Ulijisikiaje siku ile mkeo alipokuambia ana ujauzito wako?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,420
40,405
Nakumbuka siku hiyo sikukaa nyumbani, ilibidi nitoke mimi mwenyewe nikaenda mafichoni nakujitafakari, kweli mimi nitaitwa baba? Na majukumu yangu yatakuwa wapi?

Nikakumbuka msemo wa wahenga, unaosema, 'mwanamke akikuzalia ina maana amekupenda' vinginevyo anaweza akatoa ujauzito wako au akapachikwa ujauzito na mtu mwingine, kisha akakudanganya ni ya kwako.

Kwa furaha niliyokuwa nayo, sikutaka ata awe anafanya kazi; muda mwingi nilikuwa nambusu busu tu, pamoja na kurutubisha ujauzito wake; ukichangia na ile hali ya joto joto, pamoja na uzuri wake ilikuwa ni hatari zaidi.

Na mtoto alipokuja kuzaliwa, sura ilifanana na baba yake; Sijui kwa sababu alirutubishwa sana?

Wakuu; Ulipata furaha gani, siku ile mkeo alipokuambia ana ujauzito wako?

mam.jpg
 
Nina watoto watatu mpaka sasa, ila mwezi wa 11 mwaka jana mke wangu wapili alinifahamisha mimba yake imeharibika, ile sijakaa sawa December mke wangu mkubwa naye mimba yake ikaharibika.

Nilisononeka sana hususani kwa mke wangu mkubwa ila nikacheza na kalenda maana mimba iliharibikia wiki ya tatu au nne so ilikuwa ndogo.

Mwezi wa kwanza nikahakikisha nimemtunuku ujauzito. Aliponiambia baadae kwamba hajaziona siku zake nilifurahi sana.

Haijawahi kutokea huko nyuma kwa watoto wangu waliotangulia kwamba nilifurahia mimba kama hii mimba.
 
Mimi ndio hua namwamia kwamba leo hili bao nimeufunga goli....😜
By the way hadi kufikia juzi nina watoto 8..🙈
 
Mkuu Mimi ninawatoto 3 ila hakuna mimba ambayo nimewahi kuifurahia zote zinakuja kuja tu na masikitiko

maana ya kwanza mama mtoto aliibeba akiwa kwao tukaforce ndoa ya pili ikaingia ndani ya miez nane baada ya kuzaa yaani kwangu sijawai kufurahia mimba
 
mkuu Mimi ninawatoto 3 ila hakuna mimba ambayo nimewahi kuifurahia zote zinakuja kuja tu na masikitiko maana ya kwanza mama mtoto aliibeba akiwa kwao tukaforce ndoa ya pili ikaingia ndani ya miez nane baada ya kuzaa yaani kwangu sijawai kufurahia mimba
Itakuwa kwa sababu mko pamoja muda mrefu
 
Mimi hii mimba kwa mke wangu ndio nimeifurahia. Maana bila hii mimba nisingekuwa na kwangu wala nisingekuwa na mke.

Ni mimba iliyoleta mabadiliko makubwa sana maishani mwangu.

Mtoto kazaliwa tarehe 12/02/2022. Na tumeshare Mwezi mmoja wa kuzaliwa na Mwanangu Jayden. Kanifanana balaa.
 
Nakumbuka siku hiyo sikukaa nyumbani, ilibidi nitoke mimi mwenyewe nikaenda mafichoni nakujitafakari, kweli mimi nitaitwa baba? Na majukumu yangu yatakuwa wapi?

Nikakumbuka msemo wa wahenga, unaosema, 'mwanamke akikuzalia ina maana amekupenda' vinginevyo anaweza akatoa ujauzito wako au akapachikwa ujauzito na mtu mwingine, kisha akakudanganya ni ya kwako.

Kwa furaha niliyokuwa nayo, sikutaka ata awe anafanya kazi; muda mwingi nilikuwa nambusu busu tu, pamoja na kurutubisha ujauzito wake; ukichangia na ile hali ya joto joto, pamoja na uzuri wake ilikuwa ni hatari zaidi.

Na mtoto alipokuja kuzaliwa, sura ilifanana na baba yake; Sijui kwa sababu alirutubishwa sana?

Wakuu; Ulipata furaha gani, siku ile mkeo alipokuambia ana ujauzito wako?

View attachment 2160685
Inapendeza Sana kuwa baba ni Jambo kubwasana na ni baraka
 
Mimi siku ananiambia hajielew alikua anampango wa kwenda masomon Canada alipata scholarship kwa wafadhili fulan

Sasa tulikua tupo Kurasini pale Uhamiaji tunashighulikia Passport akaanza mara nahisi vibaya mara sijui nn tukaenda kula kwenye vile vikantin vya nje kule

Ile anakula nakumbuka Ali taka wali samaki ile kula akarudisha chench yule Mama akatania ushaharibu nikamwbia bado sana mpaka amalize masomo

Sasa tukarudi nakumbuka tulivyo kamilisha taratibu tukaambiwa turud kufata baada ya wiki 2 wakat tunatoka nika drive hadi pale Balacks Hospital ya Police nikamwambia tuchek kama yaliyomo yamo

Kwenda kupima ikawa kweli tukifurahi ila kipengele alipata scholarship kuacha kwenda kusoma ikawa hawez akajaribu kunishawishi kwakuwa mimba bado ndogo aiflash nikamwabia tusifanye hivyo akakubal japo kishingo upande

Sahivi tuna lijembe letu ndio furaha ya Familia na anampenda kuliko hata mm na tumepata mdogo wake tena juzi 2023 ataenda kuendeleza kitabu Mzumbe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom