".....kuanzia bar, stationary, usafirishaji, kilimo, ufugaji nk na zote hakuna hata moja iliyofanikiwa walau hata kurudisha mtaji!..."
Hizo biashara hazilipi kivile hasa kama uliweka watu. I bet stationary ulienda kwa mkumbo baada ya kuangalizia. Inahitaji location sahihi sana, wateja wawepo sio wakupitie au wakufuate. Hiyo sio online business kwamba mtu akiona nguo nzuri ataifuata from Mbezi to Tabata.
Usafirishaji ukute ulinunua bodaboda nyingi kama kichaa wakati wewe sio mkorofi na strict, au ulinunua gari la abiria. Ulisafirisha nini hasa.
Kilimo. Hapa ukute ulilima kilimo cha uti wa mgongo ukapinda mgongo. Kilimo ni biashara, ni hesabu, ni utaalamu. Na hakitaki mtaji mdogo kama ni kibiashara, labda kama unafanya kilimo cha kubeti.
Ufugaji haurudishi hela haraka kama unavyotaka, na hauna hela kubwa kivile kama una mtaji kidogo.
Bar sijui wanaendeshaje naona wanaleta matako makubwa na wanayabadili baada ya muda kidogo.
Hapa nahisi una matatizo makuu mawili. Kuwekeza kwenye biashara common kwa Mtanzania ila hazina return nzuri kwa mtaji mdogo, zile biashara za kupatia hela ya kula. Na kukimbia biashara kabla hujaizoea.