Ulichotegemea ndicho ulichokikuta ndani ya ndoa yako?

Ulichotegemea ndicho ulichokikuta ndani ya ndoa yako?

Maisha sio kupata tu kuna kukosa, kuna kulala na njaa kuna raha na karaha kuna amani na vurugu.

Ndoa inahitaj uvumilivu, kuvumiliana madhaifu yenu, kuyabeba madhaifu ya mwenzio kama yako, kustiriana kwa kila hali, kusikilizana, kuheshimiana, kuthaminiana kwa ufupi ndoa ni full package.

Usikatishwe tamaa na watu waliokata tamaa, kaa tulia tafuta mke anaejua thamani yako, yake na ndoa kwa ujumla.

Usisahau ukiwa mwema utapata mwema, ukiwa kiruka njia utapata wa kufanana nawe.

Cha mwisho omba sana Mungu akupe macho ya moyoni uweze kumtambua na kumpata mke mwema, hakika ndoa njema ni ile yenye amani na kuridhika na kila hali.
Madame B na S ni watu wawil tofaut au mmoja?
 
Hii kitu mimi nawaambiaga sana watu, na huhitaji kuipitia kwanza ndio uelewe. Ni kujifunza kwa waliotangulia tu maana ndoa na mahusiano yao ni kitabu cha kujifunzia kwa ambao hawajaoa bado.

I have a brother, happily married for 18 years now, ila kwenye uchumba alichukua kama miezi 3 akaoa, mpaka watu walikua wanamwambia mbona ghafla sana. Ila wapo wamekaa for 5 years kwa mahusiano na walipooana tu ndoa ikakaa mwaka ikavunjika.

Uchumba hausaidii chochote katika kudumu kwa ndoa.

Wazee wetu wazamani walikuwa wanatafutiwa mke ndani ya wiki wako ndoani,wanadumu mpaka kifo kinawatenganisha.
 
"Ukioa vibaya utakufa mapema,ukiolewa vibaya utajuta maisha yako yote"😀r.Elli
 
Hakuna kiumbe stressful kama mwanamke.. ukishampatia ndoa ndio umempa nafasi ya kuonyesha makucha yake.. zile jeuri.. viburi alizo zificha ndio utaanza kuziona. Nakwambia hakuna rangi utaacha kuiona hasa ukikosa pesa.

#MaendeleoHayanaChama
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mnatuonea sana.
 
Hakuna kiumbe stressful kama mwanamke.. ukishampatia ndoa ndio umempa nafasi ya kuonyesha makucha yake.. zile jeuri.. viburi alizo zificha ndio utaanza kuziona. Nakwambia hakuna rangi utaacha kuiona hasa ukikosa pesa.

#MaendeleoHayanaChama
Namimi nakazia hapa.HAKUNA RANGI UTAACHA KUONA.
 
Back
Top Bottom