Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 13,634
- 21,238
Utafiti wa mafuta umeanza siku nyingi na hakuna takwimu rasmi za kuonyesha kuwa mafuta yamepatikana! Hii ni hisia tu na kukuza jambo bila sababu! Kwa sasa tunachohitaji ni mpaka kamili katika ziwa hilo!Mazungumzo hayo yalikua ni hatua zilizofikiwa kabla ya kwenda kwenye mahakama ya kimataifa.... kumbuka kinachogombewa siyo Ziwa Nyassa kama lilivyo inasadikika kuna mafuta ya kutosha ambapo utafiti unafanywa na Kampuni la Uingereza lenye mkataba na Malawi....! Hivyo Malawi wanasaidiwa na UK kulisukuma hili mahakama ya Kimataifa....!
My take;
Kwakuwa imekua ni mazoea kwa serikali ya sasa kujihusisha na watu wenye uwezo mdogo katika kila fani.... Rais Joyce Banda ameuona udhaifu wa timu yetu ya usuluhishi..... nawaambieni watu walioenda kutuwakilisha si ajabu kubwa walilonalo ni kutafuna posho za vikao
Hapa km taifa kulitakiwa watu kama Tindu Lissu ...! aiongoze timu ya majadiliano na hata km tunaenda kwenye mahakama ya kimataifa basi tuwe na watu wenye uwezo sio kina Jaji Werema ambao kazi yake kubwa ni kutafuta kamusi ya Kiswahili ili atuambie tusi ninini .., hana weledi wa taaluma km tulivyomtarajia.
Endapo mafuta au gesi vitapatikana bila shaka tutakuwa na mgawo wetu!