Ulichotegemea ndicho ulichokikuta ndani ya ndoa yako?

Ulichotegemea ndicho ulichokikuta ndani ya ndoa yako?

Ndoa ni taasisi nyeti inahitaji uvumilivu wa hali ya juu, ukitaka ndoa yako iwe na Amani mmojawapo ajifanye Mjinga.
 
Mbona hujaeleweka. Ndugu wa mume mara nyingi ndiyo chanzo cha migogoro mingi ya mirathi inapotokea ndugu yao amefariki; kosa la mke hapo ni nini?
Sio kweli, Ndugu wa mume wako na maisha Yao, kinachotokea ni mwanamke kutaka kuharibu mali za watoto na mwisho wa siku watoto wanahangaika, tunaisho ktk jamii tumeona haya yakitokea, Suluhisho ni kila mwanandoa kuorodhesha mali zake, na kuamua nani aendeshe mali zake akiwa hayupo.
 
Kiukweli maisha ya ndoa ni vaisi vesa, unategemea furaha ukiwa nje ukioa au kuolewa furaha ni uamue iwepo, ukubali kudhalilika, ukabali kejeli hasa kama pesa imeyumba, lakini yote yanawezekana. Niliwahi mfungulia mke wangu biashara ya m15 mi nikabaki natafuta vibarua vya kawaida, dharau zilianza hadi kufikia kuchit hapo tukiwa na watoto wawil, Nilivumilia kwa sababu ya watoto ila majuzi maji yamenifika pabaya nimeamua kuwa bachela.

So ushauri wangu tegemea yote, hakuna kiumbe dhaifu duniani kama mwanamke, hata umpe roho yako haridhiki, kama nilivyosema awali furaha ni uchague, upokee madhaifu yote yatakayotokea kwenye ndoa ikiwa ni kuvumilia usaliti, kuvumilia viburi, kuvumilia kejeli, kuvumilia kila aina ya uchafu maana mtu anapoingia kwenye ndoa anajua kila kitu amemaliza kwa kuwa anajua atakuwa happy, atakula kila aina ya raha, out nyingi, sex kibao, picnic za kutosha.

Wasijue ukiwa ndani majukumu yanaongezeka, unaweza uhamishwe kibarua uende Bukoba na we uliishi Dar, muda huo watoto wapo shule mama yao nae ana kibarua hapo ndo tutaomba Mungu asimamie ndoa maana uvumilivu wa mwanamke kwa tendo la ndoa ikizidi miezi mitatu bahati, so karibu ndoa ni kamari, sorry kwa uandishi usiopangilika, nawasilisha.
Pole sana Kejeli, matusi,viburi, wizi, usaliti ndio tabia za wanawake, usijali ni mapito kwenye maisha, weka nguvu, akili kwenye kufufua biashara, itakua ngumu mwanzoni ila itakulipa, ukitaka mwanamke piga achana naye, usichonge mzinga, hata uwape roho yako hawana shukurani hata siku moja.
 
Mliopo kwenye ndoa hongera zenu aiseeee

Nimepanga nyumba yenye wapangaji wengine watatu kwahiyo kwaujumla tupo wapangaji wanne ila chaajabu mimi pekeangu ndio nimeonesha kushindwana nandoa yangu... Je mimi ninani?
Wanavumilia tu, wewe umemua kutua mzigo mapema, Wekeza kwenye kutafuta maisha hutajuta kamwe kwenye maisha yako, Wanaume wanapoteza muda mwingi sana kwa hawa wanawake.
 
Uzi mzuri! Nafatilia siku utanifaa huu. Ila huku mtaani mbona kama watu wanaenjoy sana tu ndoa zao hadi natamani, ama ni machoni pa watu tu siri zao huko ndani wanazijua wao eeh??[emoji848]
[emoji116]
IMG-20201229-WA0000.jpg
 
Hapa ndio wasiwasi wangu, kuumwa au kokosa hela watakukimbia tu, wengi wanapokuona una muelekeo wa kimaisha utaskia nitakua na wewe kwenye shida na raha sasa njoo ukose hela hata miezi mitatu tu uone huo urongo unapojidhihirisha.
Sio wote beans, mbona sasa hiv ndoa nyingi Sana wanawake wanatakeover na nyumba zipo fresh tu, tatizo ni hukuumbwa kupewa we pambana tu na jiamin riziki zinapatikana. Kukwama ni sehemu ya maisha
 
Maisha sio kupata tu kuna kukosa, kuna kulala na njaa kuna raha na karaha kuna amani na vurugu.

Ndoa inahitaj uvumilivu, kuvumiliana madhaifu yenu, kuyabeba madhaifu ya mwenzio kama yako, kustiriana kwa kila hali, kusikilizana, kuheshimiana, kuthaminiana kwa ufupi ndoa ni full package.

Usikatishwe tamaa na watu waliokata tamaa, kaa tulia tafuta mke anaejua thamani yako, yake na ndoa kwa ujumla.

Usisahau ukiwa mwema utapata mwema, ukiwa kiruka njia utapata wa kufanana nawe.

Cha mwisho omba sana Mungu akupe macho ya moyoni uweze kumtambua na kumpata mke mwema, hakika ndoa njema ni ile yenye amani na kuridhika na kila hali.
Hiyo sentensi ukiwa mwema utapata mwema ndo yenyeweeee, sio unajihesabia haki bureee.
 
Mnalazimishwa? [emoji849]. Siku mtaambiwa mle mavi na mtakula, mnapelekeshwa hadi mnatia huruma, ndio maana wana wapanda kichwani mmetulia tu
We ni jinsia gani?
 
Back
Top Bottom