Ulaji wa Panya mikoa ya Kusini: Safari yangu ya siku 37 ilivyonifungua mambo mengi

Kweli unamjua Mr Mwazembe..Yule jamaa namkubali hanaga mambo ya aibu,enzi hizo analima bustani mahiwa alikuwa anaweza kujitwisha tenga akaenda nyangao kupeleka pilipili oho au kabichi
 
Cc Chige
 
Yule sio panya... Tuelewane hapo kwanza. Kuanzia Wayao, Wamakua, Wamatumbi, Wamakonde na makabila mengi ambayo nimekutana nayo wanakula huyo kiumbe. Na walaji wengi ni wakulima.
Kwamba "yule sio panya", usitake ku-complicate mambo!! Kuhusu hayo makabila uliyotaja, ukitoa Wayao na Wamakua, na sana sana Wamakua, narudia, hayo makabila mengine sio kweli!! Panya wanaliwa na watu wa Masasi ambako wenyeji wa huko sio Wamatumbi wala Wamakonde! Wamatumbi wapo Kilwa, na hawali panya!! Wamakonde wapo wilaya za Mtwaar mjini, Vijijini, Newala, na Tandahimba! Wenyeji wa hizo wilaya, majority ni Waislamu.

Kwa watu mnaopita huko juu juu ndio mnashindwa kutofautisha, lakini Wamakonde wenyewe na wenyeji wa huko wanajua kutofautisha kati ya Wamakonde na Wamawiya! Hawa Wamawiya ndio huwa hawachagui nyama, na wengi wao wanatokea Msumbiji!!!
Sio kweli!!!
 
Satoh Hirosh yupo sahihi panya wanaliwa sana hata mkoa wa Lindi maeneo yenye wakristo wengi.
Basically, ulaji wa panya kule hauna uhusiano na dini bali na kabila!! Na kama hoja ni dini, kwa Lindi ni wilaya ya Nachingwea ndiko unaweza kukuta Wakristo wengi, na majority ni Wamwera na hawali panya!! kutokana na ukaribu wa Masasi na Nachingwea, ndipo unaweza kukuta baadhi ya watu huko wanakula panya lakini sio kwa sababu ni Wakristo bali ni Wamakua wa Masasi!!! Kwenye posts zangu nimetaja Waislamu kwa sababu we all know Waislamu ndio wenye ku-complicate mambo yanayohusu misosi!!
 
Wakati wewe unayajua maeneo ya huko nje ndani, tena kwa kutembelea tu mimi ni mtu wa huko!! NImekuuliza, Lindi sehemu au wilaya gani? Tuanze hapo kwanza!
Chige unataka nn mkuu..mbn comment yangu imejitosheleza kujibu swali lako

Hebu funguka pengine sijaielewa hoja yako..lkn km ni kuhusu Lindi wanaliwa sehemu gani panya Tyr nimejibu
 
Kwa wale wenyej wa Mbeya vijijin wale wakulima Hawa panya huwa tunakula Sana
 
Umenikumbusha mbali sana shule ya msingi Nanjoka Tunduru ukupiga upupu na maji asubh unaweza usile mpaka mchana unashibisha balaaa
 
Mkuu naijua hiyo Wilaya pengine kuliko unavyoijua.

Wamwera wa Marambo, upande mwingine Mitumbati, Farm 2 ...17 , Mtila kuelekea Mnero wanagonga hiyo kitoweo kama wamakua.
Pia Ruangwa na baadhi ya vijiji vilivyokuwa vya Lindi vijijini kutoka Nanganga kuelekea Ruangwa wanakula panya sana tu. Maeneo ya Namakuku, Mkowe, .... e.t.c.

Wamakonde wa kitanzania wa Chiumbati na maeneo jirani wanakula panya kama kawaida.

Ukweli wamakua wanakula sana panya, na tembo(ndovu) kuliko makabila mengine ya kusini. Wanaongoza wamakonde wa Msumbiji wale wakristo.
 
Kusini Ni kusini ata nyanda za kusini nako awako nyuma wanapiga kunguru
 
Bwana weweeee, kwani hujuwi habari bila picha kuwa hainogi tuuuuu!
 
Kwa details hizi, we lazima utakuwa Chinga sema unajifanyisha tu kwamba eti ulitembelea huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…