Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

In 1967 after a trip to China in 1965, Nyerere impressed with Mao's style of communism,

wanted to adopt the same system under the guise of Ujamaa. The main doctrine behind Ujamaa was the relocation of peasants into village communes and the nationalization of all industries and properties

Wakuu naomba kuuliza, hivi kweli hii ndio hasa iliyokuwa sera za ukomunisti au it was more than this, au less pia than this, maana kama this was the whole thing, ilikuwaje tukakwama? Huku wa-China wakiyoyoma na mendeleo?
 
you guys take your time to read and dare to ask.. it seems the hero is Kambona, unfortunately he was denied his spotlight.. by jamaa aliyekuwa hataki Watanzania waendelee na aliyemuonea wivu..
 
Mara baada ya kurudi Tanzania, Kambona aliitisha mkutano wa hadhara jangwani na kuahidi kumwaga madhambi ya Nyerere ikiwa ni pamoja na mapesa aliyokuwa amewaibia watanzania. Baada ya mkutano, wengi walitoka wakiwa disappointed kwani hawakupata kile walichotarajia.

Binafsi sikubaliani na mambo mawili kwenye hiyo makala nayo ni sababu za kukosana na mwalimu, na pili ni kurudi kwa Kambona toka Uingereza bila shahada ya sheria. Ukweli haujawekwa wazi.
 
kambona hakurudi na shahada ya sheria kwa kuwa nyerere alimuomba arudi kumsaidia....

nimeumia sana kwa historia ya upande wa pili wa kambona ..alikuwa na vision ..ambYO haikitimia...kwa kuwa vision ya nyerere kiuchumi ilishindwa ..tunaamini kambona angeweza..pia tunagundua kuwa kambona alikuwa charismatic sawa na nyerere ndio maaana akaonewa wivu..ukweli kuwa aliweza kuwanyamazisha wanajeshi waliohasi..unaonesha alikubalika..na hili likawa kidonda kwa nyerere.. hadi kambona anakufa [pamoja na kuwa msasani mazishi ya kambona yakifanyika kinondoni nyerere hakwenda..hakupata kumsamehe..]...

mwanakijiji na wanazuoni wengine ..ombeni kuwahoji kati ya hawa na vitabu viandikwe wakiwa hai...RASHID KAWAWA,MARIA NYERERE,ALI MWINYI,MORISHO SARAKIKIYA[kwa nini aliondolewa ukuu wa majeshi na tangu hapo akawa mtu wa kutanga akiwa balozi wa kudumu..au kwa ajili alikuwa msomi ,na hakupata kuagwa kijeshi hadi mkapa alipomkumbuka ..it was so bad],JOHN MALECELA..DAVID MUSUGURI...kwa kifupi ningependa wazee wote wa zamani wa zamani hawa wawe identified na tuwahoji ILI TUWEKE SAWA HISTORIA WAKIWA HAI....HISTORIA YETU IMEPOTOSHWA SAAAANA!!!!

KAMBONA ANATAKIWA KUPEWA NAFASI YAKE KIHISTORIA ..HATA BARABARA NA HATA SHULE MOJA MBILI KUPEWA JANA LAKE SIO MBAYA..MBONA BIBI TITI NAYE PAMOJA NA KUTUHUMIWA ALISAMEHEWA NA KUENZIWA..???
 
very interesting... Kawawa bado yuko hai aulizwe...

Si nia yangu kukujibizana na wewe, lakini nimefuatilia mitundiko yako mingi katika threads tofauti.
Nakupa ushauri unahiari kuuchukua na kuufanyia kazi au ukauacha na kuendelea kama kawaida.

'SIO KILA THREAD LAZIMA U-COMMENT, MATOKEO YAKE UNAPOTEZA MWELEKEO WAKO WEWE MWENYE BINAFSI NA WACHANGIAJI WENGINE'

Ahsante kama umenielewa na pole kama hujanielewa.
 
you guys take your time to read and dare to ask.. it seems the hero is Kambona, unfortunately he was denied his spotlight.. by jamaa aliyekuwa hataki Watanzania waendelee na aliyemuonea wivu..

Nimeshindwa kukuelewa msimamo wako kuhusu huu mjadala! Is true that we are seeing kambona had a vision! The difference is, you compared Kambona with Idd Amin Dada, and you supported your point by saying also babu faced the same fate! Maybe you have to clear yourself on this!
 
Mwanakijiji anatushutumu sisi kwa kuwa na mwitikio wa kihisia badala ya wa kiakili! Yeye hajioni kama na yeye mwitikio wake ni wa kihisia...anauona wa kwake ni wa kiakili...Lol! Kweli Nyani haoni kundule.

Hapa bana tutakesha na Mwanakijiji. Ikija kwa Nyerere haambiwi wala hasikii la mtu. Inawezekana kabisa Nyerere alimtendea vibaya Kambona lakini hiyo aina maana Nyerere sio Hero. Sasa huyu ndugu yetu hapa anayejifanya Nyerere mamboleo...ukisema kitu chochote tu kile kinachomfanya Nyerere wa zamani aonekane na makosa sehemu flani flani...mwenzenu ananuna na kuwasusia mada
 
1. Mara baada ya kurudi Tanzania, Kambona aliitisha mkutano wa hadhara jangwani na kuahidi kumwaga madhambi ya Nyerere ikiwa ni pamoja na mapesa aliyokuwa amewaibia watanzania. Baada ya mkutano, wengi walitoka wakiwa disappointed kwani hawakupata kile walichotarajia.

Heshima mbele mkuu, very strong point hata mimi nilikuwepo siku ile pale Jangwani it was horrible!

2. Binafsi sikubaliani na mambo mawili kwenye hiyo makala nayo ni sababu za kukosana na mwalimu,

Hapa hapana, unless unao ukweli mwingine tofauti na huu maana Mwalimu, na kundi lake walisema, Kambona alikimbia Azimio La Arusha, version ambayo haiko mbali sana na hii kwenye hii story, kama una nyingine mkuu tuwekee ya sababu za Kambona kukimbia nchi yetu, aliyoiallia macho kuikomboa?

3. na pili ni kurudi kwa Kambona toka Uingereza bila shahada ya sheria. Ukweli haujawekwa wazi.

Again, kama una version nyingine tuwekee mkuu, maana kwenye hili Mwalimu hakuwahi hata kuligusa, WHY? Reading betweeen the lines now, inaonekana Mwalimu hakutaka kiongozi mwingine zaidi yake awe na ujiko mbele ya jamii yetu, yaani eti kuna Kambona ambaye naye ali-sacrifice maisha yake kwa ajili ya uhuru wetu, ilikuwa ni lazima ionekane kuwa ni yeye tu Mwalimu, ili apate ujiko wote! Sasa mnashangaa viongozi wetu wa sasa wanavyoendelea na hizi tabia! Kina Salim kuitwa waarabu just kususdi wasipewe urais, kina Mwandosya kuambiwa ni wageni CCM! hivi huwezi kuona clear kuwa kina Mkapa walikuwa wanaiga tu mifano ya mentor wao Mwalimu!

3. mwanakijiji na wanazuoni wengine ..ombeni kuwahoji kati ya hawa na vitabu viandikwe wakiwa hai...RASHID KAWAWA,MARIA NYERERE,ALI MWINYI,MORISHO SARAKIKIYA[kwa nini aliondolewa ukuu wa majeshi na tangu hapo akawa mtu wa kutanga akiwa balozi wa kudumu..au kwa ajili alikuwa msomi ,na hakupata kuagwa kijeshi hadi mkapa alipomkumbuka ..it was so bad],JOHN MALECELA..DAVID MUSUGURI...kwa kifupi ningependa wazee wote wa zamani wa zamani hawa wawe identified na tuwahoji ILI TUWEKE SAWA HISTORIA WAKIWA HAI....HISTORIA YETU IMEPOTOSHWA SAAAANA!!!!

KAMBONA ANATAKIWA KUPEWA NAFASI YAKE KIHISTORIA ..HATA BARABARA NA HATA SHULE MOJA MBILI KUPEWA JANA LAKE SIO MBAYA..MBONA BIBI TITI NAYE PAMOJA NA KUTUHUMIWA ALISAMEHEWA NA KUENZIWA..???



Mkuu PM,

Hii yako ni very strong na ni fair kuiita final authoritative kulingana na hii ishu, kutokana na all the info tulizonazo at hand, unless kama kuna zingine ambazo hatuna, ila kama hizi tu tulizonazo ni zote, yours is the final authority on the ishu!
 
Cha kushangaza hapa ni watu wanatumia article moja iliyoandikwa na This Day bila hata ya kucite source za hiyo habari kufikia conclusion . Swali langu la kwanza huyo mwandishi alipata wapi hizi habari ? Mimi nadhani ni vizuri kuwa na credible evidence kabla ya kumhukumu mtu.
 
1. it seems the hero is Kambona,

Yes, isipokuwa tu another hero, besides Mwalimu, Mwalimu bado ni the grande, lakini Kambona yuko right behind Mwalimu, or he should be!

2. unfortunately he was denied his spotlight.. na aliyemuonea wivu..

Definetely, by Mwalimu ambaye he never wanted any to share spotlight with him, katika kipindi chake chote cha utawala hakupenda kuwa na competition, ndio maana alizungukwa na all the mediocres, ambao sasa wanatupeleka pabaya, Mao alizungukwa na kuwakubali strong competitors, nina kitabu kinaitwa " The Privete Life Of Chairman Mao" kilichoandikwa na daktari wake private wa zamani, anaitwa Dr. Li Zhisui, kimechapishwa na Random House naomba mkuu wangu MMJ, kitafute uyaone mwenyewe live jinsi Mao alivyokuwa akipigwa mawe na viongozi wenziwe kila alipojaribu kuleta nonesense ideas, sasa itashangaa kwa nini China inayoyoma tu mbele na sisi kina Mkapa ndio wameishia kuwa mabepari sisi tunaimba nyimbo za kumsifu Mwalimu, na Azimio La Arusha tu!

3. by jamaa aliyekuwa hataki Watanzania waendelee

Mwalimu, alipenda sana ujiko wa siasa, alikuwa willing hata ku-sacrifice taifa letu kwa kujali ujiko wake binafsi, alitupelekea kwenye vita vya Uganda, just kuongezea tu ujiko wake kisiasa, alitaka wabongo tuendelee lakini hakuwa an vision ya how to do it na hakutaka kusikiliza wengine au the brain kama kina Professor Rweyemamu, matokeo yake ni here we are completely lost out!
 
Cha kushangaza hapa ni watu wanatumia article moja iliyoandikwa na This Day bila hata ya kucite source za hiyo habari kufikia conclusion . Swali langu la kwanza huyo mwandishi alipata wapi hizi habari ? Mimi nadhani ni vizuri kuwa na credible evidence kabla ya kumhukumu mtu.

Mkuu Rufiji,

Heshima mbele mkuu, ndio hasa maana ya burudani kwenye bulogu, ni papo kwa papo, yaani whatever comes not about yasiyokuwepo, kama una mengine mkuu tuwekee tukate ishu, hizi habari wewe fuatilia kwenye internet lod Kambona utaziona zipo nyingi sana so za Mwalimu pia, huyo mwandishi naamaini amezitoa kwenye mtandao, zikiwa na originated kwenye some library books kutoka London, ila kama una info zingine ziweke mkuu hapa!
 
Cha kushangaza hapa ni watu wanatumia article moja iliyoandikwa na This Day bila hata ya kucite source za hiyo habari kufikia conclusion . Swali langu la kwanza huyo mwandishi alipata wapi hizi habari ? Mimi nadhani ni vizuri kuwa na credible evidence kabla ya kumhukumu mtu.

Hakuna aliyehukumu wala kuhukumiwa hapa. Hiyo article imefungua macho kwa baadhi yetu kuhusu mambo wengine tulikuwa hatujui. Sasa tunachofanya hapa ni kujadiliana....hayo ya hukumu sijui umeyatoa wapi ndugu yangu wewe
 
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firrauni.Kisa kilikuwa kama ifuatavyo Bwana mmoja alikuwa na mkewe ambaye mjamzito wa kuweza kujifungua wakati wowote.Sasa siku moja yule mkewe akasikia harufu ya mishikaki nyumba ya jirani,hivyo akamtuma kijana wake mtogo na pesa ili aende kuomba kununua baadhi ya mishikaki.Kwa bahati mbaya wale wenye mishikaki wakamjibu yule kijana aliyetumwa kuwa mishikaki ilikuwa haiuzwi,ni ya chakula cha nyumbani.

Kijana akapeleka jibu kwa mama yake na haikupita muda yule mama mimba yake ikaharibika.Aliporudi Bwana wake toka kazini akamueleza kisa kizima cha mishikaki mpaka mimba kuharibika.Na kwa akili ya yule Bwana ile mimba iliharibika kwa kukosa mishikaki.Hivyo basi alikwenda kudai fidia kwa wale wenye mishikaki kwakuwa mimba ya mkewe imeharibika.Na wale wenye mishikaki wakakataa kulipa fidia.

Yule Bwana akaamua kwenda kwa Mussa na akamueleza kisa kizima na Mussa akamjibu kuwa mimba haiwezi kuharibika kwa kukosa mishikaki bali ilikuwa ni Kudrah ya Mungu.Hakuridhika na jibu hivyo akaamua kwenda kwa Pharaoh (Firauni),na akamweleza kisa kizima na hukumu ya Firauni ikawa kuwa yule bwana mwenye mishikaki anatakiwa afanye tendo la ndoa na mke ambaye mimba yake imeharibika mpaka atakapopata mimba nyingine na hiyo ndiyo fidia.

