Ulikutana na kituko gani ugenini

Ulikutana na kituko gani ugenini

Baba mdogo ana nyumba dar,ila anakaa kaka yake na familia yake kwenye hiyo nyumba,yeye yuko mkoani kikazi,akija dar anafikia kwenye nyumba yake ila analala chumba cha kawaida,siku nafika hapo naye alifika ,kutokana na uhaba wa vyumba ikabidi niminye room moja na dingi mdogo,usiku sikulala dingi mdogo amezoea kulala bila kuzima taa, anadai akizima taa mbu zinang'ata mbo,pili usiku kucha ilikuwa ni kujamba na kukoroma kwa sauti ya juu,nilijuta mno siku ile
Alf unamkata jicho
Maana usingizi hauji
 
Niliendaga sehemu kwa rafiki zangu tukaletewa maziwa mgando aisee kwanza yalikuwa kama maji wameoshea mikono watu wengi halafu vibonge vibonge vya maziwa kwa mbali na maji mengii.Ili wasinione najifanya wa kishua nikabonda kikombe cha kwanza ,sijatulia cha pili hiki hapa nikakataa ila nilichopenda kulikuwa na mguu wa ng'ombe umebanikwa pale watu wachache tafuna sana minofu na mingine tukapewa turudi nayo town
.Toka siku hiyo mimi na maziwa mbalimbali.
 
Hao sio wajuzi
 
Kukimbizwa na Mbwa 🏃‍♂️🐕
Hadi leo naenda kwa mashaka
Kuna uyo mama tulienda kuchukua mbolea kumbe mbwa hawajafungia eh ile kuingia mbwa huyu hapa miguuni af mwenyewe anatuangalia tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom