Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Ninaposikia wanafunzi waliomaliza darasa la saba hawajui hata mikoa 5 ya Tanzania au nchi kumi za Afrika, natumaini unatania.

Ukitaka kujua ukweli wa haya jifanye SEKI tu walau kwa dakika 10 katika primary yeyote utabaini ukweli wa hili.
Sitaki kukutafunia sana, this is just a clue kukupa hamasa ya kujionea.

Raha ya kitu utest mwenyewe sio uhadithiwe.
 
ni kweli tunao mfumo mbaya wa elimu unaowaandaa watanzania kukariri ili wajibu maswali kwa kuwa lengo lao ni kuahiriwa badala ya kutumia elimu yao kupambana na mazingira yanayowazunguka, na zaidi hata level ya university pia watu wanakaririshwa na waadhiri wao ili kujibu maswali badala ya kupima ufahamu wao ukitaka kujua nenda maofcn uangalie graduates hawana kipya katika kuboresha kazi bali mzoea tu ni kwa kuwa walikariri ili kuweza kujibu maswali na walipo maliza wakasahau, "education means something remaining in brain after forgeting every thing leant" tafsiri ya hili ni kuwa taifa hili halina wasomi wengi ila lina watu walikwenda shule wakapata vyeti kwa mfumo wa kukariri na ndiyo maana maendeleo hayapatikani hatuna wabunifu kwa sababu tunaodhani ni wasomi siyo kwa kuwa mfumo wa elimu haukuwafunza kuwa wabunifu bali watu wa kukariri ndo maana tunawashabikia wanaotaja takwimu kichwani bila kujali kama wanachosema ni logical au la, kwa sababu mfumo wetu wa elimu umetufanya tushindwe kutofautisha kati ya facts na trueth, hii ndiyo tanzania yetu.
 
Enzi hizo tulizijua hadi nchi zinaitwa Vanuatu na Tuvalu....

But siku hizi Mulugo hajui hata Zimbabwe na Pemba ziko wapi halafu mnawalaumu graduates wa bongo kwa kushindwa kujiamini. Kansa kubwa kuliko zote kwenye elimu ya vyuo vikuu vya bongo ni wanafunzi kuangaliziana na kuingia na makaratasi yenye majibu, Mzumbe ndio wanaongoza ligi. Graduate asiyejiamini hata kujibu exams akaingia na majibu a.k.a MIG au akakaa kwenye mtandao wa kuangaliziana darasani hawezi kuongoza Portfolio hata $10,000.

Hii nchi CCM wameifikisha pabaya sana.

You sick ma dude.

Halafu wewe bottom line yako ya usomi ni figure ya portfolio tu.

Mbona Dick Russo kaongoza portfolio zote zilizopitia NYSE bila hata ki degree cha kwanza uchwara cha Almeida College?
 
Ukitaka kujua ukweli wa haya jifanye SEKI tu walau kwa dakika 10 katika primary yeyote utabaini ukweli wa hili.
Sitaki kukutafunia sana, this is just a clue kukupa hamasa ya kujionea.

Raha ya kitu utest mwenyewe sio uhadithiwe.

Nafuatilia habari zinazosema kuna vijana wengi tu, way in excess of a tenth, wanamaliza darasa la saba bila kujua kusoma proficiently, kwa hiyo siwezi kushangaa sana.
 
Kiranga, Nyani Ngabu,

..kwa mtizamo wangu wa-Tz hawapewi hata ile elimu ambayo tumeambiwa wanatakiwa kupewa.

..sasa ukiongezea na tatizo la lugha ya KIINGEREZA basi ndiyo tunakuwa tumeharibu kabisaaaaaa.

..matokeo yake ni wahitimu ambao hawezi hata kubabaisha kwamba wanajua kitu fulani.

NB:

..kwa kweli hizo story zenu za "big-jii" zimenikumbusha mbali sana.
 
Enzi zetu wanafunzi wa darasa la nne wakipata muda katikati ya vipindi lazima kucheza na atlas sana.

