DOKEZO Hali ni mbaya sana Shule ya Msingi Kitanda - Mbinga TC

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Shule ya msingi Kitanda ni shule ambayo ipo katika kata ya Kitanda halmshauri ya Mbinga mji ,ni shule ambayo ipo kilometer 15 kutoka makao makuu ya halmshauri ya Mbinga mji na makao makuu ya wilaya ya Mbinga. Shule hii inakadiriwa kuwa na wanafunzi 700+ na walimu wasiopungua 8 lakini chakushangaza Ina mambo ya ajabu sana yanayopelekea shule hii kushuka kitaaaluma kila uchao.Mambo hayo ni kama yafuatayo-

1. Walimu kutofundisha wanafunzi. Huwezi amini toka January mpaka December wanafunzi wametumia kuandika kurasa 10 tu za daftari.
2. Wanafunzi wengi wanarandaranda nje ya madarasa hususan muda wa vipindi Badala ya walimu kuwasimamia wanafunzi kukaa darasani huwa wanawaacha wanafunzi Hawa wacheze mipira muda wa vipindi.
3. Walimu kuwa busy sana na mambo yao mengine tofauti na kazi waliyoichagua.
4. Ulevi na utoro kazini uliopindukia kwa baadhi ya walimu.
5. Utoro uliokithiri kwa wanafunzi.
6. Walimu kutokuwafuatilia watoto wachelewaji wanafunzi wanaenda shule muda wanaotaka wao.

Mambo haya na mengine sana yamepelekea wazazi kususa kutohudhuria kwenye vikao vya shule hivyo kupelekea hali mbaya sana ya kitaaaluma katika shule hii. Naziomba Mamlaka husika hususan idara ya elimu msingi na mkuu wa wilaya ya Mbinga kuinusuru shule hii katika hali. Hali halisi imejidhihirisha katika matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne mwaka 2023.

Screenshot_20240107-174829.jpg
 
Back
Top Bottom