Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Kafara, Jun 16, 2007.

 1. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2007
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mengi yamesemwa kuhusu Mzee wetu huyu na sisi tuliokuwa shuleni wakati ule tulilishwa kile ambacho naamini ni sumu. Wakubwa tuelimisheni ukweli kuhusu Mzee huyu.

  [​IMG]

  source: ThisDay November 30, 2007, http://www.thisday.co.tz/News/3077.html


  natumaini waandishi wa historia ya tanzania watampa nafasi yake kwa mchango mkubwa aliyoutoa.

  RIP mzee kambona.

  ===========================
  [h=2]Oscar Salathiel Kambona, alitaka kumpindua Nyerere kwa kushirikiana na wapiganaji wa Umkhonto.[/h]
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jun 17, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ngoja nitoe kumbukumbu yangu, it may have holes.

  Inasemekana kuwa Kambona alikuwa rafiki mkubwa sana wa Nyerere aliyekuwa bestman kwenye harusi yake iliyofanyika London. Katika serikali za kwanza kwanza za Nyerere, Kambona alikuwa ni Waziri mwandamizi aliyekuwa an sauti kuliko mawaziri wengin wote, isipokuwa labda Kawawa. Wakati wa maasi ya 1964, inasemekana pia kuwa ni Kambona na Okello ndio walioongea na kuwatuliza askari waasi. Vile vile katika zile siku 100 za kuelekea Muungano, Nyerere alisikiliza sana ushauri wa Kambona kuliko mtu yeyote kuhuhusu umuhimu wa muungano na structure yake.

  Hata hivyo baadaye uhusiano kati ya Kambona na Nyerere ulianza kuwa mbaya hasa pale Kambona alipoanza kujenga majumba mengi ya kupangisha Dar kwa haraka haraka huku akiwa waziri, jambo ambalo halikuwa tamu kwa Nyerere. Halafu wakati Nyerere anaandika Azimio la Arusha, Kambona alijitokeza kumpinga Nyerere directly kutokana na ile miiko ya uongozi ambayo ilikuwa inaingiliana na zile nyumba alizokuwa amejenga hapo Dar.

  Kwa vile mwishoni lile Azimio la Arusha lilipita na kuanza kutaifisha majumba ya kupangisha yakiwemo na yale ya kambona, basi Kambona akasuka mpango wa kumpindua Nyerere kusudi kusimamisha hiyo operation ya Azimio la Arusha. Waliohusika katika mpango walikuwa wengi sana ikiwa ni pamoja na Titi Mohammed, Lifa Chipaka, Kamaliza, na wengineo. Sielewi mpango wenyewe ulivujaje, lakini wahusika wote walishikwa na kuswekwa kwenye gereza la Keko. Kutokana na umaarufu wake, Kambona alisaidiwa na walinzi wa gereza hilo kutotoroka. Nadhani kwanza alikimbilia Malawi ambako ndiko alikoondokea kwenda kuishi uhamishoni London.

  Kitu kimoja binafsi huwa nadhani kuwa Mzee kambona was right kuhusu vipengele kadhaa vya Azimio la Arusha, hasa ule utaifishaji wa njia kuu zote za uchumi. Hata hivyo kwenye miiko ya uongozi nadhani vile vile alikuwa kakosea. Kilichotakiwa ni kuwa kuandika upya miiko hiyo huku ikiheshimu mali alizokuwa nazo mtu kabla ya kuwa kiongozi.
   
 3. M

  Majige Member

  #3
  Jun 17, 2007
  Joined: Nov 11, 2006
  Messages: 29
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Katika mahojiano na gazeti la new africa huko nyuma Nyerere aliulizwa ikiwa kuvunjika kwa urafiki wake na Kambona ni moja ya mambo yanayomkosesha raha ktk utawala wake,Nyerere alisema hapana na alimshangaa Kambona kama katibu wa TANU alihusika katika maandalizi yote ya azimio la arusha hata kabla halijatangazwa na mwishoni akabadilika kulikana. Kilichomsikitisha Nyerere ni kuwapigia magoti waingereza waliokuwa wakoloni wetu waje wamwokoe wakati wa maasi ya jeshi,wakati tulijidai tunaweza kujitawala.

  Toafauti kati ya hawa ni attitude towards money/richness and how to get it.

  Nyerere alifuata msimamo wa biblia na wa kikomunisti,kuwa ni ngumu kwa tajiri kuingia ktk ufalme wa Mungu,huwezi kuwa tajiri pasipo kutumia nguvu ya watu wengine hivyo kwa kuwa tajiri umenyonya wengine(marxism),pia maneno ya mtakatifu mmoja kuwa unapompa maskini shati humsaidii bali unampa haki yake! Kambona nafikiri hakuona vibaya mtu kutumia akili na nguvu zake kuchuma mali.