Mtu lazima uulizwe kuonesha Kamchatka na Novaya Zemlya ziko wapi, up to this day nakumbuka vimiji vya Siberia huko kwa sababu tulikuwa makini kujifunza. Wenyewe. Outside of homework and teachers assignments.

Ninaposikia wanafunzi waliomaliza darasa la saba hawajui hata mikoa 5 ya Tanzania au nchi kumi za Afrika, natumaini unatania.

Why, by darasa la nne nilikuwa na kijidaftari kilichorekodi karibu nchi zote za Afrika, miji mikuu, marais, idadi ya watu, lugha kuu na hela zinazotumika.

Huku sikosi kusikiza kipindi cha RTD cha Chris Katembo "Mkoa kwa Mkoa" kikinihabarisha kuhusu tamaduni na habari za mikoa yote ya Tanzania, pamoja na kingine kilichozungumzia nchi za Afrika, "Kutoka Afrika" or something like that, Ku supplement kitabu cha "Wafanyakazi wa Afrika" cha darasa la nne, kilichofundisha kuhusu kilimo cha pamba Sudan kwa ramani za kuonesha Wadi zote, mpaka uchimbaji wa dhahabu namakaa ya mawe huko Witwatersrand.

Hivi vipindi, pamoja na vile vilivyokuwa vikitoa madarasa ya shule kwa redio, bado vipo au ni historia sasa?

Mtoto wa darasa la nne leo ukimuuliza Wadi Hadad (aka Wad al Hadad) au Witwatersrand ni nini anaweza kujibu? Labda utamuonea, unaweza kukuta hata mhitimu wa leo wa Chuo Kikuu hajui !

I will spare them Novaya Zemlya and Kamchatka for now. Lest some may not be able to locate Lake Tanganyika on the globe.

usinikumbushe enzi zile miji mikuu yote tuliijua kwa kichwa sitokaa nisahau mji mkuu wa Bulgaria uliitwa Sophia.
unakumbuka kubandika stempu?? yani posta walikuwa wanatoa stempu ambazo zilikuwa zinaonyesha vitu mbali mbali vya tanzania kuanzia mazao hadi wanyma na ndege. basi utanunua ubandike ili mwisho posta wakiita shindano upeleke.

imagine mtu unabandika na kusema kama ni zao linapatikana wapi (mkoa) na kama ni mnyama hivyo hivyo. miji mikuu yote ya kila mkoa tulijifunza na zao la biasahra la kila mkoa leo hii.............

bureeeeeeee kabisa waalim tumebaki hatujui tufundishe nini.
 
..kwa kweli hizo story zenu za "big-jii" zimenikumbusha mbali sana.

Wee acha tu aisee. Tumetoka mbali sana. Resources za kutosha kama walizonazo hawa madogo wa siku hizi sisi hatukuwa nazo lakini comparatively nadhani kiufahamu tulikuwa juu zaidi.

Nchi, miji mikuu, na majina ya marais nilikuwa nayajua hadi najishangaa. Hata uniamshe usiku wa manane uniulize Asuncion na Tirana ni miji mikuu ya wapi nitakwambia bila wasiwasi kabisa.

Siku hizi siyo kama zamani.
 
TANZANIA NI MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZIMBABWE halafu unajidai kwamba kuna wasomi?

Nani atamfunga kengele mwenzake?

Nani anajidai kwamba kuna wasomi? Define wasomi, maana hata watoto wanaosoma chekechea wanaweza kusema wanajifunza alphabet kwa usomi.
 
Kuna ka ukweli lakini.
ukweli wenyewe ni kwamba Watanzania walioko nje wako kivyao serikali ya Tanzania hata haijui.
Hizi Data kwamba Watanzania hawauziki si zakweli na sielewi watu wanazitoa wapi.
Binafsi nawajua waTanzania zaidi ya 100 wenye PhD wanao fanya kazi hapa USA tu.

Achilia mbali vijana waliopata divion 4 form six wakazamia hapa ambao sasa wana Masters za Computer science engineering accounting na finance!!!
Hawa wote serikali ya Tanzania bado inawaona ni form six failures.

