Ulichotegemea ndicho ulichokikuta ndani ya ndoa yako?

Ulichotegemea ndicho ulichokikuta ndani ya ndoa yako?

Mmh am not sure wewe huyo uombe msamaha au ndiyo ile "sikia mamilooo potezea hiyo bana" weee ntakufinyaa😀
Hapo sio msamaha bali ni amri ya kihuni tu. Msamaha lazma uendane na lugha laini na maneno yenye ushawishi mrembo.

"Samahani sana my mupenzi, najua nilikukwaza jana but i was so pissed off...I want us to be gud ma beibe"

NB: Huu msamaha hutakaa uupate kama unatabia za ajabu. Hii hupewa watu wanaojiheshimu tu.
 
Ups and downs hazikosekani hata ukiishi na wazazi. Muhimu kujua mapungufu ya mwenzio na kuyaishi. Namshukuru Mungu na nazidi kumuomba anilindie familia yangu.
Yeah, ni kufocus on how to be supportive and positive sio kukaa na kutaka kum reduce mtu kwa madhaifu yake. Its very inhuman and psychologically destructive.
 
Ndoa ni zaidi ya Mapenzi kwakua Mapenzi kuna wakati huisha.
 
Wengine wanaishi hadi kinyumba miaka tele na kuzaa watoto juu; ila bado ndoa zinakuja kuwashinda.

Kuchunguzana hadi mnazaa na watoto, kazi kweli kweli
Hii kitu mimi nawaambiaga sana watu, na huhitaji kuipitia kwanza ndio uelewe. Ni kujifunza kwa waliotangulia tu maana ndoa na mahusiano yao ni kitabu cha kujifunzia kwa ambao hawajaoa bado.

I have a brother, happily married for 18 years now, ila kwenye uchumba alichukua kama miezi 3 akaoa, mpaka watu walikua wanamwambia mbona ghafla sana. Ila wapo wamekaa for 5 years kwa mahusiano na walipooana tu ndoa ikakaa mwaka ikavunjika.

Uchumba hausaidii chochote katika kudumu kwa ndoa.
 
Dah, pole sana mkuu...Kimsingi ndoa inataka utulivu sana wa akili esp. kwenye kipengele cha kuchagua mwenza wa maisha.

Hali ni mbaya sana esp. kwa watu ambao wanaanzia juu kimaisha. Wale ambao wanaoa wakiwa blessed na kila kitu esp. wakiwa na uchumi imara.

Ni ngumu sana kupata mwanamke mwenye tabia zake halisi. Wengi huangukia kwa wasanii ambao wanapenda pesa tu na maisha yako mazuri. Kuwajua sio jambo jepesi sababu atakuonesha upendo 100% na manjojo yote sababu ya uhakika upo ila psychologically unakuta huyu sio mke wa kuoa.

Atakupa furaha as long as kilichomvutia kwako kikiwepo ila maisha hayako hivyo sasa. Life is very dynamic...Unaweza ukawa na maisha mazuri leo baada ya miaka miwili ukawa kibarua unasaidia fundi kupandisha zege ghorofani. Una watoto majukumu yanakuelemea na mke amekubadilikia completely anakutesa na kauli za shombo na usaliti juu.
Dah!... Mungu atusaidie sana.
 
Mada kama hizi ni kuandika maneno machache yenye yenye kujaza kurasa elfu kwa maelfu.

"Dunia ni starehe, na bora ya starehe ni kumpata mke mwema".

Ndoa tamu sana na ina machungu yake kadhalika.

Niko poa sana na wake zangu.
 
Mliopo kwenye ndoa hongera zenu aiseeee

Nimepanga nyumba yenye wapangaji wengine watatu kwahiyo kwaujumla tupo wapangaji wanne ila chaajabu mimi pekeangu ndio nimeonesha kushindwana nandoa yangu... Je mimi ninani?
Utakiwa una matatizo tena kama wewe ni sisi, basi unatuangusha sana.
 
Ndoa ni security kwa mwanamke.

Mwanamke ana hofu ya maisha hadi pale ajapoolewa, akiolewa tu basi ni uhakika na anashusha pumzi.

Mwanamme anapooa ndo hofu ya maisha inaanza, yeye ndo atajua familia inaishi vipi wakati huo na hata baada ya 'yeye' kufa!

“Tujengee nyumba, kuna leo na kesho... ukifa nisihangaike na wanangu”!!
Noma Sana , Great thinker [emoji109][emoji106][emoji110]
 
Ndoa ni kama weather ya dar sometimes joto,mvua,upepo mara tetemeko. Mambo hua hayatabiriki huku your sweetheart akiwa na uwezekano mkubwa kuwa adui yako mbaya sana .
 
Maisha sio kupata tu kuna kukosa, kuna kulala na njaa kuna raha na karaha kuna amani na vurugu.

Ndoa inahitaj uvumilivu, kuvumiliana madhaifu yenu, kuyabeba madhaifu ya mwenzio kama yako, kustiriana kwa kila hali, kusikilizana, kuheshimiana, kuthaminiana kwa ufupi ndoa ni full package.

Usikatishwe tamaa na watu waliokata tamaa, kaa tulia tafuta mke anaejua thamani yako, yake na ndoa kwa ujumla.

Usisahau ukiwa mwema utapata mwema, ukiwa kiruka njia utapata wa kufanana nawe.

Cha mwisho omba sana Mungu akupe macho ya moyoni uweze kumtambua na kumpata mke mwema, hakika ndoa njema ni ile yenye amani na kuridhika na kila hali.
Maneno ya busara sana. [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Ndoa ni sacrament takatifu, ila wahusika ndio tatizo.
 
Back
Top Bottom