Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Dereva aliyeuawa azikwa Dar

Na Muhibu Said

MAZISHI ya dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), anayedaiwa kuuawa kwa risasi na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwano Ditopile Mzuzuri, jana yalitawaliwa na simanzi na vurugu zilizosababisha askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujeruhiwa usoni kwa jiwe.

Askari huyo ambaye hakuweza kufahamika mara moja, alikumbwa na mkasa huo baada ya vijana wenye hasira waliokuwa katika barabara ya Kawe wakikusanya michango ya mazishi ya marehemu, kulishambulia kwa mawe na viatu gari la jeshi aina ya Range Rover alilokuwa amepanda askari huyo na mwenzake.

Vijana hao, wakiwamo madereva na makondakta wa daladala, walilishambulia gari hilo baada ya askari huyo na mwenzake, kutaka kumkamata dereva wa daladala aliyedaiwa kutaka kusababisha ajali katika barabara hiyo.

Tukio hilo lilitokea saa 7.30 mchana katika eneo la Kawe Mzimuni, karibu na nyumbani kwa marehemu na kusababisha tafrani iliyodumu kwa takriban dakika tano.

Baada ya kulituhumu kutaka kusababisha ajali hiyo, askari hao kwa kutumia gari lao, walilifukuza daladala hilo na walipofika katika eneo hilo, walilitangulia kwa mbele na kulizuia.

Kitendo hicho, kilionekana kuwachukiza vijana hao ambao waliamua kulizingira gari hilo na kulishambulia kwa ngumi, mawe na viatu.

Kutokana na kuelemewa na vurugu hiyo, dereva wa gari hilo la jeshi aliliondoa gari hilo kwa kasi katika eneo hilo na askari aliyejeruhiwa, alivua kofia yake na kuitumia kama kitambaa kufuta damu zilizokuwa zikichirizika usoni.

Mbali na tukio hilo, wakati mwili wa marehemu ukifanyiwa ibada katika Msikiti wa Shamsia, Kawe, vijana hao walifunga barabara na kuanza kukimbia mchakamchaka huku wakiimba nyimbo wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kuikejeli serikiali.

Vijana hao ambao waligawanyika katika makundi mawili, moja likikusanya michango ya mazishi kutoka kwa madereva wa magari yaliyokuwa yakipita katika njia hiyo na lingine likiimba.

Hali hiyo iliwafanya askari polisi waliobeba silaha kufanya kazi ya ziada kuwadhibiti vijana hao wasilete vurugu katika mazishi hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Maringo.

Zaidi ya Sh300,000, zikiwamo Sh100,000 zilizotolewa na Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, zilitangazwa kukusanywa katika mazishi hayo.

Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani saa 8.30 katika gari la polisi aina ya Land Rover Defender na kuagwa na ndugu, jamaa, marafiki na majirani kabla ya kupelekwa katika msikiti huo kwa ajili ya sala.

Mbali na Mrema, viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo, ni Naibu Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mtoro, Sheikh Khalifa Khamisi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva na Makondakta Mkoa wa Dar es Salaam (Uwamadar), Shukuru Mlawa na Kamanda wa Polis Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow.

Kamanda Rwambow aliwataka ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa watulivu katika kipindi cha msiba na kuwaahidi kuwa polisi inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha haki inapatikana.

"Watu wasivuruge azma hiyo, mshitakiwa kishafikishwa mahakamani na amepelekwa gerezani. Kiutaratibu hatutakiwi kuzungumzia kitu kilichopo mahakamani, kitatuharibia kupata haki yetu, kwa mfano hayo mabango hayatusaidii kitu, naomba tuviamini vyombo vya serikali," alisema Rwambow.
 
Mkuu wa mkoa Ditopile ashtakiwa kwa mauaji

Na Tausi Ally

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Kapteni Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (58), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la mauaji ya dereva wa daladala, Hassan Mbonde.

Pamoja na mamia ya watu kufurika mahakamani, eneo la mahakama lilijaa ukimya wakati mkuu huyo wa mkoa akipandishwa kizimbani.

