Jinsi ya kujiandaa pale mwenza wako apatapo Mimba Kwa Vijana Masikini; ili Kupunguza Ugumu siku ya kujifungua na uzazi!

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
10,364
23,057
JINSI YA KUJIANDAA PALE MWENZA WAKO ANAPOPATA MIMBA KWA VIJANA MASIKINI ILI KUPUNGUZA HALI NGUMU WAKATI WA KUJIFUNGUA NA UZAZI na MALEZI KWA MIAKA 10

Anaandika, Robert Heriel.

Andiko hili lawafaa Sana Vijana wa Aina zote hasahasa Vijana Masikini. Andiko hili halitamuumiza yeyote, hivyo mtu yeyote anaweza kulisoma.

Haya soma;

Kwenye maisha kuna mambo yanakuja Kwa upesi bila taarifa, huwezi kuja Kwa makusudi wewe ukayaita bahati au Ajali. Kupata mimba au kumpa mimba mwanamke wakati mwingine huweza kuwa suala la ghafla ikiwa hamkupanga. Na ikitokea hivi baadhi ya watu huchangangikiwa, hujuta na kujilaumu Kwa Yale waliyoyafanya, wengine hufikia uamuzi wa kutoa mimba.

Ikiwa siku moja nawe utakuwa miongoni mwa waliopatwa na Jambo Hilo Kwa ghafla,ukiwa bado haujajipanga, na Hali ya maisha yako bado ni duni haijatengemaa, basi hivi ndivyo utafanya;

Kuna maandalizi ya namna Tatu;
1. Maandalizi ya kiroho
2. Maandilizi ya kimwili
3. Maandalizi ya kiuchumi!

Maandalizi yote ni muhimu na yanategemeana. Hata kama unakipato kizuri na maisha mazuri lazima uzingatie mambo hayo wakati wa ujauzito. Mimba sio tuu kuweza kuilea kiuchumi Bali hata kimwili na kiroho.

Na hivi ndivyo utakavyofanya Kwa habari za mimba;
1. Tangu siku ya Kwanza umegundua Una/anamimba anzeni kuweka akiba kulingana na uwezo wenu. Robo ya mnachozalisha Kwa mwezi wekeni akiba. Mfano. Kwa mwezi unaingiza 400,000/= basi itakupasa kila mwezi uweke 100,000/= Kwa ajili ya ujauzito WA mtoto. Hiyo utaiita Ada ya mimba kila mwezi. Usitumie hata ufanyeje. Kama utazidisha ni Sawa lakini isipungue.
Kama hujaajiriwa na unajifanyia vikazi vyako vya kila siku labda ni kibarua au umejiajiri hakikisha kila siku Robo ya mapato yako yatenge Kwa ajili ya mimba. Labda kila siku unaingiza 5,000 basi kila siku itakupasa uweke akiba ya 1,500/= ambayo Kwa mwezi itakuwa ni Tsh 45,000/=

Akiba hiyo utaikusanya tangu mwezi wa Kwanza wa mimba mpaka siku atakayojifungulia, pesa hiyo utaitumia Kama pesa ya dharura na matumizi ya lazima wakati WA ujauzito na baada ya kujifungua.

Ni lazima ujiandae vyema kiuchumi ili siku mtoto akifika usipate shida, sio uanze kukusanya pesa zikiwa imesalia miezi miwili ya kujifungua.

Kuweka Ada ya mimba kutaendelea Kwa miezi Tisa tena baada ya mtoto kujifungua.

2. Kama mnaishi pamoja, mimba ikishafikisha siku Mia moja ishirini, Sawa na miezi mitatu anzeni kuomba pamoja na mtoto aliyetumboni mkimuombea Dua njema Kwa kutamka maneno kadiri ya mawazo yenu yanavyotaka mtoto awe.
Kama ni Muislam msomee Quran mtoto wakati wa jioni ukiwa na Mkeo, na Kama Mwanamke upo pekeako pasipo mume iwe Kwa sababu yoyote Ile, basi wewe ndiye itakibidi ufanye hivyo.
Utamsomea maneno ya nguvu na faraja mtoto akiwa tumboni, mimba ikiwa na miezi minne tuu. Halikadhalika na Wakristo watatumia Biblia.
Kwa wale wasioamini lolote katika hayo, watawanenenea maneno ya nguvu na faraja watoto(mimba) kila siku iendayo Kwa Mungu. Kila muda wa kulala ufanye hivyo.
Utasoma na kuomba Dua Kwa dakika zisizopungua thelasini.

Ikiwa mimba imekuwa kubwa Sana kiasi kwamba inamfanya mama kuwa mchovu kupita kiasi hata akashindwa kufuata Ratiba ya usiku ya kuomba, basi itambidi afanye hivyo mara atakapoamka kutoka usingizini kila siku iendayo Kwa Mungu.
Baba ikiwa yupo basi ataendelea na Kusoma na Ratiba ya Dua hata Kama mama amelala Kwa kulishika tumbo la mkewe.

