Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Asilimia kubwa ya wasomi wa kibongo wanauzika sana na wengi wanafanya vitu vyao katika nchi za US, UK, UAE , Canada na nyingine nyingi duniani tena wana vyeo vya juu. Hata baadhi ya waajiri kuwaomba Wabongo waliowaajiri kuwapendekeza Wabongo wengine kwa waajiri hao ili nao waajiriwe. Wabongo hao wengi wamejijengea sifa ya uchapakazi, uaminifu, uelewa mkubwa wa kazi zao, kutokuwa walalamikaji.

Uzuri wa Watanzania hawajikwezi kama waganda na wakenya.
 
Mkuu bado namba yetu ni ndogo kulinganisha na wenzetu huko majuu na vilevile inachangiwa na ubnafsi wetumaana watu waTanzania waliopo nje tena kwenye nafasi nzuri ni wagumu kutoa information au kuwa-connect wenzao.
Sio kweli, Ugumu upo Tz, pindi tukija nyumbani kuwekeza na kuwanyanyua wenzetu, watumishi wa serikali wanatuwekea mizengwe mingi. Bureaucracy huanzia embassy zetu, Airport/Bandarini, TRA, wizaras, kiasi tunajiuliza kwanini nisumbuke kiasi hiki, wakati nikienda Kenya au Burundi, mambo ulimswano? Nikiwekeza Kenya, itabidi nitafute kibali cha Mbongo kufanya kazi Kenya, why? Nitampa kazi mkenya. Hatuoni matunda ya wasomi wetu waishio nje, sababu ya serikali ya CCM. Soma mambo yaliyotokea THI na marehemu Dr. Masau, it is very discourage.
 
Katika kupinga hoja yako iliyojaa dharau na kejeli kwetu waTanganyika tulioajiriwa nje, nitaanza na hiyo picha yako. Hiyo Laptop ipo on, na webcam inarecord uchafu unaofanywa na huyo prostitute kwa mikono yake kustarehesha wengine. Kwa akili zako zilivyo ndogo ulidhani its funny kuweka uchafu. Kwa kuwa wewe ni mchafu, mshamba na usiyejua athari za picha kwa wakwe zako au wazazi wako. Kuhusu mada uliyoleta, kuna maswali mengi naomba nikuulize. Je unayo takwimu za wabongo wote wanaoishi nje? Je uliwasiliana na employers wa nje kupata maoni yao kuhusu wabongo? Je uliongea na wabongo wangapi na wa nchi ngapi mpaka ukafikia conclusion hii? Nini nafasi yako na elimu yako kwa ujumla?

Sitaki kubishana na wewe kwa sababu nilishatabiri kuhusu kutokea kwa watu kama wewe kwenye aya ya kwanza kwenye hii mada yangu, kwa hiyo wala sijashangaa kwa sababu najua hulka ya baadhi ya wasomi wa TZ, kwamba hawako tayari kubishana kwa hoja, bali kwa kashfa na kejeli, huo ndio usomi wetu.

Hivi unaweza kufananisha wasomi wetu au hata kuwashindanisha na wasomi wa nchi chache tu za hapa Afrika, kwa mfano majirani zetu na baadhi ya nchi za Afrika Magharibi ambao wakati sisi tukiwa tumelala usingizi wa pono wenzetu walichangamkia ajira za mashirika ya umoja wa mataifa na makampuni makubwa huko ughaibuni na kupata exposure kungali mapema.

Sijasema hakuna wasomi Watanzania huko Ughaibuni bali nimesema hatuna wasomi wengi wenye weledi na wanaoweza kuiletea sifa nchi yetu ukilinganisha na wenzetu wa nchi nyingine za Afrika....

Lakini kwa kukosa ufahamu wa kusoma mada na kuelewa umekimbilia takwimu, na hilo tu ndilo baadhi ya wasomi wetu wanalolifahamu hakuna kingine
 
Mentor, Kwa mtazamo wangu msomi ni yule anayezalisha maarifa baada ya tafakari kubwa na ya muda mrefu. Mtu anayejiuliza maswali na kupata majibu ili aweze kuisaidia jamii hapa duniani.

Naomba nikutolee mfano wa Sophocles, na wale wasomi wa kwanza duniani. Hawa ndio tunaoweza kuwaita wasomi, kwa sababu utafiti wao unagusa kila eneo la maarifa bila kujali kama ni sayansi, biashara, tiba au sanaa.

Will I be correct then as to say, "TANZANIA HAKUNA WASOMI" hence declaring closed your topic that, "WASOMI WETU HAWAUZIKI" ??!
 
