Ulikutana na kituko gani ugenini

Ulikutana na kituko gani ugenini

Nilienda ugenini nikawa nafukuza paka asisogele sahani yangu wakati wa kula lkn chakushangaza wenyeji baada ya kumaliza kula wakawawekea paka chakula kwenye sahani yao waliomalizia kula nikatamani kutapika..
 
Binadamu huwa tunatembeleana sana yaani je ni kitu gani ulikutana nacho ugenini ukabaki mdomo wazi au kucheka tu

Mimi nilikutana na maneno katika kutambulishwa kwa mtoto wake mdogo alikuwa kama ana miaka 6 hivi akalopoka tu mama huyu ndio uncle jana ulisema upendi kuongea nae kwenye simu mama akasema sio huyu kwanza toka mtoto akagoma akasema ndio yeye si ulisema anaitwa…… nikaaga mda uho uho sikurudi tena kwakee

Je wewe ni kipi ulikutana nacho au mtoto alikuumbua kwa lipi?
Umenikumbusha mbali sana ,nilikua na safari mkoa X ya ghafla ikabidi nikalale kwao jamaa yangu anaeishi huko ila hakua kwao alisafiri akaniambia nisiwe na wasiwasi niende tu eee bwana eee ile asubuhi naamka si nikasikia baba mtu kapigwa Kofi Kwa kutokumalizia bao la pili kwenye tendo
 
Tulipokelewa tukawekewa maji bafuni, nikaogea kopo la njano.....nilivorudi ndani nikawekewa mbege kwenye kopo la njano, nikajua yanafanana.

Asubuhi baada ya chai wageni tunataka kumiminiwa tena mbege kopo halionekani nikasikia "yesuuu huyu josefu kaacha kikombe bafuni" kikafatwa aaaah qmmmmm.

Sirudii tena kunywa mbege kwenye makopo nitaomba glass

min -me huko kwenu sio
 
Baba mdogo ana nyumba dar,ila anakaa kaka yake na familia yake kwenye hiyo nyumba,yeye yuko mkoani kikazi,akija dar anafikia kwenye nyumba yake ila analala chumba cha kawaida,siku nafika hapo naye alifika ,kutokana na uhaba wa vyumba ikabidi niminye room moja na dingi mdogo,usiku sikulala dingi mdogo amezoea kulala bila kuzima taa, anadai akizima taa mbu zinang'ata mbo,pili usiku kucha ilikuwa ni kujamba na kukoroma kwa sauti ya juu,nilijuta mno siku ile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom