Ukitaka kujua kama unapendwa kweli ugua

Ukitaka kujua kama unapendwa kweli ugua

Mwanaume una Mungu tuu kama Kimbilio lako na wewe Mwenyewe .
Mungu “asipokusaidia” mwambie achukue roho yako.
Onyo: Don’t take your life as a Man.
Mwanaume kamili anajipenda na kujithamini, hashindani na Uke wa Mwanamke hadi anatoa mijasho, yeye anajiburudisha yeye tuu Mwanamke ni second na tegemeo lake ni Mungu na miguu yake miwili, nje ya hapo bora afe kwa kukonda hata mbavu zionekane zote.

Be a man even when dying!

Mkuu bado kuna vijana watakubishia....
 
Hali gani? Wanawake wengi wa kitanzania wana unafiki na ubinafsi wa hali ya juu ndani yao. Hili nimelithibitisha yapata miaka 3 sasa. Wengi wakiumwa wao wanataka kuhudumiwa na kupewa attention na care, ila akiumwa mwanaume hata kukopa hela hataki.

Kuna jamaa yangu alikuwa anaumwa nimem save juzi tu hapa. Alikuwa na mke wake, mke alikuwa mfanyakazi mwenye kipato kizuri. Jamaa alikuws anahitaji 500K kwa ajili ya operation. Mke alikana kata kata kuwa na hela.

Imagine jamaa usiku halali ni kuugulia maumivu tu, analia wakati mwingine kama mtoto. Mbaya zaidi huyu mwanamke aliwahi kuumwa mwaka mzima, aliwahi kulazwa miezi miwili, jamaa alitoa jumla ya 5M ya matibabu. Hapo mke alipata hela special kazini ya likizo ya matibabu ila akaficha.

Huyu jamaa alimpigia ndugu yake amsaidie, ila mke wa huyo ndugu yake naye kamuambia mumewe wana majukumu mengi hivyo asitoe hiyo hela. Imagine mtu anateseka halafu wanapigiana mipira hivi.

Mwisho ikabidi anitafute. Nami bila hiyana nikam save jamaa yangu.

Funzo: mwanaume jijali, jipe raha na ujipende mwenyewe KWANZA. Potelea mbali hata wakikuona mbinafsi. 90+% ya mnaowaita wake zenu ni wabinafsi and they are money oriented.

Inasikitisha. Mke wake amenipigia simu ananishukuru(unafiki tu), jamaa kesho anakwenda kufanya OP.

Nimejifunza hapa. Huyu ni mmoja tu, je, wapo wangapi wanakufa kabisa kutokana na ubinafsi na uchoyo wa wanaowaita wake zao? Jibu unalo.!
Nime screenshot, nitaprint niiweke sebuleni kwa faida ya kila atakayekuja kwangu.
 
Umenikumbusha mbali Mwaka flan kipindi cha homa ya dengue nikiwa mitaa ya Uhasibu niliumwa Ule ugonjwa vbaya mno kutembea siwezi kichwa Sina nguvu Yani siwez Fanya chchte Hapo nilipitisha siku nzma sijala nimelala tu kama mfu Kuna Huyo manzi yangu nikamwomba anisaidie japo matunda aniletee akadai Hana hela nkamwambia njoo hela nakupa akakataa katakata halaf jioni ananiambia kamsindikiza rafiki yake karume kununua vitu, aisee niliumia Sana Ila nilimchezea mchezo uliomuumiza Sana kisaikolojia.
Kuna wanaume wanapata wanawake wavumilivu na wenye upendo wa dhati lakini wanawatenda vibaya mno. Mimi nilikuwa na ndugu yangu maisha yalimpiga akakimbiwa na mwanamke wake . Huyu jamaa alimnunulia huyu dada hadi gari. Huyo mwanamke yeye walitengana na mume wake wakawa wanaishi na mume wake nyumba moja huku wametengana vyumba. Ndugu yangu akaanzisha uhusiano na yule mama. Akawa anamsaidia hadi kesi yake mahakamani. Jamaa biashara zake zilivyoyumba huyo mama akawa hana habari naye. Huyo ndugu yangu akaachana na huyo mama. Huyo mama akachukua kila kitu cha ndani akamuachia kitanda na godoro. Jamaa akaenda kupanga chumba na sebule akawa anaishi na mwanae. Akapata dada mmoja wakawa wapenzi. Jamaa kipindi cha corona ile ya kwanza akaumwa na mwanae ile serious, jamaa akawa hana hela hata ya kununua dawa. Dada wa watu akajitoa muhanga kununua dawa na matunda etc mpaka wakapona . Ilichukua mwezi ndio wanapona. Jamaa kapata vihela kidogo karudiana na yule mama na kumuacha yule mwanamke bila sababu. Ghafla akakata mawasiliano.
 
Wanaume huwa mnajichanganya tu unamkuta mwanaume kang'ang'ania asikopendwa yaan dalili zote za mateso huko mbele anaziona lakini anapuuzia{sijui huwa mnarogwa},,mara nyingi matokeo yake ndo hayo unakuta mtu hata hakujali anakuona wa kazi gani.