Mkuu bado namba yetu ni ndogo kulinganisha na wenzetu huko majuu na vilevile inachangiwa na ubnafsi wetumaana watu waTanzania waliopo nje tena kwenye nafasi nzuri ni wagumu kutoa information au kuwa-connect wenzao.

Nakubaliana nawe kwa asilimia kubwa. Tunapenda kula wenyewe ...............!!!

Ungiangalia wenzetu hata Kenya na Uganda tu huwa wanavutana zaidi yetu ........ halafu sisi kila siku tunawabeza kuwa wakabila. Ukabila wao wakiwa nyumbani, wakiwa nje wanaushirikiano sana kuliko sisi!!
 
Elimu zenyewe ndo hizi za kubadili matokeao na kufaulisha wanafunzi ili wasichafue rekodi za watawala!
Unategemea ni products gani zitatoka?
Natabiri kuanzia miaka kumi ijayo nchi hii, products zitakazotoka sio tuu hawatauzika nje ya nchi bali hawatahuzika humu humu nchini.
Halafu kuna watu humu wanatokwa na povu kutetea kwamba wasomi wetu wanauzika! Lakini ni hawa hawa wanaopiga kelele kwamba mfumo wetu wa elimu haufai, sasa mfumo usiofaa utawezaje kuzalisha wasomi bora watakaomudu kuingia kwenye ushindani wa soko la ajira huko ughaibuni?
 
Asilimia kubwa ya wasomi wa kibongo wanauzika sana na wengi wanafanya vitu vyao katika nchi za US, UK, UAE , Canada na nyingine nyingi duniani tena wana vyeo vya juu. Hata baadhi ya waajiri kuwaomba Wabongo waliowaajiri kuwapendekeza Wabongo wengine kwa waajiri hao ili nao waajiriwe. Wabongo hao wengi wamejijengea sifa ya uchapakazi, uaminifu, uelewa mkubwa wa kazi zao, kutokuwa walalamikaji.

Kwa hiyo hushawishiki kukubali mapendekezo ya kubadili mfumo wa elimu kwa vile huu uliopo unatoa wasomi wanaouzika kama ulivyosema?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nakubaliana nawe kwa asilimia kubwa. Tunapenda kula wenyewe ...............!!!

Ungiangalia wenzetu hata Kenya na Uganda tu huwa wanavutana zaidi yetu ........ halafu sisi kila siku tunawabeza kuwa wakabila. Ukabila wao wakiwa nyumbani, wakiwa nje wanaushirikiano sana kuliko sisi!!
Mifano ni mingi ukienda kwenye taasisi za Utalii kama mahotelini na kwenye Bank zetu hapa nchini, nafasi nyingi za maana zimeshikwa na Wakenya na waganda na hivi sasa wapo waafrika Magharibi wanaoanza kuchangamkia ajira za hapa nchini na hata waajiri wanakiri kwamba hatuwezi na hata tukipewa nafasi hatuna ufanisi. Hivi sasa kila kampuni inatafuta faida hivi unafikiri bado kuna kubebana kama enzi za mashirika ya umma?
 
Sitaki kubishana na wewe kwa sababu nilishatabiri kuhusu kutokea kwa watu kama wewe kwenye aya ya kwanza kwenye hii mada yangu, kwa hiyo wala sijashangaa kwa sababu najua hulka ya baadhi ya wasomi wa TZ, kwamba hawako tayari kubishana kwa hoja, bali kwa kashfa na kejeli, huo ndio usomi wetu.

Hivi unaweza kufananisha wasomi wetu au hata kuwashindanisha na wasomi wa nchi chache tu za hapa Afrika, kwa mfano majirani zetu na baadhi ya nchi za Afrika Magharibi ambao wakati sisi tukiwa tumelala usingizi wa pono wenzetu walichangamkia ajira za mashirika ya umoja wa mataifa na makampuni makubwa huko ughaibuni na kupata exposure kungali mapema.

Sijasema hakuna wasomi Watanzania huko Ughaibuni bali nimesema hatuna wasomi wengi wenye weledi na wanaoweza kuiletea sifa nchi yetu ukilinganisha na wenzetu wa nchi nyingine za Afrika....