  Je historia ya sasa tz tunaweza kuwahukumu vipi hawa waasisi wa taifa letu?mawazo ya yupi yameonyesha ku hold?

  Baada ya kuvunjwa azimio la arusha tumejionea na tunaendelea kuona na kujadili viongozi wetu wanavyofuja mali na kuliibia taifa, rushwa, nepotism, etc.

  Nakubaliana na mawazo hapo juu kuwa implementation ya azimio ilienda haraka sana kabla hatujawa na skilled personnel ya ku takeover na kuendesha taasisi mbali mbali.

  For me Nyerere was right and had the right intention to selfishlessly serve the poor people of tz and lived to his words until his death.
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Jun 18, 2007
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Mzee Kichuguu asante for brief,

  Unajua huwa sometimes na regret kumezeshwa zile nyimbo za nursery ...Kambona ha ha! wivu ulimshinda shauri ya mapesaaa! But kambona in some extent naona alikua sahihi kupinga mpango wa azimio la Arusha.Hata Nyerere mwenyewe nadhani alikuja kugundua kosa.

  ONA LEO MAMBO YA UJAMAA YALIVYO KIMYA KIMYA
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jun 18, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kwenye uendeshaji wa uchumi nadhani he was right; tatizo lake moja tu ni kuwa alikuwa anataka utajiri na akashindwa kujenga hoja ya namna ya kutunza mali za viongozi waliopo madarakani wanazopata kihalali bila kutumia madaraka yao.

  Kwa mfano nyumba ya kupandisha ambamo wamepanga raia wa kawaida haina uhusiano wowote na madaraka ya kiongozi, kulikuwa hakuna haja ya kuitaifisha.
   
 6. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2007
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu kingine pia. Kabla hajahamia London, na labda baada ya uhusiano na mwalimu kuanza kuyumba, Kambona alimwambia mwalimu kuwa hali yake ya afya haikuwa nzuri.

  Mwalimu alimwelekeza Kambona kwenda kutibiwa uholanzi ambako kulikuwa na daktari aliyekuwa rafiki yake mwalimu. Kambona alikaa uholanzi kwa matibabu kwa zaidi ya mwezi. Aliporudi nyumbani, kwa mashangao wa mwalimu, Kambona alijiuzulu uwaziri na ukatibu mkuu wa TANU.

  Ingawa alitaja sababu za kiafya kama sababu za kujiuzulu kwake, bado hazikumconvice mwalimu hivyo ukapangwa mpango wa kumkamata. Sijui ni vipi aligundua mapema na hivyo kuponyoka mapema hadi Nairobi alikopandia ndege kwenda London. Inawezekana pia kuwa hakuridhika na nafasi aliyokuwa nayo. Wakati anaondoka kwenda kwenye matibabu alikuwa waziri wa maendeleo vijijini baada ya azimio la Arusha.

  Inawezekana pia kuwa uhamisho wa kumpeleka kwenye wizara hiyo ilikuwa kumkomoa.
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mzee G,

  Kambona alipokuwa anatoroka kuelekea London, alikamatwa pale Nairobi Airport na askari wa Kenya, akiwa na masanduku mengi ya dola cash, Kenyatta allipompigia Mwalimu simu on whta to do na Kambona, bado akiwa chini ya ulinzi pale Airport, Mwalimu alimjibu kuwa wamuchie aendelee na safari yake,

  ukweli ni kwamba Mwalimu alikuwa happy kuondoka kwa Kambona, ili ampromote Kawawa, ambaye alikuwa yes man!, as opposed na Kambona aliyekuwa objective!
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Jun 18, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nilisoma article moja ya Letters to the Editor iliyondikwa na Oscar Kambona kwenye gazeti la Africa Now kufuatia yale mahojiano kati ya Peter Enahoro na Nyerere aliyoongelea Majige hapo juu; Kambona alisema aliswekwa ndani pale Keko Maximum Security Prison, ila alisaidiwa na walinzi wa pale kutoroka. Na kuwa alitoroka kwa roli la mizigo hadi nchi ya jirani ambayo sina uhakika kati ya Kenya na Malawi lakini nadhani alikuwa amesema alitorokea Malawi. Gazeti hilo lilikuwa Africa Now toleo la 32, December 1983.