Binafsi huyu kaka akipata hata mafua nachanganyikiwa mimi pia nikiugua namuona anavyohaha.Ni kumuomba tu Mungu akupe anayekupenda na umpende pia
Tatizo jingine wanaume wanajivunia usaliti, kuwa na michepuko nje ya ndoa wanaona ni ujanja kwao na urijali, wanasahau wake zao ni binadamu na wanamaumivu pia sana.sometimes mchepuko ukimkoleza vizuri anaanza dharau, kuchelewa kurudi nyumbani na vituko mbalimbali kwa mke wake.

Iko hivi hata kama mwanamke alikupenda kiasi gani upendo huwa unapungua automatically, na siku ukipata shida kama kufilisika au ugonjwa ukaanza kurudi kwa mkeo unakuwa umeshachelewa mkeo alishakutoa moyoni zamani na chuki, maumivu yamemtawala anaona hata ukifa ni sawa tu labda itampunguzia maumivu ya usaliti,dharau na tabia chafu unazozifanya ukijisifu eti ni urijali.

Tuna mioyo na sisi, na usiombe mwanamke alipenda sana akabadilika my friend umeisha. Mwanamke anaweza hata kukua huku anakuchekea.
 
Aisee hiyo ni roho ngumu mno, yaani mume aumwe niwe na pesa nisimpe ili atibiwe mmh , utakua na furaha gani na pesa zako huku babe,mpenzi,mkata kiu wako akiugulia maumivu?[emoji19]. Yanauzwaga hadi mashamba ili mgonjwa atibiwe akipona tutatafuta vingine.

Note: ni tabia ya mtu tu haina uhusiano na ke wote, do not generalize.
Hamna usiseme hivyo, utakuta yeye pesa zake anamalizia kwa makahaba na michepuko yake nje, akipata shida ndo anakumbuka kuna mke, wanawake wanavumilia mengi sana kwenye hizi ndoa jaman, msiangalie upande mmoja tu watu wanaishi kwa maumivu kwa kigezo cha ndoa.
 
Hamna usiseme hivyo, utakuta yeye pesa zake anamalizia kwa makahaba na michepuko yake nje, akipata shida ndo anakumbuka kuna mke, wanawake wanavumilia mengi sana kwenye hizi ndoa jaman, msiangalie upande mmoja tu watu wanaishi kwa maumivu kwa kigezo cha ndoa.
Ni kweli miss ila mtu kuumwa mi naona haina excuse inabidi atibiwe, vipi akifa je? Wewe ukose na hao makahaba wake wakose ndiyo utafurahi?. Mi nadhani ni bora atibiwe akishapona ndiyo umwambie ukweli anachofanya siyo vizuri , hata yeye will feel guilty kwamba pamoja na yote aliyokufanyia but still ulikua naye bega kwa bega kwenye matibabu, atakuheshimu.
 
Tatizo jingine wanaume wanajivunia usaliti, kuwa na michepuko nje ya ndoa wanaona ni ujanja kwao na urijali, wanasahau wake zao ni binadamu na wanamaumivu pia sana.sometimes mchepuko ukimkoleza vizuri anaanza dharau, kuchelewa kurudi nyumbani na vituko mbalimbali kwa mke wake.

Iko hivi hata kama mwanamke alikupenda kiasi gani upendo huwa unapungua automatically, na siku ukipata shida kama kufilisika au ugonjwa ukaanza kurudi kwa mkeo unakuwa umeshachelewa mkeo alishakutoa moyoni zamani na chuki, maumivu yamemtawala anaona hata ukifa ni sawa tu labda itampunguzia maumivu ya usaliti,dharau na tabia chafu unazozifanya ukijisifu eti ni urijali.

Tuna mioyo na sisi, na usiombe mwanamke alipenda sana akabadilika my friend umeisha. Mwanamke anaweza hata kukua huku anakuchekea.
Dah kumbe ndio mpo hivyo....aisee wacheni malaya waendelee kuwepo
 
Kweli baadhi ya wanawake ni wa binafsi sna

Mfano kuna bi mkubwa hapa naishi nae yy anakipato na mumewe anakipato lkn anataka tu ela ya mumewe itumike kwenye matumizi ya nyumbani kusomeaha watoto na n.k yeye ya kwake cjui inaendaga wapi kibati anacheza siku kikivunjwa hamna maendeleo miaka nenda rudi

Sasa Mme wake sometimes anazidiwa na majukumu kibaya zaidi anatakiwa akagenge kwao lkn akimwambia bi mkubwa anaanza kulalamika ooh hela hamna huku zake hazionekani
 
Wewe ni mjinga halafu ni si ajabu huyajui maisha vzr

Unaweza ukaumwa mpk hivyo vihela hela vyake vinavyokupa kibri vikaisha sasa ni nani wakukuonea huruma km sio watu wako wa karibu???

Kaka yangu alifikisha account ya million 220,v8 na ghorofa juu hakuwahi kuona umuhimu wa ndugu hata mmoja leo hii ananipigia simu mimi kuniomba 10,000/- na toka kashika hela ni 8years hajawahi kunipigia simu wala kujua nipo wapi from no where kapiga simu kajitambulisha kaomba 10k.

Kua uyaone, ugonjwa umewashikisha adabu vibri na wajinga km wewe wengi sana na unashikishwa adabu km masihara hivi..
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] life bana ...tatizo watu wanajisahau sana
 
Back
Top Bottom