katika hali hii nadhani utafiti wa "kisomi" kuhusu kambona na wengine itabidi kukubali kuanzia kwenye simulizi.
Simulizi ndiyo hizo ambazo mwandishi katoa baadhi ya info kutoka kwenye magazeti ya Uingereza ambako Kambona aliwahi kuhojiwa na may be for some reasons habari hiyo haikuchapwa zama hizo kwa kuwa ilikuwa inatoa upande wa pili wa shilingi. Sasa ni simulizi zipi ambazo mnazitaka? Akina Chipaka (Lifa) bado wako hai waje watuambie ilikuwaje wakasundwa gerezani. Tatizo ninaloliona ni kwamba wale walio pro-Nyerere wataongelea uzuri wa Nyerere na umalaya wa Kambona, lakini hawawezi kusema ubaya wa Nyerere na uzuri wa Kambona. Sasa utachukua stori ipi ambayo ni sahihi?
Naomba tuwasiliane na Prof. Issa Shivji nadhani anaweza kutusaidia maana na yeye alipitiwa na panga la Nyerere zama hizo katika harakati za kuandika vitabu. Hapo ndipo unapoweza kuona kwamba kuna vitabu ambavyo vilikuwa na balanced info havikutoka vilibaki kapuni na vile ambavyo vina mazuri ya Nyerere na serikali yake vilitoka haraka sana na kuwa recommended kama vitabu vya rejea kwenye mitaala ya sekondari na vyuo.