Wakati fulani nikiwa na miaka kama 14 hivi tulihama kutoka mkoa tuliokuepo tukahamia Mwanza, sasa tulivyofika tukapanga, wapangaji tulikua sisi tu na mwenye nyumba, Kuna mambo yalinishangaza sana nilipokua pale.
1.walikua hawaoshi nyama, yaani ikitoka buchani inakatwa inawekwa maji inapikwa( wamasema ikioshwa inaisha utamu.
2.Hawachemshi maji ya kunywa wanasema wakichemsha wataumwa tumbo ( whaaat!!!)
3.Sabuni ya kuogea hiyo hiyo wanaoshea vyombo yaani mtu yupo bafuni utasikia "weee fulani oga haraka ulete sabuni tuoshe vyombo"🤮
4.Yule mama alijifungua sasa, kwa madai yake nepi za mtoto zinatakiwa zichemshwe ndo zinatakata vizuri kwa hiyo nepi zenye pupu ya mtoto zinatolewa tu pupu, zinapitishwa kwenye maji halafu zinawekwa kwenye sufuria na sabuni ya unga zinachemshwa halafu ndo zifuliwe sasa, hilo sufuria ndo baadae usiku wanapikia wali😆.
Nakumbuka tulikaaga pale mwaka mzima sikuwahi kunywa hata maji kwenye ile nyumba yaani ile hygiene yao ilikua inanipa kinyaa.Halafu wenyewe walikua wanaona sawa tu.
Halafu walikua watu tu wa maana na nyumba kali sema kuna vitu tu walikua hawajui nadhani.
NB: hawakua wasukuma