Lakini kwa kukosa ufahamu wa kusoma mada na kuelewa umekimbilia takwimu, na hilo tu ndilo baadhi ya wasomi wetu wanalolifahamu hakuna kingine
Mfano fani ya medicine, kuna watanzania wengi mno wanatumainiwa sana nje, Engineering wapo wabongo NASA, Boeing na makampuni makubwa na nafasi kubwa. Tatizo lipo katika serikali yetu. Tukitaka kuja kuwekeza tunaletewa mizengwe. Hivyo wengi wameamua kuachana na serikali ya CCM
 
Kwa hiyo hushawishiki kukubali mapendekezo ya kubadili mfumo wa elimu kwa vile huu uliopo unatoa wasomi wanaouzika kama ulivyosema?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Swali zuri kwa kweli.
Mimi nilitarajia tutaweka vichwa pamoja na kutafuta suluhisho kwa maana wakati huu ambapo kuna mjadala mzito kuhusu mfumo wetu wa elimu, tunatakiwa kutoa maoni na mapendekezo kuhusu namna bora ya kuboresha elimu yetu hapa nchini ili tumudu kuingia kwenye ushindani katika soko la ajira na si huko ughaibuni tu bali pia hata hapa nchini, lakini badala yake tunaingia kwenye kubishana kusiko na kichwa wala miguu
 
BAK uko sahihi sana mkuu, yaani mimi ninamarafiki ambao wameajiriwa UK, USA, CANADA NA SA ambao kwanza utashangaa mambo wanayoyafanya. yaani mimi nilimshangaa mama mmoja anaitwa Hulda swai yaani ukiona team yako na jins alivyo excell utashangaa. ana run centre yenye watu zaid ya 100 ambao wanafanya kazi chini yake na wote wanaperform vizuri.

Nilisikitika sana alipoambiwa arudi Tz na mkuu wa nchi watu wakamtisha ukirudi Tz utafanyiwa majungu bora uendelee kujilia bata wako huko CSIR.

Nimependa Analysis yako...upo juu!! Bora huyo mama hajarudi...si unakumbuka yaliyomkuta Dr. Mahalu(yule wa Institute ya Moyo-THI nadhani) ,manake kafanywa kitu mbaya na serikali kupitia NSSF..dah Bongo pagumu sana!!
 
Dar ina watu 4.5M kama sikosei... Kama bookshop za jiji lote la Dar zinafika 50... Naomba nifutwe kuwa member wa JF! Na kama jiji hili lina public library at least moja/mbili kwenye kila jimbo la uchaguzi iwe la CCM au CUF au CDM naomba nifukuzwe uanachama JF.

Kama mahudhurio ya wasomaji kwenye maktaba kuu ni sawa na mahudhurio ya Harusi moja ya pale diamond Jubilee naomba nifukuzwe Membership ya JF.

Kama maktaba kuu mwaka huu imenunua vitabu copy 1M kwa mwaka naomba kufukuzwa JF

Kama posho za waBunge kuna cku zimechelewa kulipwa kwa wiki moja ... Futilia miki kwenye membership ya JF.
 
Najua kauli yangu hii itawakera wengi hususan hao wanaojiita wasomi, lakini najua kwamba ukweli mara nyingi huwa unauma sana.

Katika orodha ya nchi za Afrika ambazo wasomi wake wanaibwa na kusombwa na kupelekwa huko Ulaya na Marekani kufanya kazi , Tanzania haitajwi kabisa.

Watanzania wengi wanaokwenda nje kufanya kazi, ni vibarua zaidi, wenyewe wanajiita wabeba mabox, na hata kama ni wasomi, basi utawakuta wanafanya kazi ambazo huwezi kusema zitaweza kuisaidia nchi.

Hata hivyo wapo Watanzania wachache sana ambao wamenunuliwa nje na kufanya kazi huko kwa sababu ya uwezo wao kiufahamu katika taaluma zao.

Lakini hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukidumaza akili zetu.
Mara nyingi wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipiga kelele kuhusu haja ya Serikali kubadili mfumo wa elimu ili kuweza kuwashindanisha wasomi wake na wasomi wa nchi nyingine duniani lakini jambo hilo limeonekana kama vile halina maana.

Najua serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi imeshawahi kubadili mitaala ya elimu mara kdhaa, lakini ninachojaribu kusema hapa ni je tabia ya wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani badala ya kuelewa imekomeshwa kwa kutafuta chanzo chake?

Ukweli ni kwamba, ni vigumu kwa wasomi wengi wa Tanzania kushindana kwenye soko la dunia kitaaluma kwa sababu, hawakuandaliwa kuwa watu wanaofahamu, bali wameandaliwa kuwa watu wanaokariri …
[/ QUOTE]

Haahaaa....shule na elimu zetu majanga matupu. Chuo kikuu, watu wanasoma past papers na madesa kwa bidiii kuliko kusoma vitabu. Na wakiingia mtaani self learning haipewi umaanani. Kwa mfano ni watu wachache sana wanajisomea wenyewe vitabu na majarida mbalimbali yanaweza kupanua upana wa mawazo na uelewa wa mambo baada ya kutoka chuoni.... Na hata postgraduate courses, wengine wanawalipa watu kuwaandalia report za tafiti zao za programmes wanazofanya. Elimu yetu ni majanga...na mitazamo yetu ni majanga mara mbili.
 
