Mkasa wa Oscar Kambona

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
Oscar Kambona.
Kuna wakati ukitaka kumwangamiza mtu basi muhusishe na Kambona.

Hii ilikuwa baada ya Kambona kukimbilia Uingereza kufafuta hifadhi.
Namweleza Oscar Kambona:

MASAHIHISHO
Katika video nasema Mwalimu Nyerere aliondoka Dar es Salaam kwenda Butiama baada ya kuundwa kwa TANU.

Ulimi umeteleza.

Mwalimu aliondoka Dar es Salaam kwenda Butiama baada ya kuacha kazi.

Kambona akatumwa kwenda kumrudisha President wa TANU New Street.


View: https://youtu.be/u4dHCqHCbPI
 
Shekhe umekuja tena na hekaya zako

USSR
USSR,
Mimi si Sheikh.
Tatizo hili hapa tulilimaliza miaka mingi iliyopita.

Wengi hapa wananiita Mzee Mohamed.
Kwani ndugu yangu kalamu yangu inakubughudhi?

Huu uwanja kila mtu anaandika akipendacho.

Ikiwa labda kuna sheria inayozuia kuandika kwa namna fulani tafadhali nifahamishe.
 
Hiyo SAFINA NA MAARIFA ni udini mtupu yani hapo mwanzon hakuna mkristu aliyeoneshwa
 
Bagamoyo,

Ahsante sana kwa kutuwekea hazina hii.

"Ten Africans," nimekisoma na kipo katika Bibliography ya kitabu cha Sykes.

Martin Kayambo yupo pia katika, "Modern Tanzanians," nacho pia kipo katika Bibliography ya kitabu cha Sykes.

Katika "Modern Tanzanians," Martin Kayamba anasifiwa kwa makubwa aliyofanya na halikadhalika anashutumiwa kwa kuwa kibaraka wa Waingereza.

Kitabu hiki kimekusanya Biography kadhaa za Waafrika maarufu wa karne ya 20 mwanzoni lakini mimi zilizonivutia ni ya Kleist Sykes, Martin Kayamba na ya Ali Juma Ponda na Hassan Suleiman.
 
Nimelisoma yeye mzee wenu haya hayajui kwakuwa sio waislamu na hawakuishi manyema, tandamti, gerezani, magomeni na viunga vinginevyo vya barazani
 
Nimelisoma yeye mzee wenu haya hayajui kwakuwa sio waislamu na hawakuishi manyema, tandamti, gerezani, magomeni na viunga vinginevyo vya barazani
Inside...
Nimeweka link.

Nimeeleza kuwa nimekisoma "Ten Africans" na kipo kitabu hiki katika Bibliography ya "The Life and Times of Abdulwahid Sykes..."

Nikaendelea kueleza kuwa Martin Kayamba yupo pia katika, "Modern Tanzanians," kitabu chenye Biography kadhaa lakini zilizonivutia ni tatu ya Kleist Sykes, Martin Kayamba na ya Ali Juma Ponda na Hassan Suleiman.

Hiki kitabu pia kipo katika Bibliography ya kitabu cha Sykes.

Katika "Modern Tanzanians," Martin Kayamba anaelezwa kama kibaraka na Erica Fiah alipomwandikia taazia baada ya kifo chake.

Erica Fiah alichapa taazia hii katika gazeti lake Kwetu.

Vitabu hivi nimevisoma katika miaka ya 1980.

Ndugu yangu hujafika makamo ya kunikejeli katika kusoma na kuandika wala kunikejeli kuwa mimi ni mtu wa Kariakoo.

Naijua dunia: Durban, J'burg, Sun City, Cape Town, Mbabane, Manzini, Harare, Bulawayo, Lusaka, Maputo, Mombasa, Nairobi, Naivasha, Kampala, Jinja, Entebbe, Addis Ababa, Khartoum, Omdurman, Jazeera, Cairo, Alexandria, Port Said, Ismailiyya, Suez, Damieta, Mehal El Kubra,Tanta, Lagos, Ibadan, Aden, Taiz, Sanaa, Jeddah, Makka, Madina, Dubai, Muscat, North Sea, London, Glasgow, Edinburgh, Cardiff, Berlin, Humburg, Amsterdam, Hague, Geneva, Paris, Le Havre, Iowa City, Chicago, New York, New Jersey, Washington, Istanbul.

1710087957273.png

Durban, Golden Mile​
 
Nimelisoma yeye mzee wenu haya hayajui kwakuwa sio waislamu na hawakuishi manyema, tandamti, gerezani, magomeni na viunga vinginevyo vya barazani
Kama uhuru wa Tanganyika ungeanzia Kariakoo na kumalizika Kariakoo,hakika tusingekuwa na nchi inayoitwa Tanzania.

Kama uhuru wa Tanganyika ungelitafutwa na kupambaniwa na Waislam pekee yake,tungekuwa na nchi inayoitwa Jamhuri ya kiislam ya Tanganyika.

Hicho kitabu cha huyo Ustadhi kinafaa zaidi kusomwa Madrassa na na misikitini.Jamii ya watu wastaarabu yafaa kukipuuza kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom