Ukitaka kujua kama unapendwa kweli ugua

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
3,979
5,295
Hali gani? Wanawake wengi wa kitanzania wana unafiki na ubinafsi wa hali ya juu ndani yao. Hili nimelithibitisha yapata miaka 3 sasa. Wengi wakiumwa wao wanataka kuhudumiwa na kupewa attention na care, ila akiumwa mwanaume hata kukopa hela hataki.

Kuna jamaa yangu alikuwa anaumwa nimem save juzi tu hapa. Alikuwa na mke wake, mke alikuwa mfanyakazi mwenye kipato kizuri. Jamaa alikuws anahitaji 500K kwa ajili ya operation. Mke alikana kata kata kuwa na hela.

Imagine jamaa usiku halali ni kuugulia maumivu tu, analia wakati mwingine kama mtoto. Mbaya zaidi huyu mwanamke aliwahi kuumwa mwaka mzima, aliwahi kulazwa miezi miwili, jamaa alitoa jumla ya 5M ya matibabu. Hapo mke alipata hela special kazini ya likizo ya matibabu ila akaficha.

Huyu jamaa alimpigia ndugu yake amsaidie, ila mke wa huyo ndugu yake naye kamuambia mumewe wana majukumu mengi hivyo asitoe hiyo hela. Imagine mtu anateseka halafu wanapigiana mipira hivi.

Mwisho ikabidi anitafute. Nami bila hiyana nikam save jamaa yangu.

Funzo: mwanaume jijali, jipe raha na ujipende mwenyewe KWANZA. Potelea mbali hata wakikuona mbinafsi. 90+% ya mnaowaita wake zenu ni wabinafsi and they are money oriented.

Inasikitisha. Mke wake amenipigia simu ananishukuru(unafiki tu), jamaa kesho anakwenda kufanya OP.

Nimejifunza hapa. Huyu ni mmoja tu, je, wapo wangapi wanakufa kabisa kutokana na ubinafsi na uchoyo wa wanaowaita wake zao? Jibu unalo.!
 
Cha kwanza umwa, cha pili mkeo/mpenzio apate pesa za ghafla nyingi na wewe huna pesa, kwenye kuumwa hilo sitaongelea, ila kwenye pesa, kuna familia moja ivi walikuwa wanaishi kwa kipato cha mwanaume, uchumi ukayumba kidogo, mwanamke upande wa familia yao wakauza nyumba wakapata milioni nyingi.

Akapata mgao kwenye akaunti yake, mengi yalibadilika hadi ilibidi tuingilie kati kuweka mambo sawa, mwanamke akipata hela kama hana Mungu na wewe hauna pesa, umeshamkosa, au la, hadi watoto wako watakudharau.
 
Cha kwanza umwa, cha pili mkeo/mpenzio apate pesa za ghafla nyingi na wewe huna pesa, kwenye kuumwa hilo sitaongelea, ila kwenye pesa, kuna familia moja ivi walikuwa wanaishi kwa kipato cha mwanaume, uchumi ukayumba kidogo, mwanamke upande wa familia yao wakauza nyumba wakapata milioni nyingi.

Akapata mgao kwenye akaunti yake, mengi yalibadilika hadi ilibidi tuingilie kati kuweka mambo sawa, mwanamke akipata hela kama hana Mungu na wewe hauna pesa, umeshamkosa, au la, hadi watoto wako watakudharau.
Kabisa.
 
mkuu, shukuru Mungu na omba Mungu aendelee kuwa hivyoohivyo, wanawake wote ubongo wao ni uleule, wanatofautiana kulingana na mazingira waliyopo tu na imani kwa Mungu kama ipo , ila kama wooote watakuwa mazingira mamoja, kuna uwezekano wote wakawa na tabia sawa.
Kabisa. Umwa ujue.
 
mleta mada amesahau kitu kimoja, "umwa kwa muda mrefu"sio umwa muda mfupi, umwa muda mrefu ndio utaona subira ya upande wa pili. hii kuumwa kidogo tu hii, mtu anaweza kufake.
Kabisa, ahsante kwa kunikumbusha. Ukiumwa muda mrefu kikubwa atakuletea dharau ili muachane, atakuwa tayari kukutelekeza ndani pasi msaada wowote, umwa hata kwa miezi minne tu utajua uhalisi wa dunia hii.
 
Oa mwanamke anayekupenda,
Wanaume wengi wanawashawishi kwa mali, wadhifa n.k ili kuwawin wanwake waingie nao kwenye ndoa na kuwamiliki pasipo kutengeneza mazingira ya kumfanya mwanamke akupende
 
Wanaume huwa mnajichanganya tu unamkuta mwanaume kang'ang'ania asikopendwa yaan dalili zote za mateso huko mbele anaziona lakini anapuuzia{sijui huwa mnarogwa},,mara nyingi matokeo yake ndo hayo unakuta mtu hata hakujali anakuona wa kazi gani.

Binafsi huyu kaka akipata hata mafua nachanganyikiwa mimi pia nikiugua namuona anavyohaha.Ni kumuomba tu Mungu akupe anayekupenda na umpende pia
 
Back
Top Bottom