Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
4,975
15,317
Mtu akikuona leo hii unavyokula bata, maisha mazuri, usafiri mkali na biashara kubwa mjini, anaweza kudhani umefika hapo ulipo kirahisi rahisi tuu. Mimi mwenyewe nilikuwa nadhani hivyo!

Cha ajabu ni kwamba kila ninapojaribu kutia mguu kwenye biashara nachezea za uso mbaya kabisa najikuta natoka kapa. Mpaka muda huu nimeshajaribu zaidi ya aina 5 tofauti za biashara kuanzia bar, stationary, usafirishaji, kilimo, ufugaji nk na zote hakuna hata moja iliyofanikiwa walau hata kurudisha mtaji!

Nimebaki najiuliza nyie wenzetu mliofanikiwa kutoboa kibiashara je na nyie mwanzo mlichoma mitaji kama sisi? Hebu tupeni akili na sisi tutoboe.

NB: Usije na hoja za "fanya kazi kwa bidii".
 
Chukua muda kujifunza na pia uwe na uvumilivu. Biashara yoyote mpya matarajio ya kupata faida iwe baada ya miaka 2, kwa maana ya kupata muda mzuri wa kulisoma soko na kujifunza changamoto mbalimbali na namna ya kukabiliana nazo.

Ukitaka mafanikio ya haraka hamna biashara ya namna hiyo labda wizi. Lazima uanguke ili usimame imara.

Biashara umefanya kidogo huoni muelekeo unakimbilia nyingine, hayo unayokimbia unatakiwa uyakabili na ujifunze ili kuyashinda.

Kwaheri.
 
Chukua muda kujifunza na pia uwe na uvumilivu.

Biashara yoyote mpya matarajio ya kupata faida iwe baada ya miaka 2, kwa maana ya kupata muda mzuri wa kulisoma soko na kujifunza changamoto mbalimbali na namna ya kukabiliana nazo.

Ukitaka mafanikio ya haraka hamna biashara ya namna hiyo labda wizi.

Lazima uanguke ili usimame imara.

Biashara umefanya kidogo huoni muelekeo unakimbilia nyingine, hayo unayokimbia unatakiwa uyakabili na ujifunze ili kuyashinda.

Kwaheri.
Hapo kwenye kuvumilia miaka miwili ni pagumu mkuu hasa kama biashara haiingizi hela sasa hiyo miaka miwili unakua unaiendesha vipi, utalipaje gharama nk.
 
Mtu akikuona leo hii unavyokula bata, maisha mazuri, usafiri mkali na biashara kubwa mjini, anaweza kudhani umefika hapo ulipo kirahisi rahisi tuu. Mimi mwenyewe nilikua nadhani hivyo!

Cha ajabu ni kwamba kila ninapojaribu kutia mguu kwenye biashara nachezea za uso mbaya kabisa najikuta natoka kapa..! Mpaka muda huu nimeshajaribu zaidi ya aina 5 tofauti za biashara kuanzia bar, stationary, usafirishaji, kilimo, ufugaji nk na zote hakuna hata moja iliyofanikiwa walau hata kurudisha mtaji!

Nimebaki najiuliza nyie wenzetu mliofanikiwa kutoboa kibiashara je na nyie mwanzo mlichoma mitaji kama sisi? Hebu tupeni akili na sisi tutoboe.

NB: Usije na hoja za "fanya kazi kwa bidii".

Wasikudanganye, Biashara bila kujiungamanisha na upande wowote wa Ulimwengu wa Roho, kutoboa ni ngumu sana, kila mtu ana mbinu za siri za kujiungamanisha na ulimwengu wa roho.
 
Mtu akikuona leo hii unavyokula bata, maisha mazuri, usafiri mkali na biashara kubwa mjini, anaweza kudhani umefika hapo ulipo kirahisi rahisi tuu. Mimi mwenyewe nilikua nadhani hivyo!

Cha ajabu ni kwamba kila ninapojaribu kutia mguu kwenye biashara nachezea za uso mbaya kabisa najikuta natoka kapa..! Mpaka muda huu nimeshajaribu zaidi ya aina 5 tofauti za biashara kuanzia bar, stationary, usafirishaji, kilimo, ufugaji nk na zote hakuna hata moja iliyofanikiwa walau hata kurudisha mtaji!

Nimebaki najiuliza nyie wenzetu mliofanikiwa kutoboa kibiashara je na nyie mwanzo mlichoma mitaji kama sisi? Hebu tupeni akili na sisi tutoboe.

NB: Usije na hoja za "fanya kazi kwa bidii".

Na mwisho biashara usifanye kama unavyofanya kwe the ajira, inahitaji nidhamu kubwa kuliko aliyeajiriwa. Haiwezekani unaanza biashara unataka uamke saa kumi na moja wakati unatakiwa uamke saa tisa usiku, usake chimbo, ununue bidhaa au upige mahesabu au usuke mipango mbalimbali.
 
MKuu hili nimekua nikilisikia sana japo hua siamini kama linaweza kuwa kweli... Labda utufafanulie zaidi
Ulimwengu wa roho kuna sehemu mbili, kwa Shetani au kwa Mungu.
Wote wana kanuni zao kwenye biashara unayotaka kufanya, ili watoe urahisi wa kufanikiwa. Usione pale mfano wale wa Dar Kkoo watu wanapiga business, asilimia kubwa wamejiungamanisha kwenye ulimwengu wa roho, nimewahi sikia kwa Mhindi mmoja ana mgahawa maarufu sana, huwa anatamka maneno fulani kabla ya kufanya chochote asubuhi. Na anauza balaa, Wala hakukaa sijui miaka miwili.

Watu wana mbinu mkuu, na hawatazisema labda uwe na ukaribu nao sana.
 
Sasa kama ni hivyo ina maana sisi tunaoingia kwenye biashara bila chochote uwezekano wa kutoboa ni sifuri 😐
 
Back
Top Bottom