Ujinga, maradhi na umasikini: Hivi vitu vitatu kwetu bado ni mzigo mzito!

Deghe Mangae

Senior Member
Mar 3, 2020
171
149
Hivi vitu vitatu kwetu bado ni mzigo mzito, Watanzania bado maadui hawa watatu.

Bado wapo hainiingii kichwani tunaposema wasomi tunao lakini wanayofanya ni matatizo mtupu kila iitwapo leo hii shida msomi mzima unafanya mauzauza kwa nini nisiseme. Huyu adui yupo ambaye ndo mbaya zaidi. Kwa ukosefu wa ELIMU ama uwelewa wetu hupelekea tushindwe kupambana na adui namba mbili MARADHI.

Maradhi mengi Tanzania husababishwa na uwelewa mdogo (Elimu) kila kitu MUNGU Katupa lakini ni namna gani ya kuvitumia hapo shida ndo huanzia Nikupe mfano mmoja angali ule msongamano ndani ya mwendokasi kwa staili ile kama yupo mgonjwa wa TB ya mapafu kwa nn asiambukize Wengine?

Akishaambukiza nini kinafuata? Ni zile foleni tena za kujaa kwenye vituo vya kutolea huduma atashinda huko mwisho wa siku hulazwa au akatumie dawa nyumbani unadhani Mtu huyu atakuwa na nguvu tena za kufanya kazi? Nini kifuatacho.

Ni adui namba tatu UMASIKINI Adui huyu atatupelekesha vibaya mno mpaka tunaishiwa huku akishirikiana wenzake na kututumbuki kwenye mikasa Mizito kwelikweli na kubaki ombaomba kila iitwapo leo .kwa staili hii Naomba Nirudi kwenye adui UJINGA Kila mmoja wetu Adui huyu ujinga amepambana Naye vipi kupitia kaelimu kake ndani ya Jamii ya Kitanzani amefanya nn cha maana kwa maslahi mapana ya watanzania wote?

Kama jibu ni Hapana basi AKILI HUNA na kaelimu kako ni bure na hako kasuti kako no ujue Ipo tofauti kubwa kati ya ELIMU NA AKILI ndo maana leo wasomi wengi AKILI HAWANA wamebaki na vyeti tu kwenye mikoba yao na ndiyo hawa wasumbufu ktk Nchi hii ya ahadi iliyojaa Mito ya MAZIWA NA ASALI Watu weupe ktk Nchi mbalimbali Duniani wanaitamani Sana TANZANIA leo hii wameshaona hii mito ya maziwa na asali ambayo tunashindwa kuitumia mwisho wa siku tunabaki kulaumiana kufuatia UTUMWA WA FIKRA.
 
Back
Top Bottom