Ditopile anayekabiliwa na shtaka la mauaji kwa kutumia bastola, alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa 3.09 asubuhi, akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi waliojaa kwenye magari mawili ya polisi aina ya Land Rover Defender.

Saa 3:54 asubuhi, Ditopile aliingizwa mahakama ya wazi, huku akiwa amevalia suruali yenye rangi ya kaki na shati la rangi mchanganyiko, miwani na mkononi wake wa kushoto ukiwa umefungwa bandeji.

Baada ya dakika mbili, Hakimu Michael Luguru, aliingia mahakamani na Mwendesha Mashtaka, Mrakibu wa Polisi, Germanusi Muhume, alimsomea Kapteni Ditopile shtaka la mauaji linalomkabili. Wengine waliokuwepo ni Mrakibu wa Polisi Naima Mwanga na Inspekta Raphael Rutaihwa.

Muhume alidai kuwa, Novemba 4, 2006 majira ya saa 1:00 usiku katika eneo la njia panda ya Bagamoyo na Kawe wilayani Kinondoni, Ditopile alimuua Hassan Mbonde.

Baada ya kusoma mashtaka, Muhume alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na akaiomba mahakama ipange siku nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Mtuhumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kisheria kusikiliza shtaka linalomkabili. Mahakama Kuu ndio yenye uwezo wa kusikiliza mashtaka ya mauaji.

Kabla Hakimu Luguru, hajaaihirisha kesi hiyo hadi Novemba 20, mwaka huu, mawakili wanaomtetea mtuhumiwa, Dk Ringo Tenga, Losan Mbwambo, Cuthbert Tenga na Samwel Mapande, walidai kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa aliumizwa mkono, hali iliyosababisha polisi kumpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyiwa matibabu.

Mawakili hapo hao waliiomba mahakama imruhusu mteja wao aonane tena na daktari wake ili kumpima afya yake.

Dk Ringo, aliomba mahakama imruhusu mtuhumiwa huyo afikishwe hospitali kwa kuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu na pamoja na kisukari na kwamba, juzi shinikizo lilipanda hadi kufikia 180.

Wakili huyo alidai kuwa mteja wake pia ameshtushwa na gazeti moja lililoripoti kuwa, 'Ditopile Kunyongwa' akidai kwamba limemhukumu na kuongeza kuwa linaweza kumpeleka pabaya mtuhumiwa, hoja ambayo iliungwa mkono na upande wa mashtaka.

Baada ya Hakimu Luguru kuahirisha kesi hiyo majira ya saa 4:07, Ditopile aliingizwa kwenye gari ndogo ya saluni yenye vioo vya giza na kuondoka eneo la mahakama.
 
Kama kuna mtu anaweza kumtumia ujumbe JK.. please do:


a. Atangaze mara moja kumvua Ukuu wa Mkoa Ditopile
b. Bunge la JM ambalo liko kwenye kikao litangaze kumsimamisha Ubunge (if he is still a MP)

Na kusiwe na mawasiliano yoyote kati ya JK na Dito unless itangazwe hadharani..!!
Kusiwe na mazungumzo yoyote kati ya JK na Mkuu wa Polisi au watu walio chini yake unless itangazwe hadharani
 
Jasusi
Ni kweli sisi tuna haki ya kujadili; na hata kupendekeza aina ya adhabu tunayoona sisi inafaa(has no effect any way). Hofu yangu kubwa hapa ni kwamba huyu jamaa ni mshikaji wa JK. Kwa hivi kunaweza kuwa na lenience katika utoaji hukumu. Poleni wafiwa.
 
Ninanukuu gazeti la mwananchi "Baada ya Hakimu Luguru kuahirisha kesi hiyo majira ya saa 4:07, Ditopile aliingizwa kwenye gari ndogo ya saluni yenye vioo vya giza na kuondoka eneo la mahakama".Kifungu hiki kinanikumbusha kesi ya Kinjekitile yeye alikua anapelekwa Keko na Toyota VX mda si mrefu akaonekana hana hatia. Na hali iyo inajirudia tena kwa kesi ya DITO Sasa waungwana kwa mendo huu haki itatendeka kweli?Nionavyo hapa hakuna kesi,Ditopile ataendelea kupeta mitaani kama kawaida.
 
Mzee Zanaki,

You got it right, kwa wale wanaosema eti tusubiri mahakama ndio tujadili please acheni mchezo, can you imagine dereva wa basi angempiga risasi Ditopile?

Kwa nini tusijadili wakati wezi wa kuku wanapanda ngarandinga, muuaji wa binadamu asiyekuwa na hatiua anapanda saloon? Wewe umeshawahi kufika pale mahakamani halafu unieleze mshitakiwa anayekaa rumande anavyoweza kuondoka na Salooon? Hiyo Saloon ni ya nani? Na inampeleka wapi? Why Saloon na kina Ngaiza walikuwa wanapanda ngarandinga? Huyu Ditopile ni nani mpaka apande Saloon? At this point ni muuaji kama vile wezi wa kuku na mbuzi, anastahili kuwa kwenye ngarandinga bro!

Ndio maana inabidi tujadili maana wakubwa wapo hapa, sasa tusipojadili huyu kesho atakuja mahakamani na benzi ya serikali, je atafungwa na hakimu gani? Hebu vijan muache mambo yenu ya Ulaya, yule dereva ni binadamu mwenye mke na watoto, na mlipa kodi pia, na Mumgu anamjua kwa jina na namba za nywele zake, No! ni lazima tuwashe moto hapa kila siku na tukumbushie kila siku mpaka siku ya hukumu, sisi tusiposema yule marehemu dereva wa basi atasemewa na nani? Wewe tayari Tibaigana ameshaanza kumsemea Ditopile kuwa ameua kwa kutokukusudia, lakini hajmtaja kabisa marehemu,

We are going to stand for marehemu dereva wa basi, na wewe unayesema kuwa madereva wa mabasi wana-deserve kupigwa risasi, are you out of your mind? Ni nchi gani duniani huwa wanafanya hivyo? Wazee mnaokaa NY au Italy hebu tuambieni jinsi madereva wa huko walivyo na balaa, lakini je kuna sheria ya kuwapiga risasi? Wakati viongozi wanaiba nchi, unataka madereva wa mabasi wafanye nini, ni lazima wachomeke kuwahi abiria kama viongozi wanavyowahi kununua magenerator mabovu na yasiyokuwepo ya Richmond, jamani kuna maisha ya binadamu yaliyopotea hapa watu wawe careful!

Please!
 
Huu ndio wasiwasi wangu kuwa sheria inaweza kupindishwa halafu jamaa akaachiwa huru kama kwamba huyo kijana aliyeuwawa hakustahili kuishi. Kuna watu wengi wamewahi kuachiwa kienyeji tu, kwa mfano wale wazungu waliomuua changudoa Modesta walivyochiwa hurur bila maelezo yoyote kama kwamba huyo Modesta alikuwa si binadamu.

Huyu Bwana anatuhumiwa kuua mtu, ni lazima ashughulikiwe kama watuhumiwa wengine na sheria ichukue mkondo wake kama kawaida. Alale sakafuni, ale ugali kwa maharage na kujisaidia kwenye ndoo kama watuhumiwa wengine wanavyofanya wakiwa huko Keko. Asipewe upendeleo wowote. Kwa sasa hivi anapandishwa kwenye saloon yenye EA KONDISHENA na TINT wakati watuhumiwa wengine wakichukuliwa na karandinga, maana yake nini. Je kweli haki itatendeka?
 
Serikali ya Awamu ya nne imefanya kosa kubwa sana huyu bwana immediately baada ya kufunguliwa hayo mashitaka alitakiwa afukuzwe kazi na Rais mara moja ! Sijui wana subiri nini , kuna mtu anayeweza kuniambia mkuu wa mkoa wa Tabora ni nani ? Kisheria bado ni Ditopile mpaka hapo atakapofukuzwa au kujiuzulu . Sasa tutakuwaje na mkuu wa mkoa ambaye anatuhumiwa katika kesi ya mauaji. Wanabodi ni nani anayemshauri Rais ?

Na hawa wapinzani wako wapi ? siasa ni mchezo mchafu kwa hiyo ni lazima watumie hizi loop holes zinazojitokeza ...walitakiwa waunganishe special treatment huyu mtuhumiwa anayopewa , kuchelewa kwa Rais kumfukuza kazi katika kujijenga kisiasa ..... walitakiwa waitumie hii issue kuonyesha ni kwa jinsi hakuna tofauti kati ya kasi mpya na serikali nyingine za CCM zilizopita.
 
Mzee JJ, na Mwanasiasa,

Vipi wazee? Huyu Ditopile bado kisheria ni Mkuu wa mkoa pamoja na kwamba ameua toka juzi, mko wapi?

Waandishi wa habari acheni kutuwekea nyani usoni, mtoto wa Rupia na Kingunge walipokuwa na kesi enzi zile mlikuwa nmnatufahamisha mpaka namba ya gari walilopanda, waliokuwemo ndani ya gari, magari yaliyowafuata, yalikotokea, na yalikokwenda, na yalikoishia,

sasa leo vipi mbona mnaanza kuwa mabubu? Hili gari alilopanda Ditopile lilikuja mahakamani likitokea wapi? Nani alikuwa dereva, Je ndani ya hilo gari kulikuwa na askari wa kumlinda mshitakiwa wa mauaji, Ditopile Mzuzuri? Alipofika mahakamni je alikaa kwenye selo ya pale mahakamni na washitakiwa wengine? Je alikuwa na pingu wakati wote kama sheria inavyotaka? Je baada ya kesi gari alilopanda lilimpeleka wapi? Je kwenye ngarandinga ya washitakiwa inayowarudisha keko na segerea, hakukuwa na washitakiwa wengine wa mauaji kama Ditopile Mzuzuri? Kwa nini nawao hawakuletwa na Saloon? Magereza toka lini wameanza kusafirisha wauaji na Saloon?

Mbona mnaanza kuwa mabubu mapema? Na viognozi wetu wa nchi mbona kimyaaa? Kulikoni?

Jamani tuibieni tani yenu, IPTL, Richmond, sawa, lakini msianze kutuuuuua!
 
Kweli nimeamini kuwa maajabu yote yanawezekana Tanzania.Hivi kuna mantiki gani kwa Dito kuondoka mahakamani na usafiri mwingine badala ya ule ulio mahsusi ie karandinga?Kama wameshaanza kumpatia special treatments katika hatua hii basi sintoshangaa hii kesi ikiisha kinyemela.

Ila kwa hakika huu ni mtihani mkubwa sana kwa JK.Najua atakuwa ameshafahamishwa kuwa mshkaji wake "kaharibu" huko nyumbani lakini JK anatumia kisingizio cha kuwa nje ya nchi kutotoa uamuzi unaopaswa kufanywa haraka:kumvua Dito ukuu wa Mkoa hadi kesi itapokwisha.

Mimi naona probabilites kuu mbili kuhusiana na kesi hii:
1. JK kutambua kuwa huu ni mtihani mkubwa kwa uongozi wake,na hivyo kuchukua maamuzi ya kiuongozi badala ya kiushkaji.Na kikubwa anachoweza kufanya katika hili ni kutoingilia uhuru wa mahakama kwa kumlinda mshkaji wake,na pia kumvua madaraka huyo jamaa ili kesi yake iendeshwe kama dhidi ya Dito na sio dhidi ya Mkuu wa Mko wa Tabora.Pia kwa kufanya hivyo,atawatendea haki wakazi wa Tabora ya kutonyimwa kiongozi mkuu wa mkoa kwa uhuni wa mpuuzi mmoja.JK akipanga karata vizuri,hili litamwongezea umaarufu zaidi ya sakata la Zombe na wale wauza madini.Na pengine linaweza kuwasahaulisha watu mauzauza ya Richmond na madudu mengine

2.Kulindana na more kulindana.Wajuvi wa mambo wanasema Dito yuko damdam na JK pengine zaidi ya Lowassa au Msabaha.Inaweza kuwa yaleyale yalowafanya akina Kinje waue na kuendelea kupeta mitaani hadi leo.Kinachoweza kumpa nguvu JK ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania kuna sheria kwa ajili ya walalahoi na zile kwa ajili ya wenye nazo.Ndio maana unaambiwa kuna wezi na majambazi na wengine wanaitwa wabadhirifu japo kimsingi ni wezi na majambazi pia.Vilevile,mifano ya huko nyuma ambako vigogo au watoto wao walishawahi kuichezea sheria na umaa ukabaki kuongelea chinichini tu inaweza kumpa JK nguvu ya kumkingia kifua mshkaji wake.