Ukweli ni kwamba pamoja na sifa tunazo mpa Nyerere kama Baba wa Taifa lakini bado yako mambo mengi ambayo yamejificha na hii inatokana na wakati ule hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari hivyo kila alichosema nyerere kilikuwa ni ukweli natulikuwa atuwezi kumkanusha.Wako watu kama akina Kambona ambao waliona mbali lakini kwa rigidity yake mwalimu alikana mawazo yao.

sio yote yanayosemwa juu ya Idd Amini ni sahihi,mengine yako EXAGGERATED.Nilipata kuona mkanda mmoja wa video wamwonyesha Amin akila nyama za watu lakini ile ni mikanda ambayo imetengenezwa na watu kwa maslahi yao. Tukumbuke pia ugomvi kati ya Amin na Nyerere ndio umefanya kuenea kwa hiyo kasumba na uongo.Yuko askari mmoja alipata kusema kuwa Tanzania ndio walikwenda vunja daraja la mto Kagera kwa justification ya vita kisa rafiki ya Nyerere ambaye ni Milton Obote arudi tena madarakani.

Ukistaajabu ya Idd Amin Utayaona ya Nyerere.
 
Mwanakijiji,Nyani Ngabu,FMES,

Mimi kinachoniudhi ni zile siasa za kuitana majina sijui makupe,makabaila,wanyonyaji,wahujumu, maadui -- siasa za good vs evil.

Mwanakijiji nakumbuka uliwahi kuita hoja za namna hiyo kuwa ni hoja za kujenga uwoga. Mimi naongeza hizo ni hoja za kujenga chuki,mifarakano, na migawanyiko. Lakini hebu jiulize ni mara ngapi miaka ile ulisikia hoja za namna hiyo?

Historia ya nchi yetu imechezewa kweli kweli. Inachoshangaza ni jinsi wale waliokuwa na ufahamu walivyokuwa wamejikunyata wakati hali hiyo ikiendelea.
 
Mkuu FMES,

Nimeeleza kuwa kuna mambo mawili ambayo siafikiani nayo kwenye hiyo makala ambayo ni sababu za kukosana hawa wawili, na sababu ya kurudi nyumbani bila shahada. Nakumbuka kusoma maandiko yako siku za nyuma na nakubaliana na wewe kuwa Kambona alikamatwa na masanduku yaliyosheheni dola za US pale Nairobi lakini mwalimu akaruhusu wamwache aende zake. Mbali na kazi yake, hakuwa na shughuli nyingine yoyote ambayo ingehalalisha utajiri aliojipatia haraka haraka. Sasa kama kuzuia wizi mwalimu alikuwa anazuia maendeleo ya wananchi, hiyo iko juu ya uelewa wangu. Kwangu mimi kilichowakosanisha ni ufisadi ambao rangi yake ni sawa kabisa na huu unaopigiwa kelele na kina Slaa ambao sijui kama ni waumini wa azimio la Arusha. Fisadi ni fisadi tu, awe Balali, Nyerere, Kambona...

Kuhusu kurudi bila shahada, naamini kuwa wewe FMES una access ya information toka kwenye sources ambazo ni very reliable. Ukifanya utafiti kidogo utagundua kuwa huyu bwana masomo yalimshinda. Sina sababu yoyote ya kumchukia huyu mzee, lakini nasikitika sana ukweli unapogeuzwa kuwa uongo na uongo kuwa ukweli. Mwalimu anayo madhambi yake na moja ni lile la kukumbatia watu wakiharibu sehemu moja na kupelekwa sehemu kuharibu sehemu nyingine. Lakini pia lipo lile la kutorudi nyuma baada ya kumchukia mtu.
 
Mwanakijiji,Nyani Ngabu,FMES,

Mimi kinachoniudhi ni zile siasa za kuitana majina sijui makupe,makabaila,wanyonyaji,wahujumu, maadui -- siasa za good vs evil.

Mwanakijiji nakumbuka uliwahi kuita hoja za namna hiyo kuwa ni hoja za kujenga uwoga. Mimi naongeza hizo ni hoja za kujenga chuki,mifarakano, na migawanyiko. Lakini hebu jiulize ni mara ngapi miaka ile ulisikia hoja za namna hiyo?

Historia ya nchi yetu imechezewa kweli kweli. Inachoshangaza ni jinsi wale waliokuwa na ufahamu walivyokuwa wamejikunyata wakati hali hiyo ikiendelea.

Ni nani alimuiita Kambona malaya...?
 
