Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 8,166
- 11,569
Mathalani umeomba kazi ya kukuongezea kipato, umeomba mkopo benki au kausha damu, umeomba kura kwenye uchaguzi, umeomba ruhusa kazini au shuleni, umeomba urafiki wa kike au wa kiume, umeomba uchumba au ndoa nakadhalika. Uelewa na Ufahamu wako ukijitosheleza basi utajikuta unajiandaa vizuri sana kupokea matokeo yote yatakayo kuja, ambayo ni aidha kukubaliwa, kukataliwa au kusubirishwa, kwasabb ombi linaweza kukubaliwa, kukataliwa au kusubirishwa.
Na ipo siri moja tu ya kutojiskia vibaya endapo utakataliwa, kunyimwa au kusubirishwa ulichokiomba. Nayo ni Uelewa na ufahamu wa kutosha juu ya jambo lenyewe unaloomba.
Na ili ukomae na uimarike vizuri zaid katika hali hiyo na uione kama sehemu ya maisha yako, ni lazima kukataliwa, kunyimwa au kusubirishwa mara nyingi zaidi.
Na hapo ndipo utakua jasiri zaidi, hodari na mzoefu zaid wa kukataliwa, kunyimwa au kusubirishwa na kwahivyo hautakua ukijiskia vibaya ukinyimwa, ukikataliwa, au kusubirishwa chochote popote.
Sasa sikuizi vijana wakikataana au kusubirishana kidogo tu mathalani kwenye mahusianao, asi, matokeo yake wanadungana visu, wanachinjana, wanakunywa sumu au kujinyonga.
Hii inasababishwa zaidi na kutokua na uelewa na ufahamu mpana na wa kutosha juu ya walichoombana, kunyimana au kusubirishana, lakini zaidi sana kutokua na uzoefu wa kukataliwa, kunyimwa au kusubirishwa mara nyingi zaidi 🐒
kwahiyo omba mara nyingi zaidi uwezavyo, nyimwa au kataliwa mara nyingi zaidi, subirishwa sana ili hatimae uwe mzoefu na jasiri wa kunyimwa, kukataliwa na kusubirishwa, lakini pia kubaliwa mara chache zaidi ili uinjoy raha ya kukubaliwa.
Ukikua utalewa 🐒