Ukitaka kujua kama unapendwa kweli ugua

Ukitaka kujua kama unapendwa kweli ugua

Sasa unataka mwanamke akukopee hela? Hilo neno limenikata kuendelea kusoma! Tafuten hela Vijana maisha Ni matamu Sana!
We unajua ugonjwa unavyo filisi? We mwili Una ugonjwa utawezaje kuendelea kutafuta pesa au hujawai kuona watu Wanauza Mali kwaajir ya kujitibu au we umekulia vijijin uko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mjinga halafu ni si ajabu huyajui maisha vzr

Unaweza ukaumwa mpk hivyo vihela hela vyake vinavyokupa kibri vikaisha sasa ni nani wakukuonea huruma km sio watu wako wa karibu???

Kaka yangu alifikisha account ya million 220,v8 na ghorofa juu hakuwahi kuona umuhimu wa ndugu hata mmoja leo hii ananipigia simu mimi kuniomba 10,000/- na toka kashika hela ni 8years hajawahi kunipigia simu wala kujua nipo wapi from no where kapiga simu kajitambulisha kaomba 10k.

Kua uyaone, ugonjwa umewashikisha adabu vibri na wajinga km wewe wengi sana na unashikishwa adabu km masihara hivi..
Huyo atakuwa kalelewa kijijni ndani uko hajui watu wamefilisika kwa kutafuta matibabu ya ugonjwa kwa kuuza Mali na kupona hawaja pona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali gani? Wanawake wengi wa kitanzania wana unafiki na ubinafsi wa hali ya juu ndani yao. Hili nimelithibitisha yapata miaka 3 sasa. Wengi wakiumwa wao wanataka kuhudumiwa na kupewa attention na care, ila akiumwa mwanaume hata kukopa hela hataki.

Kuna jamaa yangu alikuwa anaumwa nimem save juzi tu hapa. Alikuwa na mke wake, mke alikuwa mfanyakazi mwenye kipato kizuri. Jamaa alikuws anahitaji 500K kwa ajili ya operation. Mke alikana kata kata kuwa na hela.

Imagine jamaa usiku halali ni kuugulia maumivu tu, analia wakati mwingine kama mtoto. Mbaya zaidi huyu mwanamke aliwahi kuumwa mwaka mzima, aliwahi kulazwa miezi miwili, jamaa alitoa jumla ya 5M ya matibabu. Hapo mke alipata hela special kazini ya likizo ya matibabu ila akaficha.

Huyu jamaa alimpigia ndugu yake amsaidie, ila mke wa huyo ndugu yake naye kamuambia mumewe wana majukumu mengi hivyo asitoe hiyo hela. Imagine mtu anateseka halafu wanapigiana mipira hivi.

Mwisho ikabidi anitafute. Nami bila hiyana nikam save jamaa yangu.

Funzo: mwanaume jijali, jipe raha na ujipende mwenyewe KWANZA. Potelea mbali hata wakikuona mbinafsi. 90+% ya mnaowaita wake zenu ni wabinafsi and they are money oriented.

Inasikitisha. Mke wake amenipigia simu ananishukuru(unafiki tu), jamaa kesho anakwenda kufanya OP.

Nimejifunza hapa. Huyu ni mmoja tu, je, wapo wangapi wanakufa kabisa kutokana na ubinafsi na uchoyo wa wanaowaita wake zao? Jibu unalo.!
Ukiona hivyo ujue jamaa Alikwisha muumiza huyo mke kitambo. Sasa hayo ni matokeo ya maumivu aliyosahau huyo mume
 
Nimeoa mke mbinafsi sana mpaka najuta kwanini... Nilimuoa japo kanpa watoto wawili wazuri ila simtaki na nmemtafutia mbadala wake...pesa yake ni yake tu ukichukua hata miaa lazima irudi atakupigia kelele hata kwa mda wa miezi 6 mfululizo mpka utaitoa
Vizuri.! Kasoma?

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Baadhi ya wanawake,kwakweli wanafikirisha sana,tumshiikishe Mungu katika kuchagua hawa wenzi wetu.Baadhi ya wadada hawana huruma na ni wakatili sana,sijui wana roho za aje?
Nilidhani labda ni IQ tu,kumbe ni ubinafsi na sijui kutukomoa... unakwama lakini mtu huambulii msaada wake,waweza kusaidiwa na rafiki yako lakini siyo baadhi yao hawa.
Yuko radhi hela iende vikoba/ chama lkn asikuudumie wewe na huko wala hadaiwi bali ni kuongeza hisa tu.
 
Nyie si mnasemaga "mwanamke akiwa na akili ya kuvukia barabara tu zinatosha, hizo zingine tutatumia zangu" sasa mbona leo mnaanza kuwalaumu? alisikika mtu mmoja 😆😆
 
Kuna wanawake wana roho ngumu sana. Niliwahi kuwa na mwanamke namjali sana. Kuna.kipindi akaja kaa na mimi, sasa mambo yakawa hayako vizuri. Anaona nahangaika naunga unga tu ili mradi asikose kitu anajua kabisa kuwa mambo sio poa. Lakini ye kimwa. Sasa alikuwa na begi la mgongoni kaliweka kabatin kwangu, asubuhi moja natoka nikawa na shida na beg, nikalichukua kuchek ndani ana kama lak sita, nikaitoa nikaiacha chini ya nguo nikasepa.
Baada ya muda akagundua nmeondoka na bag akapiga simu, umeondoka na bag, nikamjibu najua waswas wako ni pesa ipo chini ya nguo. Akaanza jitetea kuhusu hiyo pesa sijui hivi na vile.
Mimi sikumuuliza nakawa na akili kichwani kuwa huyu sio mtu anayeweza kukusupport.
Aiseee [emoji30][emoji30][emoji30]
 
Duh, kweli wanawake selfish sana, aisee sera yangu kuu mwaka huu na ijayo, ni kuwa "mimi kwanza" miradi na uchumi wangu ndo kipaumbele, sio hawa ngedere ambao shamba likiisha mazao wanahamia kwingine.
[emoji457][emoji457][emoji375][emoji375]
 
Umenikumbusha mbali Mwaka flan kipindi cha homa ya dengue nikiwa mitaa ya Uhasibu niliumwa Ule ugonjwa vbaya mno kutembea siwezi kichwa Sina nguvu Yani siwez Fanya chchte Hapo nilipitisha siku nzma sijala nimelala tu kama mfu Kuna Huyo manzi yangu nikamwomba anisaidie japo matunda aniletee akadai Hana hela nkamwambia njoo hela nakupa akakataa katakata halaf jioni ananiambia kamsindikiza rafiki yake karume kununua vitu, aisee niliumia Sana Ila nilimchezea mchezo uliomuumiza Sana kisaikolojia.
Ulimpiga tukio gani ,?? Tuhadithie hapa tupate Cha kujifunza
 
Back
Top Bottom