Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,055
Kuwekeana mipaka kwenye ulaji ni jambo la hekima, lakini kuwekeana ukomo kwenye kujitolea ni ama kukosa uelewa, kukosa maarifa, au anayetaka hilo liwepo ni mnafiki, ana dhamira mbaya.
Kuweka ukomo wa muda wa uongozi ndani ya CCM na ndani ya Serikali, ni jambo la muhimu sana. Uongozi ndani ya CCM na ndani ya Serikali, ni ulaji. Kwenye ulaji ni lazima na ni muhimu kuwekeana ukomo. La sivyo waliokaa kuizunguka meza iliyojaa vyakula vya kila aina hawataondoka.
Uongozi ndani ya vyama vya upinzani ni mateso, ni kujitolea, ni kujitoa sadaka na wakati fulani ni kuwa tayari kufa kwaajili ya kutetea kile unachokiamini. Ni wangapi wanaweza kupigania kwenda jela? Ni wangapi wanaweza kupigania kushambuliwa kwa risasi? Ni wangapi wanaweza kupigania kufilisiwa?
Huwezi kuweka ukomo wa mtu kujitolea. Huwezi kuweka ukomo wa mtu kujitolea maisha yake kwaajili ya watu wengine. Kwenye kujitolea, mara nyingi watu huishia kumbembeleza mtu fulani awe kiongozi wao, au aliyekuwa kiongozi aendelee kuwa kiongozi.
Kuna watu, kwa unafiki tu, wanataka kulinganisha uongozi ndani ya chama cha upinzani CHADEMA ni sawa na uongozi ndani ya CCM, chama dola, chama tawala na chama maslahi.
Ukiwa kiongozi ndani ya CCM tayari umevaa ngao ya kutoshtakiwa hata ukitenda uovu. Tayari umejivika ngao ya kutosumbuliwa na vyombo vya dola, tayari umejivika ngao ya kunyenyekewa na viongozi wa Serikali, tayari umetengeneza mazingira wezeshi ya biashara zako kukua, umepata ticket hata ya kukwepa kodi na usisumbuliwe na TRA, tayari umekaa njiapanda ya kukusanya hongo za wanaogombea uongozi.
Kwa upande mwingine, ukiwa kiongozi wa CHADEMA, umekata ticket ya kubambikiwa kesi, kupelekwa mahakamani na kunyimwa dhamana, umeidhinisha kufilisiwa kwako kwa kubambikiwa kodi kwenye biashara zako, huna uhakika kama utaishi na kufa kwa mapenzi ya Mungu, wewe na ndugu zako kuandamwa na vyombo vya dola.
Nani anayeyatamani haya? Pia inajulikana kuwa CCM inafanya jitihada wakati wote kupandikiza mamluki kwenye uongozi wa CHADEMA ili kuweza kuiua. Kwa ukweli huo, pale unapokuwa na wachache waliojitolea, ambao mna uhakika siyo mamluki, mna uhakika hawarubuniwi wala kusaliti chama, kwa nini wasibembelezwe kuendelea kuwa viongozi kuliko mkaingiza mamluki au wanaorubuniwa na ikawa ndiyo mwisho wa chama?
Kwa sasa kuna watu ambao kwa vyovyote mtu unaweza kusema ndio waliojitolea, iwe mvua iwe jua, yawe mafuriko au tetemeko la ardhi, wanasimama na CHADEMA katika misingi yake ya kutetea na kupigania haki. Na hawa sio wengi. Ngazi za juu:
1. Freeman Mbowe
2. Tundu Lisu
3. John Mnyika
4. Mchungaji Msigwa
5. Mbilinyi Sugu
6. Heche
Katikati na chini, wapo, tena siyo wachache, lakini wanafahamika kwa majina.
CHADEMA, hata siku moja isibebe hoja za wanafiki eti kwa nini chama kina baadhi ya majina kwenye nafasi za uongozi kwa muda mrefu. Lengo la hawa watu, kukiwepo na huo upenyo wa kubadilisha viongozi mara kwa mara, kuna siku wataingiza watu wao waiue CHADEMA. Fikiria kama CHADEMA ingekabidhiwa kwa Mambe, Mzee Lowasa, Halima Mdee au Sumaye, hivi ingekuwepo bado?
Kwenye ulaji tuwekeane ukomo. Kwenye kujitolea, na kwenye kupigania haki hakuna ukomo, japo kiongozi anaweza kuamua kupumzika au wanachama wakaamua kupumzisha. Jambo la muhimu ni kuhakikisha wakati wote chama kipo kwenye uongozi wa mtu jasiri, mkweli, asiye mwoga na aliyejitoa nafsi yake kwaajili ya anachokipigania.