Najua wapo "wajuzi" wa sheria watakaosema kuwa JK sio mahakama hivyo hawezi ku-influence kesi hiyo.Wako wrong.Afrika,Rais ni sawa na Mungu (na pengine zaidi) na akiamua kitu hakuna wa kukibadilisha japo mahakama zipo.Kwa mtizamo wangu,kesi hii sio tu mtihani mkubwa kwa JK bali pia kipimo cha upendo wake kwa wale wasio na kitu ambao pamoja na blunders kadhaa zinazoendelea bado wanaamini kuwa JK anaweza kuleta "maisha bora kwa kila Mtanzania"
 
Mkishangaa ya Mussa mtaona ya firauni..... Kama mlishangaa ya Mwalimu JKN(mnavyodai kupendelea wakristo) sasa shangaeni ya JK....
 
Kitendo cha Rais Kikwete kuacha masaa zaidi ya 72 kupita bila kuchukua hatua yoyote ya kiutawala dhidi ya Kapt. Ditopile Mzuzuri ambaye ni mkuu wa mkoa wa Tabora anayetuhumiwa kumuua kijana Hassan Mbonde kinashangaza na kwa kweli kinatia shaka.

Hadi tunakwenda mtamboni Bw. Ditopile Mzuzuri alikuwa anatambulika kama Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Mkuu wa Mkoa fulani ni kiongozi anayemwakilisha Rais katika mkoa huo na anawajibika kwake tu na si kwa mtu mwingine wala chombo kingine. Ni kwa ridhaa ya Rais mkuu wa mkoa anafanya kazi yake na ni kwa uamuzi wa Rais anaweza kuondoka katika nafasi hiyo. Kwa sababu hiyo, Ukuu wa Mkoa siyo nafasi ya kisiasa kama Ubunge bali ni nafasi ya utawala ambao mara nyingi hutolewa kama fadhila na shukurani kwa marafiki na watu wa karibu.

Bw. Mzuzuri amekuwa ni kiongozi ambaye amekuwa karibu na viongozi wengi tangu huko nyuma kutokana na shughuli zake kama mwanasiasa na kada wa chama. Hivyo nafasi nyingi ambazo amezipata katika utumishi wa nchi yetu zimetokana na uhusiano alionao na ukaribu alionao na viongozi wa juu wa chama na serikali.

Ni kutokana na ukweli huu, ndio maana wananchi wengi wanafuatilia kwa ukaribu tuhuma hizi nzito ambazo zimetolewa dhidi yake. Na ni kwa sababu hiyo basi tunataka tuone haki inatendeka. Haki tunayoizungumzia hapa siyo ya kulipia kisasi cha Hassan Mbonde tu bali haki ya Bw. Ditopile kuendeshewa mashtaka pasipo kuonewa, husuda, au upendeleo wa aina yoyote.

Haki lazima itendeke. Siyo tu itendeke bali pia ionekane inatendeka! Hapa ndipo njia panda ya Kikwete ipo. Kwa maoni yangu, hakuna ugumu wowote ule kwa Mhe. Kikwete kumvua madaraka Bw. Ditopile. Kitendo cha Mkuu wa Mkoa kutuhumiwa kufanya kitendo cha mauaji ni suala zito mno kwani maana yake ni pana mno. Je kama kweli Bw. Dito alifanya mauaji hayo, je alimuua huyo akiwa kama Mkuu wa Mkoa na hivyo kuiweka serikali ya Tanzania kwenye hatari ya kushtakiwa? Je, kuendelea kukaa rumande je anapata upendeleo wa aina yoyote kwa vile yeye ni mkuu wa mkoa? Wakuu wa Mikoa wanapigiwa saluti na polisi (kwa vile wanamuwakilisha Rais) je Bw. Mzuzuri anapokwenda kuonana na Polisi anapata heshima hiyo? Kwa vile bado ni mkuu wa mkoa, je mkoa wa Tabora uko chini ya uongozi wa nani, na je ka Dito ana mawasiliano yoyote na viongozi waliochini yake? Kwa vile Mkuu wa Mkoa anawajibika kwa Rais je tangu tukio litokee Bw. Dito amezungumza na Rais Kikwete?

Ni katika kujibu maswali hayo, ndipo umuhimu wa kumvua cheo hicho unapoonekana. Haiwezekani mtu ambaye yuko karibu na Rais namna hiyo akatuhumiwa kufanya tendo hilo na Rais kuendelea kukaa kimya. Kama Rais anaweza kuwateua watu akiwa safarini nina uhakika anaweza kabisa kumvua mtu madaraka akiwa huko huko Safari.

Kwa mara nyingine tena, uongozi wa Kikwete unatutia shaka. Shaka tulilonalo ni kama kweli Rais Kikwete ana washauri wazuri au ni wale ambao wanaangalia kila jambo kwa mwanga wa siasa, umaarufu, na kujipendelea. Rais alichukua muda kushughulikia suala la Msabaha, na alipolishughulia ilikuwa ni kiini macho. Tunatumaini kuwa suala la Ka' Dito halitaangukia kwenye upande huo!!

Kwa jinsi ilivyo sasa suala hili si zito. Linakuwa zito pale tunapofikiria kuwa aliyetuhumiwa kufanya tendo hili ni Mkuu wa Mkoa. Endapo Rais atamvua madaraka mara moja (kuendelea kuchelewa ni kujitafutia aibu isiyo ya lazima) basi kutafanya upepelezi na shughuli nzima ichukue mkondo ule ule unaochukuliwa kwa watu wengine. Iweje, Dito afikishwe kwa gari tofauti, na kuondoka kwa gari la peke yake wakati watuhumiwa wengine wanatoswa kwenye karandinga? Iweje Ditopile aende kujisalimisha nyumbani kwa Mkuu wa Polisi badala ya kwenda kituo cha polisi? Iweje Mkuu wa Polisi atamke kuwa Dito aliuua bila kukusudia kabla mahakama haijaamua hivyo? Iweje hivi au vile!!!? Ni wazi kuwa Bw. Ditopile anapewa huduma tofauti ambayo watuhumiwa wengine hawapati kwa vile yeye ni Mkuu wa Mkoa!! na rafiki wa karibu wa Rais.

Wito wetu kwa Mhe. Kikwete ni kuwa katika suala la kutafuta haki hakuna udugu, uswahiba, au urafiki wa namna yoyote ile unaotakiwa kuzingatiwa isipokuwa haki, na haki peke yake. Licha ya kitendo hiki kumgusa Rais Kikwete kwa namna fulani, ni lazima ajue kuwa kitendo cha kusita sita kinatufanya tuwe na shaka kuwa kuna jambo linapikwa litakalofanya haki isitendeke au isionekane kutendeka. Tunachotaka siyo Rais Kikwete aamue kama Bw. Mzuzuri ana hatia au la. Bali, asaidie utafutwaji haki kwa kuondoa kiwingu chochote cha upendeleo kinachotokana na ukweli kuwa Mshitakiwa bado ni Mkuu wa Mkoa na bado ana nyadhifa zote alizonazo. Na ili kuondoa kiwingu hicho, Rais Kikwete asijihusishe kwa namna yoyote ile na kesi ya Dito yeye mwenyewe au wajumbe wake. Tunataka kujua pia kama Mkuu wa Polisi alizungumza na kiongozi yeyote wa serikali kabla ya kumweka lupango Dito, na kiongozi huyo ni nani, walizungumza nini, na kwa nini?

Ni pale tu ambao Rais Kikwete atamvua Ditopile nyadhifa zake zote na kumuacha abakie kuwa kama raia mwingine, akijitetea mbele ya mahakama zetu na hatimaye kupatiwa hukumu anayostahili ndipo hati itaonekana imetendeka. Kinyume cha hapo, Watanzania watajuta kuichagua serikali hii kwa kura nyingi, kwani mazingaombwe yatakuwa yamepata nafasi tena. Tunarudia, haki lazima itendeke, na siyo kutendeka tu, bali pia ionekane imetendeka. Mpira uko upande wako mhe. Rais!!!
 
