Ukwepaji Kodi: Barua ya TRA kwa Bakhressa

Ukwepaji Kodi: Barua ya TRA kwa Bakhressa

Acha Mihemko; soma Taarifa usipende unalotaka kulisikia ndo ulisome Mkuu
 
Mheshimiwa Karume aliposema kuwa 'kuna watu wengine wana akili kama ya samaki" au Judge Werema aliposema "wengine vichwa vyapo badala ya kuvitumia kufikiria, wanavitumia kufuga nywele"; sasa nimeaanza kuelewa; watu hao ni wa aina ya huyu Ghost Ryder.
 
Duh! Nimesoma mara mbili nikidhani kuna substance, lakini nimetoka hola.
 
huu ujuaji nusunusu ndio umelifikisha taifa hapa. kila mtu mpelelezi,tra, doctor, mchumi, msanii,

kama taarifa hauna. unatulia kwanza sio umbea, hizi zama hazina nafasi kipindi huki.
jiandae ukiwa tayari njoo na thread yenye content na manufaa kwa taifa
 
Kontena Saga: Meneja wa ICD Afunguka Mazito

GR na mtandao wake wote tutakuwepo hapa kwa Ukaribu wa majuma mawaili matatu hivi tukimulika sakata hili kwa umakini mkubwa na kusaka zilizofichika hadi mwisho wake kama ilivyo ada:


Kulikoni?

Siku chache baada ya kutiwa chini ya Mikono ya Sheria Meneja wa bandari ya Nchi kavu Azam ICD, Madudu mengi yazidi kubainika na kutoa mwanya kwa zoezi la upelelezi wa shauri hilo kuwa rahisi na Serikali kuvuna mabilioni ya fedha zilizokwepwa na Wafanyabiashara hao.

Akizungumza na GR kwa tahadhari kubwa kutokana na unyeti wa Sakata hili na sababu za Kisheria hasa kwa kuwa suala hili lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi bila kuathiri uchunguzi wake, chanzo cha uhakika cha habari hizi kimebainisha kuwa sasa ni dhahiri kuwa wafanyabishara wengi wakwepa kodi walitumia mwanya wa mtumishi huyo kufanya biashara kinyume na kanuni za Mamlaka ya Mapato.


Nani Anatajwa kuhusika na Sakata Hili?

Mtumishi huyo anatajwa (Majina yamehifadhiwa kwa sababu za Kisheria) kama kinara wa sakata hilo huku akivuna Ukwasi uliopitiliza katika kipindi cha muda mfupi wa utumishi wake ikilinganishwa na malipo halali anayopata kutoka kwa Mwajiri wake.

Hata hivyo katika mahojiano hayo maalum; mtumishi huyo ameweka wazi kuwa mfumo wa kielektroniki wa Kampuni hiyo unazo rekodi zote ambazo ni vigumu kuchezewa (hacking) au kufutwa na hivyo kutoa mwanya wa kubainika wakwepa kodi wote waliotumia njia hiyo kuhujumu mapato ya Taifa.

Pamoja na kutowataja wafanyabishara wanaoonekana katika mfumo huo chanzo hicho kimeweka wazi kuwa tayari moto ulishaanza kuwaka kwa ndani kwa zaidi 6 iliyopita ambapo Uongozi wa Azam ICD uliwataka watendaji wa TRA kufanyia kazi takwimu za makontena hayo na kujua njia zilizotumika kuyaidhinisha kutoka na kukabidhiwa wahusika,; hata hivyo TRA walikwepa suala hili kwa kile kinachoonekana sasa kuwa timu moja na watekelezaji wa mbinu hizi hatari.


Azam wanakwepa Kodi?

Michezo hii inasadikia kufanyika katika bandari nyingi za Nchi kavu huku maafisa wa TRA ambao karibu wote wamekumbwa na Rungu la JPM na Waziri Mkuu wake ni ushahidi tosha wa kupata ukweli katika udanganyifu huu licha ya baadhi ya wanasiasa kubeza hatua hizi.

Amesikika mmoja wa watu waliokuwepo katika eneo hilo ambalo GR amepenya kusaka hizi taarifa akiteta na mmoja wa maaofisa; namnukuu, ??Bro hii ishu si tata kaka spin doctors wanavyoisambaza , ukweli mbona upo wazi sana mifumo ya kielekronik ina data zote nakwambia watu wataumbuka acha haya maneno ya kuchafuana kibishara, ukweli upo??, kilimaliza chanzo hicho.

Kujaribu kudodosa zaidi, jamaa huyu hakuwa mwenye ushirikiano chanya licha ya kuonekana kama ana nasaba na mmoja wa watendaji katika Bandari hiyo ya Nchi kavu.

Makontena 349 yanadaiwa kupotea baada ya kuingizwa Nchini na baadhi ya wafanyabiashara mbalimbali ambao si Bakhresa katika eneo la kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni ya Azam ICD (Mali ya Bakhresa Group of Companies).


Huko Uraiani Shwari?

Katika Hali ya Taharuki baadhi ya watumishi wa Bandari hiyo ya Nchi kavu na TRA wameanza kuhamisha mali zao na wengine kuficha mamilioni ya fedha ambazo wamekuwa nazo katika majumba yao wakiohofia kujulikana kwa urahisi endapo wangehifadhi fedha hizo Bank.


Hali Halisi Ikoje kwa Mintarafu hii?

Mamlaka ya mapato nchini TRA inaendesha uchunguzi kwa sasa unaofanyika, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Azam ICD ili Kuhakikisha wale wote waliohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyo husika katika upotevu huo.



Wakatabah
Kalale ukiamka uje na kitu kinachoeleweka, hapa ni ushigongo shigongo tu
 
Miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na mchezaji mmoja katika klabu ya Simba anaitwa John Masamaki,hivi siku hizi yuko wapi yule galacha?

Simba walimnunuabJOHN THOMAS MASAMAKI kutoka MTIBWA FC, huyu Jamaa alishaacha soka! Ila huyu wa TRA, ngoja tusubiri
 
Hizo zote ni blah blah mkuu! The dude should abide by the rules, so u are trying to comvice me that BAKHRESSA doesnt know what is required for him to clear his GOODS?
rudia kusoma utaelewa. sentensi ya mwisho!
 
Simba walimnunuabJOHN THOMAS MASAMAKI kutoka MTIBWA FC, huyu Jamaa alishaacha soka! Ila huyu wa TRA, ngoja tusubiri

Sawa Mkuu kuna Idfonce Amlima yeye alisajili Yanga,majimaji na Bandari Mtwara kote alivuta hela..hakufungiwa aliambiwa arudishe hela alizochukua katika izo timu..FAT chini ya Mwanakatwe..
 
1448816217275.jpg1448816203568.jpg
 
Sawa Mkuu kuna Idfonce Amlima yeye alisajili Yanga,majimaji na Bandari Mtwara kote alivuta hela..hakufungiwa aliambiwa arudishe hela alizochukua katika izo timu..FAT chini ya Mwanakatwe..

Mkuu uko vizuri ktk HDD yako, Ally Hassan Mwanakatwe!
 
Mheshimiwa Karume aliposema kuwa 'kuna watu wengine wana akili kama ya samaki" au Judge Werema aliposema "wengine vichwa vyapo badala ya kuvitumia kufikiria, wanavitumia kufuga nywele"; sasa nimeaanza kuelewa; watu hao ni wa aina ya huyu Ghost Ryder.

Vp aliyesema wapo wanaofikiri kutumia matako errr 'makalio'??????!!"""""
 
Halafu AZAM kila bidhaa yake anaandika HALAL. Kumbe wizi mtupu

Mzee mwenzangu asante kuliibua hili. Neno HALAL kwenye bidhaa za AZAM lina maana kubwa sana na ovu mno. Yaani ni ushetani mtupu ili biashara inoge. hovyoo kabisa jamaa huyu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom