Ndugu zangu wakubwa kwa wadogo ifike wakati tuwe na moyo wa utu,ubinadamu,huruma na upendo..Wanadamu tumekuwa wepesi sana wa kuhukumu wengine kwa namna hata ya kutamani wafe kwa kuungua moto ,kulipuliwa,kulipiliwa au kujinyonga.Tukumbuke kila mmoja wetu ana uozo aliutenda,unena,ufikiri {waza} ,aliouona {akaushangilia,akafaidika nao,akafumbia macho,akaulea,akauchekelea}.Nikiuliza nani msafi baina yetu?Nani asie na doa?Nani angejizuia kwa 100% kutenda waliotenda watuhumiwa wa ufisadi wa mali za umma/madaraka/uongozi?
Ina maana vyombo vya usimamizi wa maadiri ya watendaji waandamizi na viongozi havijui hizi tuhuma lukuki zinazoelekezwa kwa hawa watuhumiwa waandamizi wa uhujumu nchi {kijamii,kisiasa,kiuchumi}? Tunafanyaje kuviwajibisha vyombo husika na watendaji wake?
Inawezekanaje kandarasi kubwa zikatolewa kwa misingi ya udini pale NSSF {Mfano:Inawezekana kweli Kandarasi nyingi za umeme kwenye majengo mengi zilizotolewa kwa Kampuni ya DERM Electric zilitolewa kwa upendeleo wa Ubora/Unafuu/kufahamiana/undugu/udini {Zipo taarifa ya kwamba meneja miradi ni shemeji mtu na mmiriki wa kampuni husika?{ Conflict of Interests zilikuwa declared}.
Japo itakuwa ni majungu kuanza kupiga kelele kwamba mmiriki wa kampuni ya Derm electric ambayo imekuwa ikifanya kazi nyingi nyeti za ukandarasi wa umeme ni jipu kwa sababu anamiriki vitega uchumi lukuki vya majengo ya thamani kubwa kwa kipindi kifupi au amenunua nyumba nyingi makumbusho na Kijitonyama..Yampasa kila anaetoa tuhuma atoe ushahidi usio na shaka kuhusisha moja kwa moja ufisadi ktk taasisi ya umma husika au watendaji wake na mtuhumiwa elekezi.mfano kama upo ukweli kuwa uwekezaji husika unafanywa na watuhumiwa wakuu kupitia wafaidika wa nje.
Binafsi si muumini wa majungu kabisa kabisa hivyo natamani wote tufikiri kwa sauti ya juu na umakini kwa kujiuliza maswali ambayo majibu yake yawe na majibu yasio na majungu,fitna,husuda,chuki,kijicho,gere...Kwa nini leo niamini ya kuwa Kampuni ya wataalamu wabobezi ktk usanifu majengo ya Hab Consult ilikuwa ikipewa kandarasi lukuki kwa kupendelewa sababu ya udini/urafiki/ujamaa/Ubora/Unafuu/Umahiri? wa mtuhumiwa na wahusika? Ama CRJE {wachina }walipewa kandarasi walizopewa kwa udini/Upendeleo/Rushwa/Uwezo thabiti/Bei nafuu/Ubora?
Inapaswa shutuma au tuhuma zithibitishwe pasipo shaka yeyote ikiwa kuna nia haswa ya kumtia hatiani mtuhumiwa kijamii,kisiasa ama kiutendaji..Mfano tunaposema aliajiri ndugu,jamaa,marafiki kwa upendeleo wa udini,ukanda,ukabila,ujirani,n.k n.k ni vema tukataja kwa vielelezo {sifa zao,vigezo vyao,mapungufu yao} na majina kwa uwazi pasipo woga.Mfano:Kidula,Matessa,kagomba,Magori,Mrisho, Chaulembo,Shariany,Madjapa,Mrosso n.k n.k
Lakini tena tujiulize inakuaje tuhuma hizi zijitokeze sasa?Inawezekanaje kwa kipindi chote cha utendaji mbovu tuhumiwa taasisi za udhibiti /usalama/uchunguzi/uzuiaji matumizi mabaya ya madaraka zikawa na ulemavu {naomba radhi kwa matumizi ya neno hili} wa kushindwa kusikia,kuona,kuhisi na kufikia uozo husika na kuchukua hatua?
Angalizo:viongozi na watendaji wakuu mliopewa dhamana ya madaraka na wawakirishi/wateuliwa wa wananchi jitahidini sana kutenda kazi kwa haki,kweli,kufuata matakwa ya sheria,matakwa ya utaratibu,uwazi,uwezo,uadirifu na uzalendo uliotukuka ili hata mkija kuhukumiwa kwa uonevu Mwenyezi Mungu alie hakimu na jaji mwenye haki pekee awatetee na kuwapigania kuwa mnaonewa na kukandamizwa hata kwa kuwatumia malaika zake.