Mkuu bado namba yetu ni ndogo kulinganisha na wenzetu huko majuu na vilevile inachangiwa na ubnafsi wetumaana watu waTanzania waliopo nje tena kwenye nafasi nzuri ni wagumu kutoa information au kuwa-connect wenzao.

Kenyansabroad.org:: KCA, Kenyans, Kenyan Diaspora, Kenyan Community Abroad, Kenyans overseas

The Kenyan Community Abroad (KCA) is a socio-political, non-partisan organization which is registered in Washington, D.C. and Rhode Island state in the USA. It is composed primarily of Kenyans living outside Kenya. KCA was founded in March 1997 with a view to giving Kenyans abroad a platform on which to exchange views and help bring change back home. KCA seeks to facilitate the establishment of Chapters in locations around the world where there is a significant Kenyan presence.Among the stated objectives are to:
􏰀 Provide a forum where people of Kenya who reside abroad can engage in intelligent discourse on economic, political and social issues that affect Kenyans abroad and home;
􏰀 Fight for transparency and accountability in the Kenya government;
􏰀 Facilitate the dissemination of important policy decisions to the Kenya citizenry;
􏰀 Campaign for the rule of law and democratic governance in Kenya and campaign for a modern civil society based on equality before the rule of law;
􏰀 Campaign for sound and just economic policies in Kenya aimed at empowering the Kenyan populace;
􏰀 Provide a forum for the sharing of the unique Kenyan cultural heritage in all its diversity and particularly inculcate in Kenyans born abroad the rich history and ethos of the people in their land of ancestry;
KCA believes that:
1. Fellow Kenyans need and deserve a clean and honest government that will bring economic, political and social growth. The Kenyan Community Abroad believes in taking the government away from a few individuals and putting it back in the hands of the people's institutions - Legislature, Executive and the Judiciary, where it belongs;
2. That Kenya is, and shall continue to be, a Republic, and shall be indivisible and shall be governed by a democratically elected government;
3. That Kenyans are a one people in their ethnic and religious diversity and that their destinies are yoked with that of their motherland;
4. That the challenges that face Kenya as a nation and as a distinguished member of the society of nations transcend any ethnic or regional interests and that KCA shall only champion the cause of one nation and one people;
5. That Kenya must pursue and openly cultivate the growth of democratic institutions enshrined in the new Kenyan Constitution;
6. That all Kenyans are equal and all have a stake in the welfare of their nation and they have a right to pursue for themselves and their family an honest living under the laws of Kenya;
7. In the sanctity of human life as the highest level of creation and in the UN Universal Declaration of Human Rights of 1948 and in the various human rights covenants and other international human rights instruments.
To send us your queries or suggestions Click Here . You may post your comments to: The Secretary, Kenya Community Abroad, PO Box 2805, Washington, DC 20002, USA

Kisha linganisheni na hii hapa chini:

WABONGO UGHAIBUNI: TANZANIANS LIVING ABROAD ILLEGALLY MAY BE RESCUED - FOREIGN AFFAIRS MINISTRY
 
Dar ina watu 4.5M kama sikosei... Kama bookshop za jiji lote la Dar zinafika 50... Naomba nifutwe kuwa member wa JF! Na kama jiji hili lina public library at least moja/mbili kwenye kila jimbo la uchaguzi iwe la CCM au CUF au CDM naomba nifukuzwe uanachama JF.

Kama mahudhurio ya wasomaji kwenye maktaba kuu ni sawa na mahudhurio ya Harusi moja ya pale diamond Jubilee naomba nifukuzwe Membership ya JF.

Kama maktaba kuu mwaka huu imenunua vitabu copy 1M kwa mwaka naomba kufukuzwa JF

Kama posho za waBunge kuna cku zimechelewa kulipwa kwa wiki moja ... Futilia miki kwenye membership ya JF.

Waandishi wa vitabu wenyewe hakuna na kama wapo ni wale wa kukopi na kupesti na ndio maana vina makosa kibao kwa sababu ya lugha kugongana
 
Mbona umewasahau kina Nyani Ngabu na Kiranga

Huh!?!?! Mimi ni mbeba maboksi tu. Kwenye medani za wasomi wa spesho skul sipo kabisa aisee.

Darasa la saba nilifeli, form four nikafeli, form six ndo sikwenda kabisa.

Baada ya kumaliza form four nikaanza kupiga boksi na sasa ninakimbiza mbaya.

I am an uber-proud blue-collar prezdaa wa wabeba maboksi wa kibongo kote ulimwenguni.

Wabeba maboksi oyeeeee......
 
Back
Top Bottom