t blj
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 7,143
- 17,026
Sitaki kubishana na wewe kwa sababu nilishatabiri kuhusu kutokea kwa watu kama wewe kwenye aya ya kwanza kwenye hii mada yangu, kwa hiyo wala sijashangaa kwa sababu najua hulka ya baadhi ya wasomi wa TZ, kwamba hawako tayari kubishana kwa hoja, bali kwa kashfa na kejeli, huo ndio usomi wetu.
Hivi unaweza kufananisha wasomi wetu au hata kuwashindanisha na wasomi wa nchi chache tu za hapa Afrika, kwa mfano majirani zetu na baadhi ya nchi za Afrika Magharibi ambao wakati sisi tukiwa tumelala usingizi wa pono wenzetu walichangamkia ajira za mashirika ya umoja wa mataifa na makampuni makubwa huko ughaibuni na kupata exposure kungali mapema.
Sijasema hakuna wasomi Watanzania huko Ughaibuni bali nimesema hatuna wasomi wengi wenye weledi na wanaoweza kuiletea sifa nchi yetu ukilinganisha na wenzetu wa nchi nyingine za Afrika....
Lakini kwa kukosa ufahamu wa kusoma mada na kuelewa umekimbilia takwimu, na hilo tu ndilo baadhi ya wasomi wetu wanalolifahamu hakuna kingine
Pamoja sana dada! Tatizo la wasomi wetu ukitoa mada za kuwapinga wanadhani wewe si msomi na hujui chochote! Na automatically unakuwa adui kwao
Elimu yetu ni ya kukariri sana ,matokeo yake watu wanafaulu kwa maksi za juu lakini maarifa hakuna! .na ndio sababu hatuwezi kushindana na wenzetu kwenye nafasi za kimataifa , wa Tz compitent wapo lakini ni wachache .
Elimu ni maarifa anayobaki nayo mtu baada ya kumaliza shule, wala si kurundika vyeti .na ukilijua tatizo linalokusumbua ujue hauko mbali kupata suluhisho lake ,bahati mbaya wasomi wetu hawataki kujua mapungufu ya elimu yao!