3. Tangu mwezi wa Kwanza wa mimba zingatia vyakula vyote vyenye virutubisho, Kama mbogamboga, matunda, vyakula vya protein na kidogo vya Wanga.
Sio lazima ule/ale nyama, Kama kipato kidogo hata Dagaa zinafaa, kunde na maharage.

4. Usisubiri wakati WA uzazi au kujifungua ndio ununue makorokoro na zana zitumikazo Kwa mtoto ikiwa unajua kipato chako ni kidogo.
Tangu mwezi wa Kwanza upatapo pesa nunua vitu kidogo kidogo Kama vile Mabeseni, vitanda vya watoto, nguo za kitoto za kisasa ambazo ni nzuri, Mafuta mazuri ya kisasa, usisubiri wakati WA mwisho utashindwa kumudu nahitaji yote, lakini ukichukua kidogo kidogo tangu mwezi wa Kwanza utajikuta unavitu vingi vizuri kwaajili ya malezi ya mtoto.

5. Andaa majina ya mtoto tangu mwezi wa Kwanza, andaa la kike na lakiume, majina hayo yaendane na maombi unayomuombea kila siku katika Dua zako, pia yaendane na kile unachotaka mtoto awe siku akianza harakati zake za maisha hapa Duniani.
Kikawaida majina anatoa Baba, jina linakuwa na nguvu Kama akilitoa Baba. Kama Baba hayupo kutokana na mauti basi itampasa Mama achague jina zuri.
Ikiwa Baba ataonekana ni mtu mwenye Uelewa mdogo WA mambo basi Mama atapendekeza Nina Kwa kumuomba Baba jina hilo litumike.

6. Muepushe mjamzito na Mazingira hatarishi Kama kulala bila ya chandarua, Kula vyakula hovyo mtaani Kama Vigondi, firigisi, juisi ambazo huna uhakika kama maji yaliyotumika ni salama au laa, kunywa maji yasiyo takaswa Kama kuchemshwa n.k.

7. Andaa mwili wako na mjamzito kuwa kama Baba au mama mtarajiwa Kwa kuiweka Safi kadiri uwezavyo na kuufanya kuwa na mvuto.
Mfanyishe Mkeo mazoezi, hakikisha yu Safi muda wote, asinenepe Sana wala asipunguze Sana.
Hakikisha ni msafi hata siku mtoto akijifungua avutie zaidi ili msije shindwana baadaye.
Pia nawe jiweke Kama Baba msafi na Gentleman usijisahau Sana ukavaa marapu rapu au kuacha mandevu hovyohovyo, fanya mazoezi ili uwe fresh.

Hata kama kipato kidogo lakini hakikisha hakikufanyi uchukize, uwe Baba Boya.
Kama ni mlevi, punguza kunywa pombe, kunywa kistaarabu, walau Uwe na stamina usiwe unayumba yumba Kama boya.

8. Usitangaze tangaze Kwa watu unamimba, Kama utaweza jitahidi uifiche kadiri uwezavyo, watu wako wa karibu Sana Kama mama na Baba wajue, ikiwezekana na ndugu zako tuu.
Mimba ni Jambo kubwa Sana katika Dunia hii.

9. Ikiwa hauishi na mwenza mwenye mimba labda ulimpàchika tuu kiholela, basi itakupasa uhakikishe unapanga naye siku za kuonana. Ikiwa Mazingira hayaruhusu kabisa basi utakuwa unawasiliana naye kila jioni Kwa simu, ikiwa nayo haiwezekan, basi utakuwa unamuombea Kama Baba kila jioni.

10. Hakikisha siku ya kujifungua baada ya miezi mitano ya Dua, na miezi Tisa ya maandalizi ya kiuchumi kumpokea mtoto, siku hiyo uombe Dua hasa Baba wakati mama kapatwa na uchungu, kisha baada ya kujifungua mtoto atakuwa chini ya uangalizi WA karibu na watu wa karibu tuu. Baba atafanya Dua ya kumkaribisha mtoto Duniani.
Baada ya siku Mia na ishirini tangu mtoto kuzaliwa, mtoto atatolewa nje na watu wengine wataruhusiwa kumtembelea, Kwa maana ya kumbeba.

11. Maombi na Dua vitaendelea vivyo hivyo mpaka mtoto atakapoacha kunyonya, hiyo itakuwa miezi 24 Sawa na miaka miwili. Mtoto ataanza kulala pekeake. Lakini afundishwe kusali na kuomba Dua kulingana na Imani zenu.

12. Hakikisheni watakaokuja kumuona mtoto wanajua baadhi ya taratibu zenu Kwa mfano kuongea matusi au kutokana tukana hovyo iwe ni Kwa utani au kiukwelikwelii haitaruhusiwa mbele ya mtoto. Ikiwa kuna marafiki wa namna hiyo wenye midomo michafu wapige marufuku kuja nyumbani.