  Naona account hiyo siyo kama ilivyorekodiwa na wengi, kwa mfano kitabu hiki. Maelezo ya Gagnija na Mzee ES hapo juu naona ndiyo sahihi zaidi. Nimesoma article nyingine Journal of African Studies inaonyesha likiwa linapinga madai fulani ya Oscar Kambona katika hiyo barua aliyoandika Africa Now. Mwandishi (sikumbuki jina lake ila nitalitafuta tena kurekebisa post hii) ansema kuwa Kambona alikuwa akidai kuwa alisweka ndani na Nyerere ili kupata symphasizers lakini siyo kweli kuwa aliswekwa ndani.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2007
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kambona alikuwa mwongo. Tena alikuwa mtu wa wivu sana. Hakuwapenda Kawawa na Jamal, na mpaka sasa sababu zake sijui. Lakini sababu kubwa ya Mwalimu kumwambia Kenyatta amwachie ni kwamba hakutaka kumfanya Kambona "a hero" kwa kumweka ndani. Baada ya kuondoka Mwalimu aliwang'oa polepole watu wake aliokuwa amewapachika katika idara ya usalama wa taifa na jeshini. Kwa hiyo historically it was a good move.
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2007
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Gagnija,
  Kambona aligundua pale "watu wake" walipoanza kukamatwa mmoja mmoja, akaona hana njia bali kukimbilia Nairobi akipitia Moshi.
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mzee Jasusi,

  Ninakuaminia kwenye hizi kind of ishus, ninaamini kabisa kuwa unayosema ndio ukweli wenyewe kuhsu Kambona, ingawa mpaka leo sielewi kwa nini Mwalimu, alimruhusu huyu Mnyasa kubanda chati, over wabongo, bado sijaelewa!

  Maana ukilifuatialia kwa makini ishu lake, utaona jamaa hakuwa na uchungu kabisaa na bongo, halafu vipi kuhusu mtoto wake mmoja anayesadikiwa kuwa ni shoga, aliyepigwa risasi huko majuu, kuna ka-"tetesi" kuwa someone kutoka kunyumba alihusika ili kumkomoa Kambona ni kweli?
   
 12. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2007
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  Nakubaliana nawe kuwa Kambona alikuwa mtu mwenye wivu sana. Kama nilivyoeleza mapema, kitendo cha kumhamishia wizara ya maendeleo vijijini ndicho kilichomletea ugonjwa uliompeleka kutibiwa uholanzi kwa zaidi ya mwezi. Mwalimu aliwahi kulalamikia tabia hiyo ya wivu. Lakini ni kweli pia kuwa baada ya Kambona kuachia uwaziri na ukatibu wa chama, mwalimu alipata mshituko na akawa amemwandalia nafasi pale Keko.

  Kwamba alitoroka baada ya kuona watu wake wanakamatwa mmoja baada ya mwingine inanipa tatizo kidogo. Nijuavyo, watu wake walikuja kukamatwa Kambona akiwa amehamia Uingereza alipojaribu kupanga kuiangusha serikali. Nafikiri kwa jinsi alivyokuwa maarufu, alikuwa na watu waliomtaarifu mapem juu ya mpango wa kumweka keko hivyo akawahi kuponyoka.

  Ni kweli pia kuwa kumkamata pale Nairobi kungemfanya hero, lakini ni kwa nini mwalimu alimruhusu aende na hayo masanduku yaliyosheheni dola?
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2007
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Gagnija,

  Kweli kuna maswali mengi ambayo hatuna majibu yake ya uhakika. Kambona aliwahi kuwa waziri wa ulinzi. Alichofanya wakati huo aliweka watu wake katika nafasi muhimu jeshini na vile vile katika Usalama wa Taifa. Mzee ES, wakati wa harakati za kupigania uhuru, Mwalimu alikuwa anahitaji msaada wa kila mtu. Kambona, Kawawa, Shaba, Bomani, Eliufoo, you name them. Kuunda huu utanzania usio na misingi ya kikabila ilikuwa kazi kweli kweli. Na hapo ndio tunapaswa kuwashukuru wazee wetu wa TANU.

  Kambona alikuwa na personal ambitions, na nina hakika kama Mwalimu angemwachia madaraka aliyomwachia Kawawa ya uwaziri mkuu kwa mwaka mzima, Mwalimu asingerudi kama rais mwaka 1962. Hiyo ya kumwachia aende London nadhani Mwalimu alimwona less a threat outside the country than inside. Kumbuka this was only 3 years after the 1964 mutiny. With him outside it would be easy to root out his supporters within the army and the intelligence. Na kweli time came to prove Mwalimu right.
   
 14. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2007
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  swali ni je BBC SWAHILI SERVICE London watamkumbuka?
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Nov 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  very interesting... Kawawa bado yuko hai aulizwe...
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Nov 30, 2007
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Self imposed exile....what alternative do you have when you are being harrased, charges are being concocted against you, and much more.....were his concerns about Ujamaa and one party state right on....? Let the debate begin....
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Nov 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Nyani, that is one side of the story.... hata Idi Amin alipokimbilia Saudi alisema anyanyaswa Uganda...
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Nov 30, 2007
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna aliyemwamini Idi Amin kweli....?!?! coz he deserved it anyway
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Nov 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  yeah.. Saudi Arabia...
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Dec 1, 2007
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Still....Kambona and Amin's situations are not even remotely comparable...
   
Loading...