Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Huh!?!?! Mimi ni mbeba maboksi tu. Kwenye medani za wasomi wa spesho skul sipo kabisa aisee.

Darasa la saba nilifeli, form four nikafeli, form six ndo sikwenda kabisa.

Baada ya kumaliza form four nikaanza kupiga boksi na sasa ninakimbiza mbaya.

I am an uber-proud blue-collar prezdaa wa wabeba maboksi wa kibongo kote ulimwenguni.

Wabeba maboksi oyeeeee......
Ha ha ha ha ha ha haaaaaaaa

Copy to gfsonwin
 
Last edited by a moderator:
Mbona umewasahau kina Nyani Ngabu na Kiranga

Kiranga matendo yake yanaashiria Kuna kashule kidogo kamelala, yaani substance ipo. Lakini Bwan'Chuchu Ngabu majanga, na kwa vile mtoni hakuna ubabaishaji wa mission town Nina uhakika mzee wa miafrika ndivyo ilivyo anapigika, huenda ana laptop Tu ya kupostia JF and then homeless. Maana hata ukishaviosha vibibi haulali hapo hapo kwenye jumba la wazee lazima utafute pa kujistiri
 
Last edited by a moderator:
Kiranga matendo yake yanaashiria Kuna kashule kidogo kamelala, yaani substance ipo. Lakini Bwan'Chuchu Ngabu majanga, na kwa vile mtoni hakuna ubabaishaji wa mission town Nina uhakika mzee wa miafrika ndivyo ilivyo anapigika, huenda ana laptop Tu ya kupostia JF and then homeless. Maana hata ukishaviosha vibibi haulali hapo hapo kwenye jumba la wazee lazima utafute pa kujistiri

Hahahaaaa uzuri ni kwamba maoni yako na matamanio yako si uhalisia wangu! Hivyo huna uhakika kama napigika au nakula bata. Kwa kifupi ni hujui. Hivyo acha kujifanya mjuvi wa usiyoyajua.
 
umezungumza ukweli mtupu mkuu, kama tunataka kweli kulikomboa taifa hili lazima tuanze kurekebisha mfumo wetu wa kielimu kwanza, hapa partisan politics lazima ziwekwe pembeni na tufanye kazi kama taifa moja......mhe Mbatia kalianzisha hilo hivyo ni kazi kwetu kuliendeleza kwa faida yetu sisi na kizazi kijacho.
 
Hahahaaaa uzuri ni kwamba maoni yako na matamanio yako si uhalisia wangu! Hivyo huna uhakika kama napigika au nakula bata. Kwa kifupi ni hujui. Hivyo acha kujifanya mjuvi wa usiyoyajua.

Weka picha ya home kwako hata ya uongo...

Ila hauli vumbi kama sisi kwa hiyo uko juu bila kujali aina ya maisha huko mferejini
 
...chngeni sana jmani..., hizi kauli mnazotumia kjdharau wa-tz ndizo wanazotumia wnzenu kjinufahisha ktka nchi yenu na nyie mkbaki klalama tu..., hacheni kkariri maneno ya wanasiasa bwna...!
 
Usikute unachanganya ...mambo mimi nachojua watanzania hawapo wengi nje kwa sababu hawakuchangamkia fursa za kwenda nje kama wenzetu wakenya, waganda, waghana na wanigeria.....wenzetu vitu kama greencard huchangamkia sana ikilinganishwa na sisi.....jaribu kuchunguza...
 
Hivi mtu akisema ughaibuni anamaanisha ni wapi?
Mkuu hii mada ni nzuri sana, japo siipendi picha yako. 2000, niliwa Washington DC katika mkutano wa watanzania waishio DMV na Rais Mkapa pamoja na waziri wa nje then alikuwa Mh JK. Hii ilikuwa kauli ya hao viongozi "Nyinyi tunataka mbaki hapahapa mtufundishie watoto wetu" Nikamsikia Membe nae akisema vitu kama hivyo nilipokuwa UK. Tofauti kubwa na viongozi wa Kenya, Burundi nk wanaojivunia wasomi wao. Can you Imagine JK yupo proud na yule looser Hasheem Thabeet ambae yupo bench, kiliko yule bingwa wa upasuaji wa moyo alipokuwa anawika Texas? Imagine JK anamsafirisha Diamond na kundi lake kwenda nje kwenye ufunguzi wa mashina, lakini serikali haina pesa kuwalipa posho madaktari. Serikali ya CCM ni balaa na janga kwa wasomi
 
Hiv wewe ukisikia watz unapata picha gani.? we unajua watz ni hao unawaona kwenye tv? tatizo sio utanzania, tatizo ni attitude.. kama una akil za mende uctarajie makubwa.. watu tumeajiriwa na makampuni moja kwa moja huko unakokuita nje , na bado tuna excel .. we umekalia wasomi cjui nini.... we unataka kila mwenye nafas nje ajitangaze? tatizo jingine ni wewe na viongoz wako wasiothamini uwezo wa watu.....endeleeni kuhubiri ujinga mkshtuka tu, kumekucha.. tunaanza kuwatawala!!!
 
Wasomi bora wakae uko ughaibuni, waangalie akina prof Ndulu wa benki kuu anavyo endeshwa na wanasiasa uchwara akarusu pesa za low quality kutengenezwa, kabla ya kuja bongo tulisikia sana mazuri kutoka kwao. Hakuna viwanda unategemea wataalamu wa kushindana kimataifa kutokea wapi? hao wachache n wale waliosoma zamani na baadhi walipata sponsor kusoma nje ya nchi
 
Hilo la ubinafsi lipo kwa baadhi na hilo la uchache limesababishwa zaidi na uzalendo hasa miaka ya nyuma, miaka ya karibuni hili la uzalendo limepungua.

Mkuu bado namba yetu ni ndogo kulinganisha na wenzetu huko majuu na vilevile inachangiwa na ubnafsi wetumaana watu waTanzania waliopo nje tena kwenye nafasi nzuri ni wagumu kutoa information au kuwa-connect wenzao.
 
Huu uchafu tuliokuwa miaka hii nayo inaweza kuitwa elimu!!!


Kwa hiyo hushawishiki kukubali mapendekezo ya kubadili mfumo wa elimu kwa vile huu uliopo unatoa wasomi wanaouzika kama ulivyosema?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Itasaidia kuamsha hisia za wabongo kutamani kuja mtoni maana kwa sasa tunaambiwa wapiga box mmepigika sana due to recession. Ila tukiona crib tutajua financial crisis sio issue

2286331403
 
Hili Serikali imeliona na ndiyo sababu kwa sasa kuna kitu kinaitwa competence-based curriculum ambayo ni tofauti na ile ambayo ilikuwa teacher-centred. Tatizo ni kwamba bado walimu hawajaelewa jinsi ya kuimudu kwa hoyo bado wanafundisha wanafunzi past papers ili waweze kufaulu mitihani. Ila kama walimu watapata orientation hii hali itabadilika na hivyo kuwafanta Watz kuweze ku-compete kwenye soko la ajira au kuwa na ujuzi wa kujiajiri wenyewe.

Hizo ni porojo tu, Mwanafunzi wa leo anayemaliza darasa la Saba mwambie ataje tu hata mikoa 5 ya tanzania na nchi walau 10 barani afrika kama atakwambia.
Badala ya kuitanua elimu tunazidi kuishusha na leo watoto wanasoma ramani za kata, wakifika sekondari hakuna mazoezi ya vitendo hata kidogo yanayopelekea watoto kuelewa bali ni ile ya kukariri na kuona majibu yanatoka yaliyoko katika vitabu na ikitokea vinginevyo hakuna anayeweza kuelezea.
 
Ni Hawa Wasomi wa SASA wa MAZIWA wa AZIMIO LA ZANZIBAR... Sababu Kabla ya HAPO Jaribu kusogelea University of Botswana... angalia FACULTY zake uone kuna wanani; University of Namibia; University of Cape Town; University of North Carolina; University of San Diego n.k

Isipokuwa wasomi wetu wa AZIMIO la ZANZIBAR wana attitude kama WaKENYA... Hawajali; Wanajisikia; Wanajibagua na Hawajui The Real World... Mfano Hadi Leo wanadhani CCM ni CHAMA CHA Kijamaa... Wako NYUMA kwanini Wasiachwe ???
 
Naamini mimi ni msomi. Najiamini ndo maana nakataa hayo uliyoandika.
Hukutafuta sababu za ziada kujua kama kweli idadi ya wa-TZ walio nje kikazi ni wengi au wachache. Pia unastahili ufahamu ni nini kilichowafanya hao unaodhani ni wazuri kujaa nje ya nchi.

Kubwa zaidi ni kwamba kigezo chako ni mfilisi. Hakina maana yoyote ktk JF. Unawezaje kutumia idadi ya walio nje kikazi kuwa ndo kigezo cha ubora wa elimu ya nyumbani?

Nigeria ina watu wengi huko Duniani, Filipino nao wako kwa kiasi kikubwa. Angalia wasomali, waganda na watu wa Ethiopia au hata wayahudi. Sababu za wao kwenda nje unaziona au huzioni.

Sisi TZ hatukuwa na sababu kwa miaka mingi na kwa kiasi kikubwa siasa zetu zilituaminisha kwamba ni bora kuliko nje ya nchi. Kwa ubaya au hata uongo hiyo ndo ilikuwa hali halisi na tukaamini. Ondoa hiyo dhana kwamba ni kwa sababu ya ubovu wa usomi wetu.

Hebu unda sababu upya.
 
Back
Top Bottom