Ukifanya utafiti kidogo utagundua kuwa huyu bwana masomo yalimshinda

Mkuu wangu G,

Heshima mbele, I mean sina shaka kabisa na maoni yako maana yametulia, ukweli ni kwamba hii ni mara ya yangu ya kwanza kusikia kuwa Kambona, alikimbia shule kwa kutokuwa na uwezo,

Ninawajua kwa karibu sana viongozi wafuatao ambao wanamjua Kambona, kuliko wengine wote, hasa Marehemu Kanyama na Nyirenda, ambao pia walikuwa wa-Malawi, wenziwe none of them aemwahi ku-mention hii kitu na nimewahi kuongea nao wote kwa undani sana kuhusu Kambona,

Than kuna one of his very best friend, Mzee Masha, Lusinde, Sarakikya, Sitta, Hashim Mbita, hawa wote walikuwa marafiki wake wa karibu sana, lakini none of them anayekumbuka kuhusu hii kitu,

Sitaki kutoa hukumu, lakini ninakuahidi mkuu nitarudia tena, one more time kuongea na wale waliokuwa wakimfahamu sana kuskia kama wanalijua hili la Kambona, kukimbia shule, halafu nitakurudia mkuu, lakini ninayaheshimu sana maneno yako.
 
Mara baada ya kurudi Tanzania, Kambona aliitisha mkutano wa hadhara jangwani na kuahidi kumwaga madhambi ya Nyerere ikiwa ni pamoja na mapesa aliyokuwa amewaibia watanzania. Baada ya mkutano, wengi walitoka wakiwa disappointed kwani hawakupata kile walichotarajia.

Binafsi sikubaliani na mambo mawili kwenye hiyo makala nayo ni sababu za kukosana na mwalimu, na pili ni kurudi kwa Kambona toka Uingereza bila shahada ya sheria. Ukweli haujawekwa wazi.

hold on a minute... sikuona hii ina maana kuna mtu alishawahi kuwa na "orodha ya mafisadi" na akapewa uwanja kumwaga madhambi ya Nyerere na Mwalimu mwenyewe alikuwa hai wakati huo akashindwa? Au alitishiwa kufungwa tena?
 
Mwandishi wa makala hiyo kuibalance angeweza kabisa kwenda kufanya interview na watu wengine ambao wanahusika katika hii issue. Kuna watu wapo waulizwe, aulizwe Malecela, aulizwe Kawawa, wapo viongozi wanaojua historia yetu kwanini inaogopwa kuulizwa? Kwanini maneno ya Kambona yachukuliwe kama msaafu kamili?

Mtu mwenye uchungu anaweza kutia chumvi hadithi yoyote na hakuna mtu mwenye uchungu kama mtu mwenye kisasi. Binafsi katika suala hili ninasoma nikiwa skeptic kwa sababu ninafahamu saikolojia ya maumivu; watu wengi maumivu yakianza maisha yao husimama. Na miaka kwa wengine haiponyi maumivu hayo.

Kuna mambo kadhaa ambayo ni ya kweli (facts)

a. Kambona alishiriki kikamilifu na kwa kiasi kikubwa katika Uhuru wa Tanganyika. That is a historical fact.

b. Kambona alikuwa na nafasi mbalimbali za uongozi mara baada ya uhuru. That is a fact.

c. Kambona alishiriki kikamilifu katika kuituliza nchi na hususan wanajeshi baada ya maasi ya 1964 (ambayo hayakuwa ya Tanzania peke yake). That is a fact.

d. Kambona baada ya kutangazwa Azimio la Arusha aliondoka Tanzania na kwenda kuishi Uingereza akijipa uhamisho. That is a fact.

e. Wakati vyama vingi vimeanza Kambona alirudi nyumbani na kujaribu kuwasha moto aliodhania kauacha. Haukuwaka. That is a fact.

f. Kambona alifariki akiwa hajapatanishwa kabisa na Mwalimu. That is a fact.

Now,

Kuna hadithi mbili zinazoendelea. Kuna ile ambayo wengi tulijifunza miaka ya sabini na mwanzoni mwa themanini kuhusu Kambona. Na kuna habari ambayo imeanza kusimuliwa sana pembeni na kumpa ushujaa Kambona (mythification of Kambona) na pia kumtengenezea kisa cha ukuu (legend). Kati ya pande hizi mbili (official version) na ile ya maelezo yake yeye mwenyewe kuna ukweli.

Nasikitika kuwa hakuna mtu aliyepata nafasi ya kumuuliza Mwalimu "what happened to Kambona and why did you exile him". Hata hivyo wapo watu wanalojua jibu hilo ndio maana nimesema "waulizwe". Kwanini hamtaki hilo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom