Ukweli mchungu: Adui wa taifa sio Ujinga, umasikini na maradhi, bali ni ni lishe

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,596
15,393
Aliyebuni kula liugali kubwa na kamboga kadoko au wali lumbesa na tumaharage kidogo ndio katufikisha hapa.

Tunakula ili tujaze tumbo sio kushibisha seli hai kwa virutubisho jengefu. Watu wengi tunashiba tumboni lakini seli za ubongo na za maamuzi ya msingi zinalala njaa kila siku. Matokeo yake ni ujinga, maradhi na umasikini.

Ukifanya mapinduzi ya lishe, utakuwa umefanya mapinduzi ya familia na taifa litakuwa lenye akili zenye akili.

Ni hayo tu.
 
Uzi makini sana huu... lishe ni tatizo kubwa. Kwa mfano watu wa Dar hasa maeneo ya uswahilini wana lishe duni mno. Familia nyingi hazimudu kula hata mara 2 kwa siku.

Vidonda vya tumbo ni sehemu ya maisha ya wengi. Na hata hicho kinacholiwa ndo huo ugali na dagaa mchele. Hili tatizo ni kubwa mno.
 
Mbona unarudi kwenye pointi kuwa maadui wa taifa ni ujinga, umasikini na maradhi. Lishe mbovu inatokana na ujinga, umasikini na maradhi. Elimu ya lishe inatakiwa itolewe. Watu wamezoa kula ugali mwingi na wali mwingi mboga kidogo tena bila matunda. Wapi uliona mboga zinaliwa zenyewe tu bila ugali au wali? Elimu ya lishe ni sifuri, hata kwenye masherehe watu wanataka washindilie pilau ndio washibe. Uwapikie watu shatashata, matunda kwa wingi, mbogamboga hawatakuelewa
 
Zaidi ya kutaka katiba mpya ili kuwe na serikali tatu hakuna kitu kingine cha maana mnachoongeaga. Nyie ni wabaya kuliko CCM.
7a076a44c9085d5d6c7a27adba77e1c6.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom