge na kumwambia mkewe mara baada ya kurudi nyumbani aweke chumvi kidogo kwenye uji wa mjukuu wake.

  Asante sana kwa kutukumbusha, je naweza kukipata tena
   
 14. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi sizungumzii kitabu ndugu yangu. Nazungumzia hali halisi, mimi duka langu nalikumbuka mpaka leo ila bahati mbaya lilipokuwa wajanja wameuza eneo pamejengwa duka binafsi. Zilipokuja Rexona na Lifebouy watu tuliona kama tumefika mbinguni!! Dah. Mchele Kitumbo ulipapatikiwa na kina mama kama vile almasi iliyoanguka kutoka mbinguni, watu walikuwa wameshachoka kula mchele mdundiko!!
   
 15. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Mimi nilikuwepo enzi zile tukiishi Mbezi Juu, na maduka yanapatikana Kawe Ukwamani tu. Kwa kweli ilikuwa hali mbaya sana.

  Lakini katu siwezi kuilaumu Serikali ya kipindi kile, kwani ile ilitokana na hali ya Hewa na uhaba wa Chakula. SErikali ilijitahidi hata kuanzisha Maduka ya Kaya, Mobile Shops (Malori ya NMC yalikuwa yanapita mitaani na kuuza chakula kama Duka)

  Pia Serikali ilijitahidi hata kuagiza Unga wa Njano ili kuwanusuru wananchi wake. KWA KWELI SERIKALI ILIJITAHIDI.

  Wakati ule Serikali tu ilikuwa inaruhusiwa kuuza Chakula kwa wananchi, tena nakumbuka hali ilikuwa na unafuu kwani hata chakula kilikuwa na RUZUKU ya serikali hivyo kuuzwa kwa bei ya chini sana.

  Na tulikuwa hatuna Rasilimali nyingi kama tulivyo sasa huenda ingelikuwa kama sasa tunaposhuhudia rasilimali zikichimbwa basi maisha yangelikuwa mazuri zaidi na hata kuweza Serikali kuwalipa mishahara / posho wananchi wake wote. Na kula chakula bure na Waisraeli enzi hizo kule Jangwani walipokula MANA.

  RIP Mwalimu J. K. Nyerere, RIP E. M. Sokoine, RIP......


  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 16. MANI

  MANI Platinum Member

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Usisahau ili kadi ambayo mjumbe wa shina anajaza resho yako. Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa single basi baba mwenye nyumba akawa nampa share yangu.
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kigarama;

  Umenikumbusha mbali sana, Kwa mtu ambaye hakuwa na utambuzi kuanzia 1984 backwards hawezi kukuelewa. Yale mawe na madebe matupu yaliyochakaa tulikuwa tunayaita 'mabandika', tuliuziwa kwa nguvu mbaazi ambazo zilikuwa haziivi, watu badala ya kuuziwa unga kwa kilo wakawa wanauziwa mahindi kwa kilo sasa jiulize ukienda kusaga kilo tatu za mahindi utapata unga kilo ngapi?, watu wakawa wanachemsha mahindi na kula. Maeneo ya nyanda za juu kusini watu walikuwa wanavaa visalfeti kama nguo, ndiyo ukawa mwanzo kwa kuruhusiwa nguo za mitumba.

  Nyerere alikuwa ana uchungu hasa na watanzania na maendeleo yao tofauti na viongozi tunaowaona leo hii wenye 'on your own mentality'. Tatizo kubwa la mwalimu lilikuwa kwa watu waliomzunguuka(wasaidizi wake), wengi walikuwa ni watu wenye uelewa finyu na kujikuta wanategemea kila initiative toka kwa Ikulu, ndiyo ikawa chanzo cha kuwa na katiba mbovu iliyolididimiza Taifa kiuchumi na kimaendeleo mpaka leo. Mtu mmoja anakuwa mchumi, daktari, mwanajeshi, polisi, mkulima etc.

  Nakumbuka moto aliouwasha Sokoine (RIP) uliwafanya watu kutupa viroba vya sukari na mafuta porini, kuna mtu alikuwa na shehena ya mafuta ya kupikia kaifungia akaona njia pekee ya kumlinda ni kufugia kuku kwenye store ila walimtia nguvuni. Nina hakika kama tungekuwa na mtu kama Sokoine leo hii tungekuwa mbali sana na kuna baadhi ya watu wasingeingia kwenye siasa kwani ingekuwa hailipi.
   
 18. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Read my lips. Government is a crappy capitalist, and the shortage of goods was a man made disaster.
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  tumetoka mbali....jamani dah....
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,766
  Likes Received: 4,980
  Trophy Points: 280
  ..nizikumbuka enzi za maduka ya kaya.

  ..Mwalimu alikuwa anadanganywa na jamaa wengine wawili.
   
Loading...