Ulichotegemea ndicho ulichokikuta ndani ya ndoa yako?

Ulichotegemea ndicho ulichokikuta ndani ya ndoa yako?

Hakuna kiumbe stressful kama mwanamke.. ukishampatia ndoa ndio umempa nafasi ya kuonyesha makucha yake.. zile jeuri.. viburi alizo zificha ndio utaanza kuziona. Nakwambia hakuna rangi utaacha kuiona hasa ukikosa pesa.

#MaendeleoHayanaChama
Hebu kwanza ninywe glasi ya maji
 
Mliopo kwenye ndoa hongera zenu aiseeee

Nimepanga nyumba yenye wapangaji wengine watatu kwahiyo kwaujumla tupo wapangaji wanne ila chaajabu mimi pekeangu ndio nimeonesha kushindwana nandoa yangu... Je mimi ninani?
Wewe ni Awafu mwenye nguvu
 
Uzi mzuri! Nafatilia siku utanifaa huu. Ila huku mtaani mbona kama watu wanaenjoy sana tu ndoa zao hadi natamani, ama ni machoni pa watu tu siri zao huko ndani wanazijua wao eeh??[emoji848]
Ndoa zinaficha mengi ndani wakiwa nje utawaona wenye furaha lkn mioyoni mwao wana mengi,ila usikate tamaa ukifika wakati wako wewe olewa tu
 
Uzi mzuri! Nafatilia siku utanifaa huu. Ila huku mtaani mbona kama watu wanaenjoy sana tu ndoa zao hadi natamani, ama ni machoni pa watu tu siri zao huko ndani wanazijua wao eeh??🤔
Eeh utakufaa sana kwa reference ili wakati unakula kichapo uelewe kuwa ndoa si lelemama.
 
Hii ipo tofauti na mtazamo wangu, mwanaume akitangulia kufa wanaokuja kusumbua NI ndugu WA mume,

Lkn jambo lingine ni kwamba wanawake wengi akili zao zimeshikwa eidha na ndugu WA familia , marafiki au hawara . sasa hapo ndio kuna changamoto na usiombe mwanamke ambae akili zake zimeshikwa hukoo hasa na ndugu maaana hata cku ukijamba kwa saut mbele yake atakwenda kuwaambia ndugu zake

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
Hili pia lilinitokea mkuu yaani mke wangu alikamatwa na ndugu zake basi ilikuwa ni kero kwelikweli kila kifanyikacho ndani anawaambia ndugu zake
 
Ndoa ni tamu saaanaaa, nikiwa mkubwa nitaolewa Tena

Shida tu ikiwa umeolewa/umeoa mtu ambaye mna mitazamo tofauti...

Hapo ndio Hakuna rangi hutaona

Kwenye ndoa naamini katika upendo, amani,kusameheana, kuvumiliana na masikilizano , hivi vikikosekana hata mtu awe anapesa kiasi gani ndoa lazima ishindikane.....

Ndoa ni tamu jamani tuache masihara
 
umeongea ukweli kabisa mkuu na yamenikuta hayo.
Mwanzo wa ndoa nilipewa maneno mengi sana ya kufarijiwa ooh tutaishi kwa hali yoyote ile kama ugali tembele tutakula,kama ugali dagaa tutakula.
Lakini cha ajabu baadae nikaja kuyumba kidogo japo hela ya chakula ilikuwa ni uhakika lakini ameniacha
Ataenda kusumbuka huko aliko hatokusau atarudi tu
 
Kiukweli maisha ya ndoa ni vaisi vesa, unategemea furaha ukiwa nje ukioa au kuolewa furaha ni uamue iwepo, ukubali kudhalilika, ukabali kejeli hasa kama pesa imeyumba, lakini yote yanawezekana. Niliwahi mfungulia mke wangu biashara ya m15 mi nikabaki natafuta vibarua vya kawaida, dharau zilianza hadi kufikia kuchit hapo tukiwa na watoto wawil, Nilivumilia kwa sababu ya watoto ila majuzi maji yamenifika pabaya nimeamua kuwa bachela.

So ushauri wangu tegemea yote, hakuna kiumbe dhaifu duniani kama mwanamke, hata umpe roho yako haridhiki, kama nilivyosema awali furaha ni uchague, upokee madhaifu yote yatakayotokea kwenye ndoa ikiwa ni kuvumilia usaliti, kuvumilia viburi, kuvumilia kejeli, kuvumilia kila aina ya uchafu maana mtu anapoingia kwenye ndoa anajua kila kitu amemaliza kwa kuwa anajua atakuwa happy, atakula kila aina ya raha, out nyingi, sex kibao, picnic za kutosha.

Wasijue ukiwa ndani majukumu yanaongezeka, unaweza uhamishwe kibarua uende Bukoba na we uliishi Dar, muda huo watoto wapo shule mama yao nae ana kibarua hapo ndo tutaomba Mungu asimamie ndoa maana uvumilivu wa mwanamke kwa tendo la ndoa ikizidi miezi mitatu bahati, so karibu ndoa ni kamari, sorry kwa uandishi usiopangilika, nawasilisha.
Dah, pole sana mkuu...Kimsingi ndoa inataka utulivu sana wa akili esp. kwenye kipengele cha kuchagua mwenza wa maisha.

Hali ni mbaya sana esp. kwa watu ambao wanaanzia juu kimaisha. Wale ambao wanaoa wakiwa blessed na kila kitu esp. wakiwa na uchumi imara.

Ni ngumu sana kupata mwanamke mwenye tabia zake halisi. Wengi huangukia kwa wasanii ambao wanapenda pesa tu na maisha yako mazuri. Kuwajua sio jambo jepesi sababu atakuonesha upendo 100% na manjojo yote sababu ya uhakika upo ila psychologically unakuta huyu sio mke wa kuoa.

Atakupa furaha as long as kilichomvutia kwako kikiwepo ila maisha hayako hivyo sasa. Life is very dynamic...Unaweza ukawa na maisha mazuri leo baada ya miaka miwili ukawa kibarua unasaidia fundi kupandisha zege ghorofani. Una watoto majukumu yanakuelemea na mke amekubadilikia completely anakutesa na kauli za shombo na usaliti juu.
 
Ndoa ni tamu saaanaaa, nikiwa mkubwa nitaolewa Tena

Shida tu ikiwa umeolewa/umeoa mtu ambaye mna mitazamo tofauti...

Hapo ndio Hakuna rangi hutaona

Kwenye ndoa naamini katika upendo, amani,kusameheana, kuvumiliana na masikilizano , hivi vikikosekana hata mtu awe anapesa kiasi gani ndoa lazima ishindikane.....

Ndoa ni tamu jamani tuache masihara
Naona uko Tindini, ukumbuke hata mua una sehemu tatu 😁 jokingly !!!
 
. Angalia Mwanaume akitangulia kufa migogoro inaanza kwenye familia, ila mwanamke akitangulia kufa hakuna shida, hapo unaweza kutambua, wanawake kwa asilimia kubwa ndio chanzo cha migogoro.

Mbona hujaeleweka. Ndugu wa mume mara nyingi ndiyo chanzo cha migogoro mingi ya mirathi inapotokea ndugu yao amefariki; kosa la mke hapo ni nini?
 
Hapa ndio wasiwasi wangu, kuumwa au kokosa hela watakukimbia tu, wengi wanapokuona una muelekeo wa kimaisha utaskia nitakua na wewe kwenye shida na raha sasa njoo ukose hela hata miezi mitatu tu uone huo urongo unapojidhihirisha.
Shida na raha ndio uongo wa kwanza kabisa aufanyao mwanamke mbele ya mashahidi.

There are some Genuine women ambao wanajua thamani ya utu hawezi kukuacha alone kipindi cha matatizo. Atastick na wewe ila mishenzi itaanza kejeli na dharau mwanzo mwisho ili ufe kabisa maana huna maana tena.😂😂😂
 
Ndugu yangu unafikiri kukaa kwenye uchumba muda mrefu ndiyo guarantee ya kudumu kwa ndoa kwa sababu mnakuwa mmefahamiana tabia vizuri? Watu wanabadilishwa na watu, mazingira na vile vinavyolisha akili zetu
I agree with you, mazingira na watu yana influence kubwa sana kumbadili mtu tabia ila pia inategemea na akili za mtu. Kama mtu wa kushikiwa akili basi jua hawezi kuwa reliable patner.

Hili unatakiwa ulisome mapema sana kipindi cha uchumba.
 
Sasa shemeji unatukandia afu hapo hapo unasifia tena kuwa wapo wanawake wenye utu jamaniiiii
Shida na raha ndio uongo wa kwanza kabisa aufanyao mwanamke mbele ya mashahidi.

There are some Genuine women ambao wanajua thamani ya utu hawezi kukuacha alone kipindi cha matatizo. Atastick na wewe ila mishenzi itaanza kejeli na dharau mwanzo mwisho ili ufe kabisa maana huna maana tena.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna watu wanakuwaga na akili zao vizuri tu, baadaye anavyoanza kushikiwa akili hata huelewi imekuwaje. Anakubadilikia mazima
I agree with you, mazingira na watu yana influence kubwa sana kumbadili mtu tabia ila pia inategemea na akili za mtu. Kama mtu wa kushikiwa akili basi jua hawezi kuwa reliable patner.

Hili unatakiwa ulisome mapema sana kipindi cha uchumba.
 
Maisha sio kupata tu kuna kukosa, kuna kulala na njaa kuna raha na karaha kuna amani na vurugu.

Ndoa inahitaj uvumilivu, kuvumiliana madhaifu yenu, kuyabeba madhaifu ya mwenzio kama yako, kustiriana kwa kila hali, kusikilizana, kuheshimiana, kuthaminiana kwa ufupi ndoa ni full package.

Usikatishwe tamaa na watu waliokata tamaa, kaa tulia tafuta mke anaejua thamani yako, yake na ndoa kwa ujumla.

Usisahau ukiwa mwema utapata mwema, ukiwa kiruka njia utapata wa kufanana nawe.

Cha mwisho omba sana Mungu akupe macho ya moyoni uweze kumtambua na kumpata mke mwema, hakika ndoa njema ni ile yenye amani na kuridhika na kila hali.
Hahahah hayo maisha ya kukosa kumuelewesha slay queen mwenye tako na sura ya kutokea outing ambaye yeye mda wote anataka awe kajiremba ni kipengele.

Mi naona cha msingi mwanamke wako awe halisi tu. Mwanamke ambaye hana huruma na wewe mapema tu ni kumkataa. Nikisemaga mwanamke anatakiwa ajitoe kwako pia sio akutegemee umpege kila wakati anapokea tu naonekanaga chizi humu.

Mwanamke mbinafsi hata umpe dunia siku ukiwa huna shinkumi atakuletea dharau tu!
 
Back
Top Bottom