Serikali yetu ni adui namba moja wa wasomi wake na pengine hiki ndo kisa hasa cha kuwa na viongozi wengi wenye PhD feki katika idara nyeti za serikali ikiwa hata Uwaziri Tanzania.

Akina David Mathayo huyu dogo ni Daktari wa kuchoma mbwa na ng'ombe sindano lakini ndo hivyo ni Dr wa PhD.

Nchimbi, alisoma Diplama pale Mzumbe kwa taabu sana Masters alisoma kwa Remote na PhD hakusoma kabisaaa, lakini ndo hivyo serikali imewakumbatia kama wasomi

Wako wengi sana, wanalindana kama mbwa mwitu wakiwa na baraka za serikali ya CCM

Hata hivyo ni kweli kwamba elimu yetu ni ya kukariri ili ufauru mtihani.

Tunahtakiwa kuandika mtaala wa elimu ya kuwezesha wahitimu kuitumia katika kutatua maisha ya kila siku.

Naunga mkono hoja!!!!!
 
Wee acha tu aisee. Tumetoka mbali sana. Resources za kutosha kama walizonazo hawa madogo wa siku hizi sisi hatukuwa nazo lakini comparatively nadhani kiufahamu tulikuwa juu zaidi.

Nchi, miji mikuu, na majina ya marais nilikuwa nayajua hadi najishangaa. Hata uniamshe usiku wa manane uniulize Asuncion na Tirana ni miji mikuu ya wapi nitakwambia bila wasiwasi kabisa.

Siku hizi siyo kama zamani.

Kuna mpaka mnemonics za kukumbuka majina ya marais.

"Nyerere Kaunda Banda Azikiwe Amin". Granted Azikiwe was out of date.

Kuna kipindi Wanaijeria na Waganda walikuwa wanapinduana sana marais, basi nachukia kwa sababu rais akipinduliwa inabidi urudi kwenye kidaftari kufuta jina kuandika jina la rais mpya, mara Shehu Shagari, Mara Muhammad Buhari, mara Lule mara Binaisa, mara Obote karudishwa, mara Okello kampindua, mara Museveni.

Nikawa nalaani mapinduzi ya kijeshi kabla ya OAU kwa sababu yananichafulia daftari langu la marais wa Afrika!

Sasa hivi kuna ma graduate wa Chuo Kikuu Ukiwaambia wataje marais wa Msumbiji tangu uhuru mpaka sasa haawawezi!
 
Kwa kiasi kikubwa ni kweli. Nionavyo, idadi kubwa ya wanafunzi vyuoni ni moja miongoni mwa sababu zinazochangia lecturers wengi kutotumia mfumo mzuri wa kupima uelewa wa wanafunzi: lecturers hivi sasa wanachojua wao ni kuandaa CATs na mitihani ya mwisho basi, na hata watoapo assignments, huwa siyo serious na hakuna presentations za maana ili ku-defend assignments hizo. Tuwapo masomoni, jitihada binafsi ni muhimu sana ili kujiepusha na udhaifu siku za usoni.
 
Me naona hapa hata hamjamuelewa mleta mada ila nina imani alimanisha wasomi wetu ambao ni product ya mfumo wetu huu wa elimu wa tanzania.

Sasa tunaanza kuchambua watz sijui yuko nchi gani na wapi ila hebu tupeni background zao utakuta kasoma shule au chuo mbele huko huko... wewe niambie mtu typicall product of our education system anayefanya vizuri mbele kama si wabeba mabokis na ni wazi watz ni wachache wanaotoka nje ya nchi ukilinganisha na jirani zetu kenya na uganda.

Pia sis wenyew tunalalamika kila siku kuhusu wakenya na waganda wanachukua kazi zetu hapa nchini na pia wenzetu wakenya wamesambaa hata mpaka arabic world..tatizo letu kubwa ni mfumo wa elimu, lugha ya kufundishia,vitendea kazi na sifa hata za walimu wetu toka juu mpaka chini, alafu hatupendi kukosolewa.