13. Ikiwa mlibarikiwa Luninga na Vitu Kama Resio au Sabufa basi tangu alipozaliwa mtoto itawapasa muchague vya kuonyeshwa au kusikika katika vyombo hivyo.
Muziki isiyo na maadili, yenye matusi au video za wanamuziki wanaokaa uchi kamwe zisiwe machoni na Masikioni mwa watoto wadogo.

14. Ikiwa mtoto atakosea, usimkemee wala kumfokea Kwa sababu Hana ajualo, hajafanya Kwa dhamiri Ila unaweza ukamuelekeza Kwa kumfundisha Kwa upole na upendo.
Kumkemea mtoto mchanga ni kuua akili yake ya udadisi na kumuwekea woga na ukatili polepole.
Mtoto kadiri anavyokua, hasa akifikisha miaka miwili mpaka minne hapo utaanza kumpa maonyo ikiwa ulimuelekeza zaidi ya mara tatu Kwa njia ya upole.
Wakati mwingine watoto sio Kwa ujeuri wanafanya mambo Bali Kwa kutokuelewa Kwa nini unawazuia wasifanye.

15. Ikiwa mtoto atajisikia kulia usimwambie nyamaza wala kumkemea, utambembeleza Kwa upendo na kumuimbia nyimbo kwani nyimbo ni Sanaa ya ghibu inayogusa hisia za mtoto, au utamsimulia hadithi za kitoto hata Kama ni mchanga, mtoto ataelewa.
Wakati mwingine utapaswa umuache mtoto alie bila kumbembeleza ili atanue mapafu lakini pia kumfundisha kuwa hapaswi kudeka.

17. Hakikisha mtoto asione mabaya na Uovu wako. Kamwe usijefanya Uovu machoni au masikioni mwa mtoto. Hayo huyahifadhi katika ung'amuzi bwete,

18. Ikiwa mtoto atakuuliza swali lolote ambalo linautata, usimwambie asikuulize maswali yake ya kipuuzi, wala usimuambie hujui,Bali mwambie akikua mkubwa Kama Fulani atajua.
Au akiwa mkubwa atajua. Lakini hakikisha maswali ambayo anapaswa kuwa na majibu katika umri wake uyajibu na utoe maelezo ili yamuelee vizuri. Watoto hupenda kujua ni Kwa nini, kabla hawajajua ni Kwa jinsi gani!
Mfano Mtoto anaweza kukuuliza mbona yeye na Baba ni weupe alafu wewe mama no mweusi, mjibu umri Fulani akifika atajua.

19. Mtoto akishafika umri wa kuona aibu akiwa uchi, hapo utaanza kumtambulisha baadhi ya mema na mabaya, Kama vile matusi na hapaswi kuyatamka Kwa sababu ni dhambi na watoto wazuri hawatamki matusi.
Mtoto umri huo mara moja moja utampa ruhusa indirect way ya kuangalia na kusikiliza Luninga na Radio hata Kwa mambo ya Uovu.
Ukija umuulize nini amejifunza au mfanye aangalie mkiwa naye, alafu mfanyie usajili.
Hakikisha ukiyafanya haya ushamfunza vyakutosha.

Kwa leo Taikon ataishia hapa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Chrysanthemum

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
539
1,848
Nasoma huu uzi nikiwa kwenye Basi la Abood , naelekea Turiani nikajifiche nshatibua msala huko na mwanafunzi wa Form 4 maana 30 years kipengele !! Oya wahuni mlichomokaje hizi mambo nirudi nikiri au nilale mbele kwa muda ?

Kwako mwendesha uzi ROBERT HERIEL
1a9a88c868204adf6b2450c643586b75.jpg
 
ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
10,364
23,057
Nasoma huu uzi nikiwa kwenye Basi la Abood , naelekea Turiani nikajifiche nshatibua msala huko na mwanafunzi wa Form 4 maana 30 years kipengele !! Oya wahuni mlichomokaje hizi mambo nirudi nikiri au nilale mbele kwa muda ?

Kwako mwendesha uzi ROBERT HERIEL View attachment 2196521

😀😀😀

Miaka 30 ukitoka jela kibiriti kitakuwa kinauzwa Buku
 
Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
8,029
7,090

Asante sana. Wakuu msaada jinsi ya kuipini hii sredi
 
Christian Ray

JF-Expert Member
Jan 20, 2022
1,481
2,250
Hi ni Moja Kati ya thread nzuri Sana ambazo nimewahi kuzisoma humu jf ubarikiwe Sana mkuu ROBERT HERIEL.Siku mke wangu atakaposhika mimba yangu tutazingatia taratibu zote kwenye Uzi huu.
 
14 Reactions
Reply
Top Bottom