Ukweli ni huu watawala wametelekeza shule za umma. Kwa sababu watoto wao hawasomi huko

The Burning Spear

JF-Expert Member
Dec 23, 2011
3,445
8,300
Linapokuja swala la elimu nawakumbuka hayati Nyerere na Mkapa, hawa wakubwa walikuwa na dhamira ya kweli kuinua elimu ya Tanzania tofauti na awamu zingine........

Pamoja na katiba mpya kuna haja ya kudai elimu bora shule za umma kwa nguvu zote, Familia zenye uwezo mdogo zinaangamiza watoto kwa elimu dunii....

1.Sina uhakika kama saivi kama bado kuna wakaguzi wa elimu shule za msingi na secondary..

2. Sina uhakika sana kama watoto wa walimu bado wanasoma shule wanazofundisha wazazi wao...

3. Sina uhakika sana kama bado watoto wanzingatia muda wa kufika na kutoka shuleni....

4.Sina uhakika sana kama bado kuna mtendaji wa serikali kuanzia ngazi ya kata hadi Raisi wana uchungu na uduni wa elimu ya Tanzania hasa shule za umma....

5.Sina uhakika sana kama bado kuna walimu wanafundisha wanafunzi kwa upendo na kujitoa kama wanafundisha watoto wao.....

walimu wa UPE Waliupiga mwingi sana.

View attachment 2767792
Shule za ummah advanced level zina faulisha kuliko za private hulijui hilo?
 
Nadhani anazungumzia Elimu bora,siyo kufaulu. Kwani hujui kuna wanafunzi wanafaulu darasa la saba kwenda kidato cha kwanza lakini hawajui kusoma wala kuandika.
 
Sina uhakika hapo tu inaonyesha dhahania tu
Kwanza wakaguzi wa elimu wapo, walimu wapo, maafisa elimu kata wapo
Tatizo kuendekeza siasa kwenye kila taasisi ndio kosa kubwa na huyo mtumishi anapataji nguvu ya kufundisha ikiwa hana motivation yoyote
 
Viongizi wetu wa sasa msamiati wa shule kwao ni majengo. Wako busy sana kuhakikisha majengo ya madarasa yapo, hayo ndiyo wananchi wanaweza kuona. Elimu bora kwao ni uwepo wa madarasa, ndiyo maana Sasa hivi ni shule chache sana zenye upungufu wa madarasa, shule nyingine walimu wanafugia kuku kwenye madarasa ya ziada. Utoaji wa elimu unachangamoto nyingi sana, kwavile viongozi wetu hawapeleki watoto wao kwenye haya madarasa waliyotujengea siyo rahisi kupata mrejesho wa Moja kwa moja wa kile kinachoendelea huko.
 
Hii nchi ngumu sana kulipokuwa na upungufu wa madarasa na kupigwa mapicha mengi watoto wakisomea chini ya miti,ilisemwa wakati huo elimu ilishuka kwa sababu hiyo ya kukosa madarasa na madawati.
Sasa madarasa yapo mpaka ya kusaza tunaambiwa tena hali hii inashusha elimu yetu. Leo tunaambiwa eti waalimu wa UPE walikuwa bora kuliko hawa wa sasa,guys,are you serious or it's just a joke?
Halafu kama kufaulu kumekuwa sasa si kigezo cha ubora wa elimu,tupeni mifano basi huko ambako wanafunzi husomeshwa pasipo kutahiniwa
 
mkipata elimu bora mkajielewa mtatawalikaje! hiyo ni mbinu ya ccm kuendelea kuzalisha vilaza huku watoto wao wakipewa elimu bora ili waendelee kutawala!
 
Back
Top Bottom