Tukubali ya kwamba mfumo wetu ni tatizo toka primary mpaka chuo kikuu...tunadhalisha wasomi hewa wanajua kukariri tu na ndiyo maana wengi wetu wanasiasa maneno mengi kweli ila vitendo hafifu. angalia wachumi wetu wa first class kina Mwigulu ndo alikuwa BOT unadhani hapo kweli kuna kitu???? Prof.Lipumba anaongea ila alishakuwa mshauri wa mwinyi uchumi ila uliona madudu hakuwa na la maana ila hapo unaona bora ambao waliishia la nane kina Lyatonga Mrema wamefanya makubwa kwa taifa hili.
 
Allow pause for an important Socratic moment.

Msomi ni nani?

Criteria inayomtofautisha msomi na mtu asiye msomi ni ipi? Hili ni muhimu ili tujue kwanza pa kuanza kuangalia.
 
Allow pause for an important Socratic moment.

Msomi ni nani?

Criteria inayomtofautisha msomi na mtu asiye msomi ni ipi? Hili ni muhimu ili tujue kwanza pa kuanza kuangalia.

Kwa dhana ya mtoa mada hapa ni vyeti....
 
Jambo moja kubwa na mhimu sana ambalo hulijui kuhusu bongo, ni kwamba amani na utulivu, uzalendo na maisha yenye unafuu kidogo kwa bongo ndicho kinachowafanya wabongo wengi watamani kufanya kazi ndani ya nchi na hata kubaki nchini kwao.

Tofauti na hizo nchi nyingine unazozifia kama vile Kenya, Nigeria, Ethiopia, na nyinginezo nyingi ambazo zina matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, kiasi cha kwamba watu wengi mara tu baada ya kuhitimu masomo yao hukimbilia nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta kazi zenye unafuu. Lakini kwa ninavyoelewa kuna wabongo wengi sana wazuri sana academically na wenye uwezo mkubwa sana, waliogundua vitu vingi na vikubwa mno.

Tunazo Mbilinyi's principles of Economy ambazo ziligunduliwa na Professor mbilinyi, tuna Mpemba Effect ya kwenye Physics ambayo hivi sasa inatumiwa viwandani na kwenye sayansi za mambo ya maji, tuna biological research nyingi sana zinafanywa na watu wa botany pale UDSM na SUA zenye results ambazo hazijawahi kuwepo pengine popote duniani. Sasa utaonekana ni kituko unaposema Tanzania watu wamefundishwa kukariri.

Kwa taarifa yako elimu ya Tanzania ni mojawapo ya classic education katika Africa. Na hivi sasa elimu yetu tunaiuza sana tu. Maana katika universities zetu sasa hivi tunapokea wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali duniani yakiwemo; Zambia, Botswana, Zimbabwe, Uganda, Kenya na hata Africa kusini.

Tuna changamoto kubwa tu ya mazingira na hasa accomodation kwa foreign students. Otherwise, naweza kusema we are the best. Suala la watanzania wangapi wapo nje kikazi hicho si kipimo cha uwezo wetu na elimu yetu. Maana uzalendo kwa nchi yetu ndiyo hasa sababu kubwa ya sisi kutokuwa nje ya nchi.
 
Kwa dhana ya mtoa mada hapa ni vyeti....

Vya kindergarten, darasa la saba, form four, six, chuo etc?

Na kama vyeti vinaweza kununuliwa kama alivyofanya Mkullo, vyeti kweli ni usomi?
 
Vya kindergarten, darasa la saba, form four, six, chuo etc?

Na kama vyeti vinaweza kununuliwa kama alivyofanya Mkullo, vyeti kweli ni usomi?

hapo anaongelea mfumo wa elimu, ya kwamba hautoi watu competent ambao wanaweza kushindana na jirani zetu kwenye soko la ajira nje hasa ulaya na USA nadhani ukilinganisha na nchi jirani kama kenya na uganda.
 
Back
Top Bottom