Ukweli upoje kuhusu stori kwamba JWTZ ilibaki Uganda kuanzia 1978 hadi 1983 na katika kipindi hicho Uganda lilikuwa koloni letu kwa muda?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,081
Ni story ambayo naisikia kwa muda mrefu sana tangu nikiwa shule ya msingi.

Ningependa kujua ukweli wake wa uhalisia uliokuwepo.

Kiutawala Uganda ilikuwa chini ya Tanzania hata baada ya Uganda kupata marais katika hicho kipindi?

JWTZ waliondoka kwa hiari ama ni Jeshi la NRA la Museveni liliwalazimu kwa njia moja au nyingine.
 
Kiutawala Uganda ilikuwa chini ya Tanzania hata baada ya Uganda kupata maraisi katika hicho kipindi ?
Hayo mambo ya kiufawala sijajua.ila hilo la kukaa huko ni kweli. Kuna mzee mstaafu mwanajeshi alikuwa huko alinihadithia japo sijamuuliza vizuri.
 
Ni story ambayo naisikia kwa muda mrefu sana tangu nikiwa shule ya msingi.

Ningependa kujua ukweli wake wa uhalisia uliokuwepo.

Kiutawala Uganda ilikuwa chini ya Tanzania hata baada ya Uganda kupata marais katika hicho kipindi?

JWTZ waliondoka kwa hiari ama ni Jeshi la NRA la Museveni liliwalazimu kwa njia moja au nyingine.
Watafute Wazee wa Wizara ya Maelezo.
Wanamajibu, au usubiri waje humu.
 
..pia Lt.Col.Benjamin Msuya alikuwa "Rais" wa Uganda toka Iddi Amin alipokimbia mpaka Prof.Lule alipoapishwa.
nilikaribia kusema watafute wazee wa kutoka mkoani moshi.

ila ukweli ni kwamba Uganda haikuwa koloni la Watanzania.

Sijui hizi lugha za "kikoloni" kwa kweli zimetoka wapi.

sio rafiki

Waganda walitueshimu sana na bado wanaendekea kutuheshimu, tusiwabeze.
 
..pia Lt.Col.Benjamin Msuya alikuwa "Rais" wa Uganda toka Iddi Amin alipokimbia mpaka Prof.Lule alipoapishwa.
Ni kweli kabisa Lt Col Ben Msuya ( amefariki mwaka jana ) alikuwa ndio rais ( mayor) wa nchi yote ....Akikaa ukulu Kampala. Na Entebe....alikuwa wasaidizi wake wapo mpaka leo......wanasimulia haya.....wengi wameacha watoto Uganda walikaa sanaa
 
nilikaribia kusema watafute wazee wa kutoka mkoani moshi.

ila ukweli ni kwamba Uganda haikuwa koloni la Watanzania.

Sijui hizi lugha za "kikoloni" kwa kweli zimetoka wapi.

sio rafiki

Waganda walitueshimu sana na bado wanaendekea kutuheshimu, tusiwabeze.

..Jwtz ilikabidhi utawala kwa Waganda siku chache baada ya Iddi Amin kukimbia.

..Na taarifa za kuanguka kwa utawala wa Amin zilitolewa redioni na Waganda wenyewe.

..Jwtz hawakutaka kutoa tangazo hilo kwa kuogopa kuleta picha mbaya kwamba Tanzania inatawala Uganda.
 
Nyerere alikuwa na moyo safi Sana, ingelikuwa ni PK ameshakushinda akakalia kiti, angechukuwa na nchi yenyewe kabisa na kuwa yake kabisaa dadek.... 😁
 
Back
Top Bottom