Wajameni,
Tumpe JK muda amalize ziara yake tuone atafanya uamuzi gani. Labda haitakuwa vizuri kutangaza hatua akiwa nje ya nchi. Tumpeni muda. Mzee ES, well said.
 
Jasusi said:
Wajameni,
Tumpe JK muda amalize ziara yake tuone atafanya uamuzi gani. Labda haitakuwa vizuri kutangaza hatua akiwa nje ya nchi. Tumpeni muda. Mzee ES, well said.

Madaraka ya Urais hayashikwi na mtu mmoja, ni taasisi. Popote pale JK alipo, ana-connection na yanayotendeka nyumbani. Kwa tukio kubwa kama hili alitakiwa angalau atoe tamko hata kupitia wasaidizi wake waliobaki Dar es Salaam.
 
Kuna baadhi ya wanabodi wamekuwa wamelalamika ya kuwa Mheshimiwa Ditto aliondoka na salon mara ya kusikiliza kesi yake ! Mimi sidhani kama kuna kosa lolote polisi walilofanya huyu mtu bado ni mkuu wa mkoa kwa hiyo astahili kupanda karandiga regardless alifanya nini !

Mimi narudia maneno aliyosema Mwanakijiji serikali ya awamu ya nne imefanya makosa makubwa sana , aiwezekani tukae masaa 72 bila ya wao kutoa maamuzi. Ukisoma kwenye magazeti inaonyesha kabisa ya kuwa hawajui wafanye nini !
 
Jasusi, don't fall for this! Rais aliweza kuwateua watu akiwa nje ya nchi nina uhakika anauwezo wa kumvua mtu madaraka akiwa bado safari kwani Rais haachi kuwa Rais kwa vile yuko nje ya nchi!! Na zaidi ya yote, hofu yangu ni kuwa kuna mtu anasubiri maelekezo toka juu!! Ndio maana kwenye matangazo yangu nimeuliza, je Dito alipoenda kujisalimisha kwa Mkuu wa Polisi, je mkuu huyo alipiga simu mahali popote kutaka kuzungumza na mtu yeyote kupokea au kutoa maelekezo? Kwanini Dito alienda kujisalimisha nyumbani kwa mkuu wa mkoa badala ya kwenda Polisi moja kwa moja? Je JK alizungumza na mkuu wa Jeshi kabla ya Tibaigana kuzungumza na vyombo vya habari?
 
Mwanakijiji,
Nimekusikia. Nilikuwa nafuata falsafa ya FD--kuangalia upande mwingine wa shilingi.
 
sasa naona kila kitu kinafutwa humu je hamuoni kuwa haki zenu za kikatiba zinachukuliwa?

Je tunarudi enzi za ukomonisti?
 
Latest niliyonayo from a highly placed source huko Bongo ni kwamba Dito offered to resign lakini aliambiwa asubiri.Bado inatarajiwa kuwa leo serikali itatoa tamko hasa kwa vile Dito alikuwa nje ya kituo chake cha kazi bila "ruhusa" (so they say).Pia habari za kuaminika ni kwamba in the Prado kulikuwa na abiria watatu,mmoja akiwa mwanamama (in itself hiyo inaweza kuwa another skandali kwa vile rumours had it kuwa huyo mwanamama ni mke wa mtu).
Reactions za wananchi ziko mixed.Wapo wanaomhurumia Dito kwa vile he was just like another bloke next door na wanashindwa kuelewa nini kilimpelekea kufanya alichofanya.Lakini wengine wanaliangalia suala hilo kwa mtizamo wa kitabaka:vigogo dhidi ya walalahoi,na hao ndio wanataka sheria ichukue mkondo wake regardless of Dito's social and political status.
One important point to note: Dito ndiye alikuwa best man wa JK kwenye harusi yake na Salma.You can imagine jinsi gani mtihani huu ulivyo mgumu kwa world traveller wetu JK.Pengine Mungu hajachoka kumpa mitihani:)
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom