Kontena Saga: Meneja wa ICD Afunguka Mazito
GR na mtandao wake wote tutakuwepo hapa kwa Ukaribu wa majuma mawaili matatu hivi tukimulika sakata hili kwa umakini mkubwa na kusaka zilizofichika hadi mwisho wake kama ilivyo ada:
Kulikoni?
Siku chache baada ya kutiwa chini ya Mikono ya Sheria Meneja wa bandari ya Nchi kavu Azam ICD, Madudu mengi yazidi kubainika na kutoa mwanya kwa zoezi la upelelezi wa shauri hilo kuwa rahisi na Serikali kuvuna mabilioni ya fedha zilizokwepwa na Wafanyabiashara hao.
Akizungumza na GR kwa tahadhari kubwa kutokana na unyeti wa Sakata hili na sababu za Kisheria hasa kwa kuwa suala hili lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi bila kuathiri uchunguzi wake, chanzo cha uhakika cha habari hizi kimebainisha kuwa sasa ni dhahiri kuwa wafanyabishara wengi wakwepa kodi walitumia mwanya wa mtumishi huyo kufanya biashara kinyume na kanuni za Mamlaka ya Mapato.
Nani Anatajwa kuhusika na Sakata Hili?
Mtumishi huyo anatajwa (Majina yamehifadhiwa kwa sababu za Kisheria) kama kinara wa sakata hilo huku akivuna Ukwasi uliopitiliza katika kipindi cha muda mfupi wa utumishi wake ikilinganishwa na malipo halali anayopata kutoka kwa Mwajiri wake.
Hata hivyo katika mahojiano hayo maalum; mtumishi huyo ameweka wazi kuwa mfumo wa kielektroniki wa Kampuni hiyo unazo rekodi zote ambazo ni vigumu kuchezewa (hacking) au kufutwa na hivyo kutoa mwanya wa kubainika wakwepa kodi wote waliotumia njia hiyo kuhujumu mapato ya Taifa.
Pamoja na kutowataja wafanyabishara wanaoonekana katika mfumo huo chanzo hicho kimeweka wazi kuwa tayari moto ulishaanza kuwaka kwa ndani kwa zaidi 6 iliyopita ambapo Uongozi wa Azam ICD uliwataka watendaji wa TRA kufanyia kazi takwimu za makontena hayo na kujua njia zilizotumika kuyaidhinisha kutoka na kukabidhiwa wahusika,; hata hivyo TRA walikwepa suala hili kwa kile kinachoonekana sasa kuwa timu moja na watekelezaji wa mbinu hizi hatari.
Azam wanakwepa Kodi?
Michezo hii inasadikia kufanyika katika bandari nyingi za Nchi kavu huku maafisa wa TRA ambao karibu wote wamekumbwa na Rungu la JPM na Waziri Mkuu wake ni ushahidi tosha wa kupata ukweli katika udanganyifu huu licha ya baadhi ya wanasiasa kubeza hatua hizi.
Amesikika mmoja wa watu waliokuwepo katika eneo hilo ambalo GR amepenya kusaka hizi taarifa akiteta na mmoja wa maaofisa; namnukuu, ??Bro hii ishu si tata kaka spin doctors wanavyoisambaza , ukweli mbona upo wazi sana mifumo ya kielekronik ina data zote nakwambia watu wataumbuka acha haya maneno ya kuchafuana kibishara, ukweli upo??, kilimaliza chanzo hicho.
Kujaribu kudodosa zaidi, jamaa huyu hakuwa mwenye ushirikiano chanya licha ya kuonekana kama ana nasaba na mmoja wa watendaji katika Bandari hiyo ya Nchi kavu.
Makontena 349 yanadaiwa kupotea baada ya kuingizwa Nchini na baadhi ya wafanyabiashara mbalimbali ambao si Bakhresa katika eneo la kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni ya Azam ICD (Mali ya Bakhresa Group of Companies).
Huko Uraiani Shwari?
Katika Hali ya Taharuki baadhi ya watumishi wa Bandari hiyo ya Nchi kavu na TRA wameanza kuhamisha mali zao na wengine kuficha mamilioni ya fedha ambazo wamekuwa nazo katika majumba yao wakiohofia kujulikana kwa urahisi endapo wangehifadhi fedha hizo Bank.
Hali Halisi Ikoje kwa Mintarafu hii?
Mamlaka ya mapato nchini TRA inaendesha uchunguzi kwa sasa unaofanyika, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Azam ICD ili Kuhakikisha wale wote waliohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyo husika katika upotevu huo.
Wakatabah